Ujasusi, uharibifu na hujuma: Jinsi Urusi inavyotumia "meli za mizimu" kukwepa vikwazo vya Magharibi

Meli ya doria HSwMS Carlskrona inafuatilia meli ya mizigo karibu na pwani ya Uswidi, kama sehemu ya ujumbe wa NATO wa Baltiki ya Sentinel.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Meli ya doria HSwMS Carlskrona inafuatilia meli ya mizigo karibu na pwani ya Uswidi, kama sehemu ya ujumbe wa NATO wa Baltiki ya Sentinel.
    • Author, Alexey Kalmykov
    • Nafasi, Ripota wa kiuchumi idhaa ya BBC Urusi
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Kremlin imesema Urusi "haiathiriki" na vikwazo vipya vya Rais wa Marekani Donald Trump, ambavyo vimeorodhesha kampuni mbili kubwa zaidi za mafuta za Urusi.

Hata hivyo, kinachoendeleza biashara ya mafuta ya Urusi ni "msururu wa meli za kivuli" – meli za mizimu na "meli za kidubwana" zinazobeba mamilioni ya mapipa ya mafuta ghafi, zikisafirisha kwa siri kwa wanunuzi duniani kote wanaotafuta bei nafuu na hivyo kukwepa vikwazo.

Meli hizi pia huhudumia wateja wengine kama vile viongozi wa kidini wa Iran, majenerali wa Venezuela, na hata wafanyabiashara wa Magharibi wasio waaminifu wanaoweka faida mbele ya usalama wa mazingira, au hata maisha ya mabaharia wanaotelekezwa baharini kwa miezi au miaka.

Shughuli za meli hizi za siri zimeongezeka kwa kasi tangu uvamizi wa Ukraine mwaka 2022, huku mfaidikaji mkuu akiwa utawala wa Putin.

Urusi inazitumia sio tu kusafirisha kwa magendo bidhaa yake kuu ya mauzo – mafuta – na hivyo kufadhili "mashine yake ya vita," bali pia kwa shughuli za "mseto" za ujasusi na uharibifu dhidi ya nchi wanachama wa NATO barani Ulaya, ikiwemo miundombinu ya kebo za chini ya bahari na mabomba ya gesi.

Kwa mujibu wa wachambuzi, meli za "mizimu" sasa zinabeba takriban asilimia 80% ya mauzo ya mafuta ya Urusi kwa njia ya bahari, zikipuuza vikwazo vya Magharibi.

Kulingana na makadirio ya wachambuzi, meli ya "mzimu" kwa sasa inasafirisha 80% ya mauzo ya mafuta ya baharini ya Urusi, na kukaidi vikwazo vya Magharibi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kulingana na makadirio ya wachambuzi, meli ya "mzimu" kwa sasa inasafirisha 80% ya mauzo ya mafuta ya baharini ya Urusi, na kukaidi vikwazo vya Magharibi.

Urusi ni miongoni mwa wauzaji wakubwa watatu wa mafuta duniani, ikishirikiana nafasi hiyo na Marekani na Saudi Arabia.

Mnamo 2024, Urusi ilizalisha karibu asilimia 10% ya mafuta yote duniani.

Kabla ya vita vya Ukraine, karibu mauzo yote ya mafuta ya Urusi baharini yalifanywa na meli za Magharibi, hasa za Wagiriki, huku shughuli za kibiashara zikiendeshwa Uswisi na bima ikitolewa London.

Lakini sasa, takribani meli nne kati ya tano zinazobeba mafuta ya Urusi hazina bima inayotambuliwa na makampuni makubwa ya kimataifa ya bima ya baharini.

Benjamin Hilgenstock, mchumi mkuu wa Taasisi ya kiuchumi ya chuo cha Kyiv, anasema:

"Urusi imeunda meli mbadala ya mafuta inayoiwezesha kukwepa vikwazo. Lakini meli hizo ni za zamani, hazina matengenezo sahihi na hazina bima ya kutosha dhidi ya ajali za mafuta. Zaidi ya robo tatu ya mauzo hayo hupitia Bahari ya Baltiki na Bahari Nyeusi – hivyo kuvuka maji ya Ulaya kila siku."

Meli chovu chini ya bendera zisizojulikana

Kulingana na takwimu za S&P Global, karibu meli moja kati ya tano baharini ni sehemu ya meli hii ya siri, meli zenye kutu, zikipiga mbizi chini ya bendera zisizo na jina, zikisafirisha mafuta kutoka nchi zilizo chini ya vikwazo.

Mafuta mengi ya Irani husafirishwa hadi vituo kama hiki, katika mkoa wa Shandong nchini China.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mafuta mengi ya Irani husafirishwa hadi vituo kama hiki, katika mkoa wa Shandong nchini China.

Nusu ya meli hizi hubeba mafuta ya Urusi pekee, asilimia 20 ya Iran, asilimia 10 ya Venezuela, huku zilizobaki zikiwa mchanganyiko wa mafuta kutoka nchi zaidi ya moja.

Wateja wakubwa wa mafuta haya ni India na China, nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu na watumiaji wakuu wa mafuta duniani.

Wanunuzi wadogo ni pamoja na Uturuki, Singapore na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Pia unaweza kusoma:
"Meli za vidambwana" hutoa nambari za kipekee za usajili za Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini za kweli zilizotolewa kwa meli zinazolengwa kufutwa.

Chanzo cha picha, Corbis via Getty Images

Maelezo ya picha, "Meli za vidambwana" hutoa nambari za kipekee za usajili za Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini za kweli zilizotolewa kwa meli zinazolengwa kufutwa.

Ili kuficha nyayo zao, meli hizi:

  • Hufanya uhamisho wa mafuta kutoka meli hadi meli baharini, mbali na uangalizi wa mamlaka za bandari;
  • Huzima au hubadilisha taarifa za mfumo wa utambulisho wa kiotomatiki (AIS) ili kuficha eneo halisi;
  • Hubadilisha majina na bendera mara kwa mara, au hata kusafiri bila bendera;
  • Hutumia nambari za usajili za meli zilizopangwa kutupwa, kana kwamba zimepata "utambulisho wa wafu."

Kampuni ya Windward inakadiria kuwa idadi ya meli zenye bendera bandia imeongezeka kwa asilimia 65 katika miezi minane ya kwanza ya 2025, na sasa mtandao huu unahusisha zaidi ya meli 1,300.

'Meli ya mizimu' sasa ina meli 1,300, kulingana na makadirio kutoka kwa kampuni ya uchambuzi wa baharini ya Windward.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, 'Meli ya mizimu' sasa ina meli 1,300, kulingana na makadirio kutoka kwa kampuni ya uchambuzi wa baharini ya Windward.

Huduma za usajili wa bendera pia zimeshamiri.

Nyingi ni matapeli tu. Na wakati zingine ni za kisheria, nchi zinazotoa ni mpya kwa sekta hii na hazina nia au uwezo wa kufuatilia matumizi ya bendera zao.

"Kulingana na kanuni za kimataifa za usafiri wa baharini, Mataifa ya bendera yana jukumu la kuhakikisha kufuata viwango vya kiufundi na kwamba bima ya umwagikaji wa mafuta inatosha," Hilgenstock anasema.

"Walakini, linapokuja suala la meli za Urusi, tunazungumza juu ya mamlaka ambayo haiwezi kuaminiwa kutekeleza kazi hii," anaongeza.

Tishio jipya kwa usalama wa dunia

Oktoba 2025, meli moja iliyokuwa ikibeba bendera ya Benin, Boracay (zamani ikijulikana kama Pushpa, Odysseus, Varuna na Kiwala), ilikamatwa karibu na pwani ya Ufaransa kwa tuhuma za kutumika kama kituo cha kurushia ndege zisizo na rubani (drones) zilizozua taharuki katika viwanja vya ndege vya Denmark.

Stéphane Kellenberger, mwendesha mashtaka huko Brest, aliiambia Agence France-Presse kwamba kukamatwa huko kulitokana na wafanyakazi kukataa kutoa ushirikiano kwa sababu hawakuweza kuhalalisha uraia wa meli hiyo.

Hii ni Boracay, ambayo ndiyo imebadilisha jina lake la awali, ambalo lilikuwa Pushpa - liliitwa pia Odysseus, Varuna na Kiwala - na ambalo lilipeperusha bendera saba tofauti kwa wakati.

Boracay, ambayo imebadilisha jina lake la awali, ambalo lilikuwa Pushpa, pia imekuwa Odysseus, Varuna na Kiwala, na imepeperusha bendera saba tofauti.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Boracay, ambayo imebadilisha jina lake la awali, ambalo lilikuwa Pushpa, pia imekuwa Odysseus, Varuna na Kiwala, na imepeperusha bendera saba tofauti.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakati inakamatwa, meli hiyo ilikuwa inasafirisha mapipa 750,000 ya mafuta kutoka bandari ya Primorsk, karibu na St. Petersburg, kuelekea India.

Tukio hilo lilichochea wasiwasi mkubwa katika nchi za NATO, hasa kufuatia mashambulio ya droni yaliyorekodiwa Sweden, Norway na Ujerumani.

Novemba 6, 2025, uwanja wa ndege wa Brussels ulifungwa kwa muda baada ya kuripotiwa kwa ndege za aina hiyo karibu na kambi ya kijeshi ya Ubelgiji.

Baada ya uchunguzi wa Boracay, NATO ilizindua operesheni Baltic Sentry kufuatilia shughuli za 'meli za mizimu' katika Bahari ya Baltic.

Mataifa kama Uingereza, Denmark, Sweden na Poland yalianza kukagua nyaraka za bima za meli zinazopita kwenye njia kuu za baharini, huku Estonia, Finland, Ujerumani, Latvia, Lithuania, Uholanzi na Norway zikiahidi "kudhoofisha na kuzuia" meli za siri za Urusi kufuatia matukio ya uharibifu wa nyaya na mabomba ya chini ya bahari.

Hata hivyo, uwezo wa nchi hizo kukamata meli hizo ni mdogo, kwa kuwa hatua kama hizo huruhusiwa tu ndani ya maji ya kitaifa (maili 12 kutoka pwani).

Katika maji ya kimataifa, sheria ya "uhuru wa usafiri" inalinda meli hizo, isipokuwa ziwe tishio la moja kwa moja kwa usalama wa taifa.

Wanasiasa wa Urusi wametaka hatua zozote za chuki dhidi ya meli zinazobeba mafuta ya Urusi zichukuliwe kama shambulio dhidi ya Urusi.

Na Estonia ilipojaribu kusimamisha meli ya mafuta iliyokuwa ikisafiri bila bendera kati ya Estonia na Finland mnamo Mei 2025, Moscow ilivamia ndege ya kivita ili kuruka juu yake.

Lakini meli za siri zinaweza kusababisha tishio kubwa zaidi kwa usalama wa kimataifa.

Hatari kubwa kwa mazingira

Kampuni kuu za usafirishaji kwa kawaida hutupa meli ya mafuta baada ya takriban miaka 15 ya huduma. Baada ya miaka 25, kwa ujumla huondolewa.

Hata hivyo, meli katika msururu mmoja wa meli hazikubaliwi kufutwa [kutokana na vikwazo vilivyowekwa kwenye vyombo hivyo].

Mfanyikazi wa kujitolea akimsafisha ndege baada ya meli mbili za mafuta zenye umri wa miaka 50 kumwaga tani 5,000 za mafuta kwenye Mlango-Bahari wa Kerch.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mfanyikazi wa kujitolea akimsafisha ndege baada ya meli mbili za mafuta zenye umri wa miaka 50 kumwaga tani 5,000 za mafuta kwenye Mlango-Bahari wa Kerch.

Desemba 2024, meli mbili kongwe za mafuta za Urusi ziliharibika katika Mlango wa Kerch, zikimwaga zaidi ya tani 5,000 za mafuta baharini tukio lililotajwa na mwanasayansi wa Urusi, Viktor Danilov-Danilyan, kama "janga kubwa zaidi la mazingira katika karne ya 21 nchini humo."

Wakati huo huo, kampuni hewa katika maeneo kama Dubai, nyingi zikifadhiliwa na kampuni za mafuta za Urusi zimekuwa zikinunua meli chakavu na kuzificha kupitia miamala isiyo wazi, hatua inayodhoofisha soko la usafirishaji na kuzuia uwekezaji katika meli mpya.

Kutokana na matengenezo duni na vifaa visivyofanya kazi, meli hizi ni hatari kwa bahari na maisha ya binadamu.

Zikiwa hazina bima, dunia nzima ndiyo inayobeba gharama pale ajali au kumwagika kwa mafuta kunapotokea.

Hata hivyo, biashara hii ya kimagendo inazidi kuwa na faida kubwa.

Kulingana na kampuni ya Xclusiv Shipbrokers, meli ya miaka 15 aina ya Suezmax hugharimu dola milioni 40, lakini safari moja tu ya mwezi mmoja kutoka Bahari Nyeusi hadi India inaweza kumpatia mmiliki wake zaidi ya dola milioni 5.

Wamiliki wa meli hizi wanajaza mifuko yao, huku dunia ikibeba mzigo wa uharibifu wa mazingira na hatari za kiusalama.

Na hata vikwazo vikiondolewa, wachambuzi wanasema meli hizi za mizimu zitaendelea kuwepo zikiibua toleo jipya la biashara ya kimagendo, "Fleet in the Shadow 2.0," kama linavyoripotiwa na jarida maalumu la Lloyd's List.