Urafiki wenye kikomo : Jinsi uhusiano wa China na Urusi ulivyopoa wakati wa vita nchini Ukraine

Karibu mwaka mmoja baada ya urusi kuanza vita vyake dhidi ya ukraine, kuna dalili kuwa China inaweza kuangalia upya dhana ya ''urafiki usio na kikomo" ambayo ilianzishwa siku kadhaa kabla ya uvamizi kamili wa Urusi ndani ya Ukaraine.
Kwa kushitushwa na kushindwa kwa Urusi nchini Ukraine na kukabiliwa na matatizo yake yenyewe, Beijing sasa inajaribu kupunguza athari za vitendo vya Urusi kwa kurekebisha mahusiano yake na nchi za Magharib.
Siku 20 tu kabla ya Urusi kuanzisha vita kamili vya uvamizi wa Ukraine, mapema mwezi Februari mwaka jana, kiongozi wa China Xi Jinping, katika hotuba yake ya kihistoria, alizungumzia kuhusu urafiki usio na ukomo’’ na "kutokuwepo kwa maeneo yanayozuiwa katika ushirikiano".
Gazeti la Financial Times, linaloongoza nchini Uingereza, linaripoti kwamba vyanzo vyake vya habari vimethibitisha kwamba viongozi wawili Xi na Putin waliijadili Ukraine, na Bw Putin "hakuelezea kutochukua hatua yoyote "iwapo Urusi iitashambuliwa.
Lakini ni dhahiri kwamba, ameshindwa kutaja mipango yoyote kwa ajili ya uvamizi kamili kwa rais Xi.
Umakini wa Bejing
Huku tukiwa hatuna uhakika kwamba Xi hakujua kuhusu mipango ya uvamizi ya Urusi, ukweli kwamba China ilikujiepusha kupiga kura ya kulaani hatua za Moscow mwezi Machi, ilikuwa makini kuegemea upande wowote katika mzozo wa Ukraine tangu mwanzo.
Mapema wakati vita vilipoanza- baadhi ya watu nchini China walionesha ari ya kushabikia hatua za jeshi la Urusi na wengi walishirikisha umma video ya hotuba iliyotafsiriwa ya Rais Putin akitangaza "operesheni maalumu ya kijeshi", maneno yanayotumiwa na utawala wa Moscow yanayomaanisha vita.
Lakini rasmi Beijing ilioesha kuwa na mkakati wa kutoonesha msimamo wake katika mzozo wa Ukraine.
Kwa upande mwingine, uongozi wa China uliilaumu serikali ya Marekani mjini Washington kwa kuanzisha mzozo, ikisema kuwa ulisababishwa na kupanuka kwa Nato katika bara Ulaya.
Kwa upande mwingine, Beijing haijakuwa na haraka ya kutoa usaidizi wa maana kwa serikali ya Urusi.

Chanzo cha picha, AFP
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Gazeti jingine maarufu la Magharibi Washington Post, linadai kuwa Urusi imekuwa ikiiomba mara kwa mara China usaidizi wa kifedha na kiteknolojia kwa pamoja.
Kupunguza athari
Wakati ambapo viongozi wa nchi hizo mbili wamewahi kukutana pekee tangu mwanzoni mwa vita ilikuwa ni mwezi Septemba, katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika mji wa Uzbekistan wa Samarkand.
Hii ni wakati Ukraine ilipoendesha mashambulizi ya kulipiza kisasi, ambayo yaliiwezesha kuyateka maeneo mengi ambayo Urusi ilikuwa imeyateka wiki kadhaa kabla.
Mzozo wa gharama ya maisha uliosababishwa kwa sehemu kubwa na vita vya nishati ambavyo Urusi ilianzisha dhdi ya Ulaya umesababisha wanunuzi wa Ulaya kutokuwa na pesa za kutosha za kununua bidhaa za China.
Kukataa kwa China kulaani uchokozi wa Urusi nchini Ukraine kulisababisha uhusiano mbaya kati yake na Magharibi.
Na ni Marekani na Muungano wa Ulaya ambazo zimesalia kuwa washirika wakubwa zaidi wa kibiashara na Uchina.
Hakujawa na uwekezaji wa china ndani ya Urusi katika miezi ya kwanza sita ya mwaka 2022 – wachambuzi wanasema Beijing inajaribu kupima hali na kujaribu kuepuka kuwekewa vikwazo vya pili na Marekani.

Chanzo cha picha, AFP
Mtaalamu wa masuala ya ushirikiano wa Urusi na Uchina, Leonid Kovacic, anaafiki kuwa kauli ya "kutokuwa na ukomo wa urafiki’’ haijaonekana katika hatua halisi . "Haitakuwa katika maslahi ya China kufanya mausiano yawe magumu na mataifa yote ya magharibi kwa pamoja ."
Huenda awali China haikuona ugumu wa suala la vita kwa EU na jinsi Ulaya ingehusika katika kuisaidia Ukraine , kifedha na kijeshi.
"Hii ndio maana China sasa inajaribu kulainisha mambo, walau kwa kiwango cha matamshi yake," aliongeza Kovacic.
Vita vya Ukaraine pia viliishawishi jinsi Uchina inavyoishughulikia Taiwan, ambayo beijing inaichukulia kama jimbo lake lililojitenga.
Wasiwasi katika kanda umeendelea kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni,huku China ikifanya mojawapo ya mazoezi makubwa zaidi ya jeshi lake la anga katika eneo linalozingira Taiwan mwezi Disemba.
Kubadilisha kazi ... na sera?
Baada ya kuteuliwa mwishoni mwa mwaka jana, waziri wa mambo ya kigeni wa China Qin Gang alizungumza na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov tarehe 9 Januari. Melezo rasmi kuhusu mazungumzo, ambayo yalifanyika "kwa ombi la Moscow",anasema kwamba ‘’Uhusiano wa China na Urusi una misingi ya kutoegemea upande wowote, kutozozana na usio kuwa wa uchokozi ."
Kauli hii ni tofauti sana na ile ya mwezi februari yaliyosema "urafiki usio na ukomo" kauli kutoka kwa Putin na Xi na hata kutoka katika maneno kuhusu "nchi mbili bora zenye mamlaka" waliyoyasema katika kikao cha Septemba.
Uteuzi wa Qin ulifuatiwa na kufutwa kazi kwa Msemaji wa wizara Zhao Lijian, ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huo kwa miaka mitatu iliyopita.

Chanzo cha picha, AFP
Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa kuondolewa kwenye cheo cha juu na kushushwa madaraka ni jambo la kawaida, huku wengine wakisema kuwa ni mkakati wa China wa mabadiliko iliyoyafanya ili kupunguza mvutano na mataifa mengine.
Kuboresha uhusiano ni muhimu huku China ikijaribu kurejesha imani ya kibiashara kwa kuachana na sera yake tata ya "zero covid" na kuacha kutoa maneno matupu "mafanikio ya pamoja" na usawa wa kijamii.
Wachambuzi wa kisiasa wanaoegemea serikali wanasema bila kurekodiwa kwamba China imekatishwa tamaa na urusi na siasa zake za kieneo.
Dalili moja ya hili ilikuwa ni ukosoaji usio wa moja kwa moja wa Xi Jinping dhidi ya Vladimir Putin mwezi Novemba mwaka jana, wakati alipotoa kauli ya pamoja na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, wakisema "matumizi au vitisho vya silaha za nyuklia havikubaliki
Huku China ikiwa haitarajiwi kuelekeza matamshi yake makali katika kulaani msimamo wa Urusi, inatarajiwa kuwa makini kwa kupima kwa uangalifu mkubwa athari za kushindwa kwa Urusi kufikia malengo yake nchini Ukraine na kujiepusha kusababisha uhasama kimataifa.















