Wafahamu wanaume wenye mamlaka zaidi China kwa sasa

g

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wanaume wamechaguliwa na Rais Xi Jinping.

Chama cha Kikomunisti cha Uchina (CCP) kimefichua majina ya wanaume watakaoiongoza China kwa miaka mitano ijayo

 Wanaume hawa ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Ofisi ni sawa na baraza la washauri wa rais.

 Wanaangaliwa kama wasomi wa hali ya juu ndani ya chama. Nchini China kupanda kwenye vyeo vya juu mara nyingi kunahitaji sio tu uwe na rekodi nzuri kisiasa, lakini pia uwezo wa kudhibiti mahasimu wa ndani.

 Sio jambo lisilo la kawaida kushuhudia mabadiliko makubwa katika Kamati ya kudumu katika mwisho wa muhula na mara hii haikuwa tofauti.

 Hakika majina mengi yaliyochaguliwa na Rais Xi Jinping, ni mapya, mbali na Zhao Leji na Wang Huning.

 Hakuna mwanamke aliyeteuliwa miongoni mwa wajumbe 24 wa ofisi ya siasa ambamo kamati ya kudumu huainishwa. Sun Chunlan, naibu Waziri mkuu wa Baraza la taifa akiwa na uzoefu wa miongo kadhaa, amekuwa ni mwanamke pekee katika ofisi ya siasa, lakini alistaafu akiwa na umri wa miaka 72

 Dhahiri zaidi ni kwamba Xi Jinping anasalia kuwa ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi na ataendelea kuongoza ili mradi anapenda kufanya hivyo au hadi pale mtikisiko wa kisiasa usiofahamika siku zijazo umuondoe mamlakani.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Hawa ni wanaume ambao, wakiongozwa na Xi Jinping, watakuwa na mamlaka makubwa zaidi ya kisiasa nchini China.

Viongozi wenye mamlaka ya China

Getty

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Li Qiang

Li Qiang

Umri : 63

Wadhifa wake wa kisiasa wa sasa: Katibu wa chama katika Shanghai

Akionekana kama mmoja wa watu wanaoaminiwa zaidi na Xi , Li alifanya kazi katika kaunti ndogo katika jimbo la Zhejiang.

Wakati Xi alipochaguliwa kama kiongozi wa chama katika Zhejiang, Li alihudumu kama mkuu wake wafanyakazi.

Timu yake ililalamikiwa kwa jinsi ilivyoshughulikia sheria ya ‘ lockdown’ katika Shanghai na ilikosolewa na wakazi wa jimbo hilo. Kulikuwa na tetesi kuhusu iwapo hili huenda limeathiri hali yake ya baadaye ya kisiasa.

 Lakini kwa uteuzi wake , ni wazi kwamba utiifu wake kwa Xi umemuweka katika nafasi nzuri. Vyeo vya wajumbe wa kamati ya kudumu vitathibitishwa mwaka ujao na wengi wanaamini kuwa Li atakuwa Waziri mkuu ajaye, ambaye ana mamlaka makubwa baada ya Xi.

G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Zhao Leji

Zhao Leji

Umri : 65

Wadhifa wake sasa: Katibu wa kamati kuu ya nidhamu

Zhao anachukuliwa kama nyota inayopaa katika uongozi wa China na ana uhusiano wa karibu na jimbo la Shaanxi province, sawa na Xi.

Baada ya kuingia katika serikali ya jimbo la Qinghai, alipanda cheo haraka na kuwa gavana akiwa na umri wa miaka 42, akiwa ni mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwa gavana wa jimbo nchini China.

Kama mkuu wa taasisi ya kupambana na ufisadi, Zhao ana wajibu wa kuimarisha nidhamu ndani ya chama na amewaripoti maafisa wa ngazi ya juu kwa kuchukua hongo kwa miaka mingi.

G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wang Huning

Wang Huning

Umri : 67

Wadhifa wake wa sasa: Katibu wa kwanza wa secretarieti ya Chama cha kikomunisti.

Akiwa mwana taamuma na profesa wa zamani, Wang alipanda vyeo baada ya kuwavutia wanasiasa wa ngazi ya juu. Alipendekezwa kwa aliyekuwa Rais wakati huo Rais Jian Zemin na kupandishwa cheo kama mshauri wake.

Kama mwanasiasa mwananadhraria wa chama , Wang anachukuliwa kama mtu anayeandaa dhana nyingi zachama cha Kikomunisti, ikiwa ni pamoja na fikra za viongozi watatuwa: Fikra ya Jiang Zemin ya kuwa bora zaidi yamara tatu, ya Hu Jintao kuhusu Mtizamo wa kisayansi kuhusu maendeleo ya Hu , na Fikra ya Xi Jinping.

 Wang anasemekani kuwa na mahusiano mazuri na makundi yote ya chama.

G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, CaiQi

CaiQi

Umri : 66

Wadhifa wake kwa sasa: Meya wa Beijing

Akiwa mshirika wa karibu wa Xi, Cai hamefanya kazi chini ya kiongozi wa Wachina katika majimbo ya Fujian na Zhejiang na imempatia ufuasi usioyumba,

Uandaaji wa Olyimpiki ya majira ya baridi - Winter Olympics kayika mji mkuu Beijing mwanzoni mwa mwaka, wakati wa kipindi cha janga ;a corona, ni jambo lililoangaliwa ndani ya chama kama mafanikio na kufaya watu wawe na hisia nzuri kumuhusu.

Hatahivyo, pia alisababisha utata wakati alipozindua mpango mwaka 2017wa kupunguza idadi ya watu katika mji mkuu, ambao uliwaathiri na kuwalazimisha watu wengi wa kipato cha chini kuhama katika mji mkuu.

G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ding Xuxiang

Ding Xuxiang

Umri : 60

Wadhifa wake wa sasa: Mkurugenzi wa Ofisi ya Sekretarieti kuu ya ofisi yar ais. Engineer Ding alianza kazi yake katika kituo cha utafiti kinachohusishwa na serikali kilichopo Shanghai.

Ingawa hakuwa na uzoefu kama wa kiwango cha jimbo au ya ugavana, kwa kawaida alionekana kama mtu muhimu wa kupanda katika mamlaka, alikuwa katibu wa Xi mwaka 2007.

Tangu mwaka 2014 amekuw amkuu wa ofisi yar ais, akawa kaimu mkuu wa wafanyakazi wa Xi.

Akiwa mtetezi mkuu wa fikra ya Xi Jinping, ni mooja wa wasaidizi wa kutegemewa zaidi. Amekuwa akiambatana na kiongozi wa China katika ziara mbali mbali za ndani ya China na nje ya nchi.

Waangalizi wanasema huenda amekuwa na Xi kwa muda zaidi kuliko afisa mwingine katika miaka ya hivi karibuni.

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Lixi

Lixi

Umri : 66

Wadhifa wake wa sasa: Katibu wa chama katika jimbo la Guangdong

Aliwa ni mfuasi sugu wa Xi ana akiwa na uhusiano wa karibu na familia ya kiongozi wa China, Li anaonekana kama mtatuizi wa mzozo baada ya kuweza kukabiliana na kashfa katika jimbo la Liaoning kuhusu data za kughushi katika mwaka 2017.

Alikuwa kiongozi wa chama katika mji muhimu wa Yanan, uliotumiwa na Mao Zedong kama makao makuu ya chama wakati wa Vita Kuu ya II ya Dunia na ambako Xi aliishi miaka saba ya kazi ngumu.

Katika Guangdong, Li alisisitizia maendeleo ya sekta ya teknolojia na mageuzi ya kiuchumi. Pia aliendeleza biashara mpya na sera za ushirikiano katika eneo hilo.