Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia 2022: Khazri ana matumaini Tunisia itaweka historia
Nahodha Wahbi Khazri anaamini kuwa Tunisia ina ubora wa kuifanya iwe mara ya sita kuwa na bahati kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar.
Wenyeji hao wa Afrika Kaskazini wamekumbana na matatizo ya kutolewa katika makundi katika mechi zote tano za awali na wanajivunia ushindi mara mbili pekee katika michezo 15 - ya kwanza dhidi ya Mexico mwaka 1978 na kisha dhidi ya Panama 2018.
Kwa mara nyingine tena wakilenga kutinga hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza, Khazri ana imani ya kuanza vyema dhidi ya Denmark na Australia kutokana na mechi yao ya mwisho ya Kundi D dhidi ya mabingwa Ufaransa.
"Naamini tunaweza kufanikiwa. Tuna timu nzuri ambayo imekuwa pamoja kwa muda mrefu," Khazri aliiambia BBC Michezo, Afrika.
"Ufaransa ni bora kuliko sisi na wanashindania taji, Denmark ni timu nzuri na Australia pia. Nadhani tuna nafasi ya kucheza katika raundi inayofuata na tutalazimika kuwa na ufanisi katika michezo miwili ya kwanza. Kabla ya Kombe la Dunia lililopita nchini Urusi, tulicheza vyema dhidi ya Uhispania na Ureno, kisha tukashinda Croatia mwaka mmoja baada ya kumaliza kama washindi wa pili."
"Tuna uwezo wa kucheza dhidi ya timu kubwa. Itakuwa ndoto iliyotimia kufika raundi ya pili."
Tunisia iliingia kwenye vichwa vya habari iliposhinda taji la mataifa manne ya Kombe la Kirin mwezi Juni, ikikutana na Chile na wenyeji Japan, kabla ya kuwalaza Comoro 1-0 na kufungwa 5-1 na Brazil katika mechi za kujiandaa kwa Kombe la Dunia Septemba.
Khazri anasema mchuano huo na washindi mara tano wa Kombe la Dunia Brazil ulikuwa wa manufaa, licha ya kushindwa vibaya.
"Ilikuwa muhimu kujipima dhidi ya timu kubwa kwa sababu kwenye Kombe la Dunia utakutana na walio bora pekee," kiungo wa kati wa Montpellier alisema.
"Ilituruhusu kujua tunachokosa, na kujifunza mambo muhimu kuhusu kile tunachoweza kuboresha."
Inahitaji zaidi ya bahati wakati ikielekea Qatar
Tunisia iliepuka washindi wa juu wa Afrika katika raundi ya mchujo ya Machi, lakini nchi hiyo ya mabingwa barani wa mwaka 2004 bado waliishinda Mali na kufanikiwa kufika katika Kombe la Dunia mara ya pili.
Ushindi wa jumla wa 1-0 wa Kocha Jalel Kadri ulitokana na bao la kujifunga kwenye mechi ya kwanza nchini Mali na beki Moussa Sissako, ambaye alitolewa nje muda mfupi baadaye.
Kutokana na kundi lao gumu nchini Qatar, Tunisia huenda ikahitaji zaidi ya bahati ili kutinga hatua ya 16 bora.
Bingwa mtetezi Ufaransa wanajivunia safu ya ushambuliaji ya kutisha akiwemo Kylian Mbappe na mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or Karim Benzema, huku Denmark wakiwasukuma wenyeji England kwa nguvu katika michuano ya Mabingwa wa Ulaya mwaka jana kwenye nusu fainali.
"Denmark ina timu kubwa yenye wachezaji wenye vipaji, na Christian Eriksen yuko katika hali nzuri. Waliiondoa Ufaransa katika Ligi ya Mataifa," Khazri alisema.
Kiuhalisia, nafasi ya Tunisia kunyakua ushindi wao wa tatu dhidi ya mechi katika Kombe la Dunia inaweza kuja dhidi ya Australia, ambao wako nafasi nane chini yao katika viwango vya ubora wa dunia wakiwa katika nafasi ya 38.
"Ni vigumu kuzungumza kuhusu Australia kwa sababu sikutazama michezo zao nyingi," Khazri alikiri.
"Lakini hakuna michuano rahisi katika aina hii ya mashindano, iwe ni Ufaransa, Australia au Denmark. Tutakuwa na mtazamo sawa kwa mechi hizo tatu."
‘Mechi dhidi ya Les Bleus itakuwa ya hisia’
Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa kabla ya kuchagua nchi ya baba yake, Khazri mzaliwa wa Corsica ametumia maisha yake yote ya uchezaji nchini Ufaransa, miaka miwili akiwa Sunderland (2016-18).
Huku Tunisia ikiwa koloni la Ufaransa kuanzia miaka ya 1880 hadi uhuru wake mnamo 1956, kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 anafurahia pambano lao la Novemba 30 kwenye Uwanja wa Education City.
"Kuzaliwa Ufaransa na kuichezea Tunisia ni maalum - nchi hizi mbili ziko karibu sana na itakuwa wakati wa kusisimua," alisema.
"Tukicheza katika ligi ya Ufaransa pia, tunajua watu wengi watakuwa wakitazama na tutakuwa tukicheza dhidi ya wachezaji bora zaidi duniani, kama Benzema, Mbappe na [Antoine] Griezmann. Itatubidi kucheza mchuano huu kwa ukamilifu na uwe bila majuto.
"Itakuwa na hisia nyingi na inawezekana kwamba kufuzu kwetu kutaamuliwa katika mechi hii.
"Hakutakuwa na uaminifu uliogawanyika nyumbani kwani kila mtu atakuwa 100% Mtunisia upande wangu. Natumai itakuwa vyema kwetu."
Kumbukumbu za 2018
Tunisia na Khazri wanarejea kwenye fainali za Kombe la Dunia baada ya kile anachokiita "ndoto kutimia" wakati alipocheza mwaka 2018 nchini Urusi.
Hata hivyo, kikosi hicho hakikuweza kutafsiri hisia zao za juu katika matokeo ya mapema, kwa kushindwa kwa 2-1 na Uingereza kwa 2-1 na kuchapwa 5-2 na Ubelgiji kabla ya ushindi wa kihistoria wa 2-1 dhidi ya Panama.
"Tulikabiliana na timu ambazo zilikuwa juu yetu," Khazri alisema.
"Tuna majuto juu ya mchezo wa England wakati Harry Kane alifunga dakika ya mwisho, kwa sababu dhidi ya timu kama hiyo kosa lolote dogo litaadhibiwa.
"Lazima tuchukue uzoefu wa Urusi kwa sababu bado tuna baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha sasa.
"Hatutarudia kosa lile lile la kumwacha mchezaji kama Kane bila upinzani."
Khazri ameichezea Tunisia mechi 71, ikishiriki michuano mitano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na amefunga mabao 24 ya kimataifa.
Baada ya kufunga dhidi ya Ubelgiji na Panama miaka minne. zilizopita, Khazri pia alikua mfungaji bora wa nchi yake kwenye Kombe la Dunia.
"Sikutarajia kufunga kwenye Kombe la Dunia".
"Tayari nilikuwa nimetosheka kwa kuwa Urusi kwa sababu nilipata majeraha kabla ya michuano hiyo na nilikuwa na mashaka juu ya uimara wangu,” alisema.
“Niliweza kucheza kwa asilimia 100, nikafunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao".
"Nilikuwa na ufanisi dhidi ya wachezaji bora zaidi duniani, kwa hivyo nilifurahi kutimiza ndoto yangu kwa kucheza na pia kufunga huko."
Sasa anatumai kutumia vizuri nafasi iliyo mbele yake huko Qatar.
"Huwezi kujua pengine hii inaweza kuwa Kombe la Dunia la mara ya mwisho" alisema.
"Natumai timu yangu na mimi tutafika katika hali nzuri kwa sababu tuna uwezo wa kufanya mambo makubwa wakati kila mtu yuko 200%".