Picha za kusisimua za tukio la kutawazwa kwa Mfalme Charles III

Mfalme Charles III na Malkia Camilla wametawazwa rasmi, huku umati mkubwa wa watu mjini London na kwingineko kote nchini humo wakisherehekea tukio hilo la kihistoria.

Takriban wanajeshi 7,000 wa jeshi la Uingereza walishiriki katika kile Wizara ya Ulinzi ilisema ni oparesheni kubwa zaidi ya kijeshi ya aina yake kwa kizazi cha karibuni. Mamia ya wanajeshi hao walisafiri hadi London kwa usafiri wa umma Jumamosi asubuhi. Hizi ni baadhi ya picha kwenye tukio hilo kubwa.

Kulikuwa na kundi la watu wachache waliojitokeza ambao hawaonyeshi kukubaliana na mfumo wa Ufalme

Watu wengi maarufu walihudhuria tukio hilo