Tetesi za soka Ulaya: Vilabu vinne vinamfukuzia Myles Lewis-Skelly

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton, Fulham, West Ham na Nottingham Forest wanamfuatilia beki wa pembeni wa Arsenal, Myles Lewis-Skelly, baada ya kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Thomas Tuchel, kusema kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 anahitaji kupata muda zaidi wa kucheza ili kupata nafasi katika kikosi chake. (Caught Offside)
Arsenal bado hawajaanza mazungumzo na kocha Mikel Arteta kuhusu mkataba mpya, huku Mspaniola huyo akiwa atabaki na miezi 18 kwenye mkataba wake ifikapo mwanzo wa mwaka mpya. (ESPN), external
Manchester United wamejiunga na vilabu kama Real Madrid, Barcelona, Paris St-Germain na Bayern Munich katika mbio za kumsajili kiungo wa Kijerumani mwenye umri wa miaka 16, Kennet Eichhorn, ambaye ana kipengele cha kuuzwa kwa kati ya £8.8m hadi £10.5m (euro milioni 10 hadi 12) na klabu yake ya Hertha Berlin. (Florian Plettenberg)
Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, yuko tayari kumbakisha kiungo wa Brazil Casemiro katika timu jiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa msimu, ili mradi tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 akubali kupunguziwa mshahara. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Matumaini ya Borussia Dortmund ya kumbakiza beki Nico Schlotterbeck yanazidi kupungua kufuatia nia ya Bayern Munich na Liverpool, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 25 akiwa hafurahishi na namna timu yake inavyocheza (Bild Plus via Get German Football News).
Vilabu kadhaa vya ligi kuu England vinavutiwa na mpango wa kumrudisha mshambuliaji wa Uingereza na Al-Ahli, Ivan Toney, mwenye umri wa miaka 29, katika ligi kuu hiyo, lakini mshahara wake mkubwa unaweza kuwa kikwazo. (Sky Sports)
Tottenham ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia mshambuliaji huyo wa zamani wa Brentford, Toney, lakini wanaangalia soko linavyokwenda wakati huu wakipanga kusajili mshambuliaji mpya Januari. (Teamtalk), external
Manchester United wanataka kumsajili kiungo mpya mwezi Januari na wameorodhesha machaguo sita, yakiwemo majina matatu ya Waingereza: Conor Gallagher wa Atletico Madrid (miaka 25), Adam Wharton wa Crystal Palace (miaka 21), na Elliot Anderson wa Nottingham Forest (miaka 23). (Fichajes - in Spanish).

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham wanapanga kumpa kocha wao Marco Silva mkataba mpya licha ya kuanza msimu vibaya katika uwanja wa Craven Cottage. (The I)
Everton wanataka kumsajili mshambuliaji mpya katika dirisha la Januari, na mshambuliaji wa Uholanzi wa Manchester United, Joshua Zirkzee (miaka 24), akiwa miongoni mwa wanaowafukuzia. (Sky Sports), external
Mshambuliaji wa Ujerumani na West ham Niclas Fullkrug (miaka 32), amepewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha la Januari. (GiveMeSport),
Chelsea wanataka kumpa kiungo wa Ecuador, Moises Caicedo (miaka 24), mkataba mpya kama zawadi kwa kiwango chake bora msimu huu. (Sky Sports)
Aliyekuwa kocha wa Manchester United, Erik ten Hag, amekataa nafasi ya kuwa kocha mpya wa Ajax. (NOS - in Dutch)














