Je, nchi nyingine zinaweza kuingilia vita kati ya Gaza na Israel?

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK
Ulimwengu bado uko katika hali ya mshtuko, baada ya shambulio la ghafla la wapiganaji wa Hamas tarehe 7 Oktoba, na baadae mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyoanzishwa na Israel kwenye Ukanda wa Gaza, pamoja na uvamizi wa ardhini unaotarajiwa katika ukanda huo.
BBC ilipokea mamia ya maswali kutoka kwa watazamaji wake kuhusu mzozo huo, athari zake na wapi unaweza kuisha, huku wengi wakijiuliza ikiwa nchi nyingine zitahusika katika vita hivi au la.
Waandishi wetu, ambao wengi wao wako katika eneo hilo kwa sasa, walijibu maswali mawili muhimu ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara:
Je, tunaweza kushuhudia vita vya tatu vya dunia?

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK
Craig Johnson, aliyeko Skelmersal, Uingereza, anauliza: Iwapo Iran itahusika moja kwa moja katika mzozo huu, je, hii itawafanya Marekani na washirika wake kujiunga na vita moja kwa moja? Je, hii inaweza kusababisha Vita vya tatu vya Dunia
Mhariri wa masuala ya kimataifa Jeremy Bowen, aliyeko kusini mwa Israel, anajibu:
Rais wa Marekani Joe Biden alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Iran au mshirika wake wa Lebanon Hezbollah kuingilia kati, Biden alijibu kwa kusema: "Msijihusishe na vita hivi.
Hivi karibuni Wamarekani wametuma meli mbili za kubeba ndege za kivita mashariki mwa Mediterania, ili kutuma ujumbe thabiti kwa Iran: kujiepusha na vita.
Marekani inasema kwamba chama chochote kitakachoingilia vita hivi kitakabiliana na jeshi la Marekani , na sio tu jeshi la Israel.
Moja ya makosa makuu katika Mashariki ya Kati ni kati ya Marekani na washirika wake, na Wairani na washirika wao.
Pande zote mbili zinafahamu hatari zinazoweza kutokea. Iwapo hali itabadilika kutoka vita baridi hadi kuwa vita vya motoi , vitateketeza eneo la Mashariki ya Kati lenye umuhimu kimataifa.
Kwa nini Umoja wa Mataifa hauingilii kati kuhusu mashambulizi ya anga kwenye Ukanda wa Gaza?

Chanzo cha picha, getty images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Sadul Haq anaisishi London anauliza: Ikiwa kila mtu atakubali kwamba Israel inaua raia na itaua zaidi kwa mashambulizi yake ya anga ya Ukanda wa Gaza, basi kwa nini Umoja wa Mataifa na nchi nyingine haziingilii kati?
Mwandishi wa kidiplomasia James Landale anajibu:
Sababu kuu inayofanya nchi nyingi kutoitaka Israel kusitisha mashambulizi yake ya anga ni kwamba zinakubali kuwa Israel imeshambuliwa na Hamas na ina haki ya kujilinda.
Ama kuhusu wito wao wa kujizuia, inahusiana na jinsi Israeli inavyojilinda.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alisema kuwa, Jumatatu asubuhi, alizungumza na Waziri Mkuu wa Israel kuhusu haja ya "kupunguza athari kwa raia mjini Gaza."
Umoja wa Mataifa pia umeitaka Israel kuepuka majeruhi ya raia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema siku chache zilizopita: "Sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria za haki za binadamu lazima ziheshimiwe na kuzingatiwa; raia lazima walindwe na kamwe wasitumike kama ngao ya vita.

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK
Israel inasisitiza kuwa ndege zake za kivita na makombora yanashambulia kwa mabomu maeneo ya Hamas huko Gaza. Lakini raia wengi tayari wanauawa na kujeruhiwa katika mashambulizi haya ya anga.
Wapalestina wanasema kuwa, sababu ya majeruhi wengi ni kwamba mashambulizi ya Israel ni ya kupita kiasi na ni ya kiholela.
Wakati Israel inasema hii ni kwa sababu Hamas inatumia raia kama ngao za binadamu















