Je, kulia kazini kunakubalika?

Chanzo cha picha, Getty Images
"Nililia baada ya kupokea habari mbaya kutoka nyumbani na mara moja nikaacha kazi," anasema Clara, 48, kutoka Lancaster, kuhusu uzoefu wake wa kuhisi mfadhaiko kazini.
Clara anakumbuka alipokuwa na na hisia kali alipokuwa msichana alipohitimu na "alikosolewa vikali," na kisha miaka mingi baadaye "alipohisi kukasirika."
Lakini je, kulia kunaonyesha udhaifu au nguvu za mfanyakazi, au ni inahusu tu hisia za mtu?
Hakika, kuonekana kwa wengi wetu kulia kazini kuna uwezekano wa kuchukuliwa kama kitu cha ajabu au kisicho na maana kama ilivyotokea wakati Kansela wa Uingereza Rachel Reeves alilia Bungeni.
Picha za Reeves zilichapishwa kurasa za mbele na matangazo ya habari ya televisheni baada ya kuonekana akilia wakati wa kipindi cha maswali na majibu na waziri mkuu wiki iliyopita.
Milipuko yake ya mihomko ilitia wasiwasi sana soko la biashara kiasi kwamba gharama za serikali za kukopa zilipanda mara moja, na thamani ya pauni ilishuka sana.
Lakini je, ina umuhimu wowote iwapo kweli nitalia?
Kulingana na maoni ya watu ambao BBC ilizungumza nao, ni kawaida kwa watu wengine kulia mahali pa kazi.
Lakini wakati Clara aliposema alipata hisia na kulia alipohitimu masomo yake, na miaka baadaye alipopata "habari mbaya" na kuacha kazi yake, Emma alihisi kwamba alipaswa kuficha hisia zake kwasababu alifanya kazi katika "mazingira magumu ya kazi, yaliyotawaliwa na wanaume," akibainisha kwamba mara nyingi alijidhalilisha kwa kuonyesha "hisia au udhaifu."
Ingawa utafiti unaonyesha kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa wa kulia kuliko wanaume, wanaume wengi walituambia pia wamelia mbele ya wenzao kazini.
Dk. Jay Clayton anasema amelia zaidi ya mara moja " kwasababu ya wagonjwa, wafanyakazi wenzake, na familia kwa miaka mingi, niliposhiriki huzuni yao."
Wakati huo huo, mwanamume mwenye umri wa miaka 38 kutoka London, ambaye anafanya kazi katika masuala ya fedha, alisema alihisi hisia za kulia kazini wakati akishughulika na masuala ya kibinafsi, na alihisi ilionyesha "utaalamu" kwa kuwa kazini
"Nguvu, sio udhaifu"
Je, kulia ni nguvu au udhaifu? "Kufikiria kulia kazini kama jambo lisilokubalika ni njia ya kizamani," anasema Sherine Hoban, kocha na mshauri wa mafanikio.
Anaongeza, "Tumehamia zaidi ya wazo la zamani kwamba taaluma katika kazi inamaanisha kuweka pembeni hisia. Katika ulimwengu wa sasa, akili ya kihisia ni nguvu, si udhaifu."
Kocha wa ukuzaji wa taaluma Georgia Blackburn anaelezea kuwa "sio kawaida kwa wafanyakazi kuhisi shinikizo kazini, kwa hivyo kampuni zinahitaji kujifunza jinsi ya kushughulika na kusaidia wafanyikazi ambao wanapitia hali ngumu." Anaongeza kuwa hili "litasababisha kuongezeka kwa tija ya wafanyikazi."
"Muajiri anayesikiliza wafanyakazi wake kwa dhati na kuwaonyesha huruma na uelewa ana uwezekano mkubwa wa kuwatia moyo na kuwafanya wawe na furaha zaidi baadaye," Blackburn anaongeza.

Chanzo cha picha, Amanda
Ndivyo ilivyotokea kwa Amanda huko Stockport, ambaye alshiriki kwenye kipindi cha Jeremy Vine Show kwenye BBC Radio 2.
Amanda anasema alilia wakati wa mahojiano ya kazi katika Chuo Kikuu cha Manchester miaka 17 iliyopita, baada ya baba yake kugundulika kuwa na ugonjwa mbaya, lakini bado alipata kazi hiyo na bado anaishikilia hadi leo.
"Nililia kila siku kwa karibu miezi tisa hadi baba yangu alipokufa," Amanda anaeleza. "Ilinifanya kutambua jinsi bosi wangu alivyokuwa wa ajabu, na jinsi mahali pa kazi palikuwa pazuri, kwamba ilikuwa inakubalika."

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mwanamitindo Amy Bowney alikuwa akipitia hali mbaya mwishoni mwa mwaka jana, alipokabiliwa na kipindi "kigumu sana" alipoacha kazi yake, ambayo iliambatana na matukio maumivu katika maisha yake ya kibinafsi.
Amy, ambaye alianzisha chapa ya mtindo endelevu ya Akin mapema mwaka huu, pia alihisi shinikizo la kuwa "mwanamitindo" wa mitindo ya kimaadili.
"Orodha yangu ya mambo ya kufanya ilikuwa: kuwalisha watoto, kuwachukua kutoka shuleni, kupanga chumba cha watoto, kubuni mkusanyiko wangu unaofuata, kuangalia wafanyakazi, kutatua malipo yangu ya kodi... na kisha kuokoa ulimwengu," Amy aliiambia BBC Radio 4's Woman's Hour.
"Nilipitia kipindi ambacho sikuweza kuacha kulia. Nililia hadharani, na jukwaani," aliongeza.
Amy hupata kuonyesha hisia kazini "za kishetani" na hana majuto , "Tunapaswa kulia na kuonyesha hisia."
"Wanawake katika nafasi za uongozi wanapaswa kuwa na uhuru wa kueleza hisia zao. Ninaona hilo kama nguvu kubwa, na ninaliona kuwa chanzo cha nguvu za kweli," alisema.
Wanaume dhidi ya Wanawake, Wafanyakazi dhidi ya Wakubwa
Lakini si kila mtu anakubaliana na maoni haya, na baadhi ya watu bado wako muhimu kwa kiasi fulani, anasema Anne Frank, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Usimamizi wa Chartered (CMI).
Anasema kuwa wanawake wanaolia wanaonekana kuwa "walio na hisia nyingi," wakati wanaume wanaoonyesha huzuni wanaweza kuaibika kwa kuwa na hisia na mazingira magumu.
Anaongeza kuwa wafanyakazi wa chini wanaweza kuruhusiwa kulia zaidi kuliko wakubwa wao, lakini si lazima iwe hivyo.
Frank anaeleza kwamba kwa "afisa mkuu kilio kinaweza kuonekana kuwa cha kushtua au hata kisichofaa, lakini kinapoelezwa kwa dhati, kinaweza kuwa cha nguvu. Inaonyesha kwamba viongozi ni wanadamu wanaojali sana kile wanachofanya."
Lakini ikiwa unatazamia kupanda ngazi ya taaluma, ni jambo la busara kuwa na ujasiri—angalau katika mashirika fulani—kama kocha Shereen Hoban anavyoonyesha.
Anaamini kuwa kulia kunaweza kuathiri nafasi zako za kupandishwa cheo, akieleza: "Hebu tuseme ukweli. Bado kuna upendeleo katika baadhi ya maeneo ya kazi ambao unaona uthabiti kama nguvu na hisia kama kutokuwa na utulivu."
Lakini Hoban anasema mashirika mengine yanaona mambo kwa njia tofauti, yakiwathamini viongozi ambao ni "wa kweli, wanaojitambua, na wanaoweza kushughulikia utata, ikiwa ni pamoja na hisia zao wenyewe."
Anaongeza kuwa ikiwa una mshtuko wa kihemko mara moja kazini, "haitaharibu kazi yako," na kwamba cha muhimu zaidi ni picha kuu: "utendaji wako, uwepo wako, na uwezo wako wa kuinuka au kusonga mbele kwa umakini."
Nini cha kufanya ikiwa unalia kazini
- Chukua muda kutafakari na kupumzika.
- Huna haja ya kuficha hisia zako; mara nyingi huonyesha kwamba unajali kikweli kuhusu kazi yako—na hilo si jambo baya.
- Lakini ni muhimu kuhisi kuungwa mkono, kwa hivyo ni vyema kuzungumza na mfanyakazi mwenzako unayemuamini, kuchukua mapumziko mafupi, au kutafuta usaidizi kutoka kwa meneja wako au HR.
- Wasimamizi na wafanyakazi wenza wanapaswa kuonyesha huruma wafanyakazi wao wanapolia - wape tishu, usijifanye kuwa haifanyiki.














