Afrika Kusini yageukia nishati ya jua kukabiliana na tatizo la kukatika kwa umeme

Mhandisi mchanga Nolwazi Zulu anasema kwamba alipokuwa kijana aliamua "atatoka nje na kufanya kitu" kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara ambako kuliharibu jamii yake.

Sasa ana umri wa miaka 25, Bi Zulu anatoka kijijini Kwazulu-Natal kwenye pwani ya mashariki mwa Afrika Kusini.

Kama ilivyo katika nchi nyingine jimbo lake la asili limelazimika kuvumilia kukatika kwa umeme mara kwa mara, maarufu kama "load-shedding ", tangu 2008.

Hii imesababishwa na kuchoka kwa gridi ya umeme inayomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini, na vituo vyake vya nishati ya makaa ya mawe ikiwa wakati mgumu kukidhi mahitaji.

Ili kujaribu kusaidia kutatua tatizo hilo, na kuongeza stakabadhi zake za kimazingira, serikali ya Afrika Kusini sasa inaendelea na juhudi za kuongeza kiwango cha uzalishaji wa nishati ya jua nchini humo.

Kufanya hivyo ni kuhimiza makampuni husika kutoa mikataba kwa ajili ya makubaliano.

Kwa sasa inataka kupata megawati 1,000 za ziada kutoka kwa nishati ya jua, kutosha kutoa umeme kwa takribani nyumba milioni moja nchini.

Hii ni pamoja na nia ya kuongeza uzalishaji wa umeme wa upepo kwa megawati 1,600.

Hivi sasa ni 11% tu ya nishati ya Afrika Kusini inatokana na nishati mbadala, na zaidi ni upepo.

Ni asilimia 0.9 tu kufikia sasa inatoka kwa nishati ya jua, katika nchi ambayo inapata wastani wa saa nane hadi 10 za jua kila siku, ikilinganishwa na nne za Uingereza.

Kampuni moja ambayo imeshinda mojawapo ya zabuni za nishati ya jua ni Art Solar, kampuni pekee inayomilikiwa na Afrika Kusini kutengeneza sola.

Ni katika kampuni hii ambapo Bi Zulu anafanya kazi katika timu ya wabunifu anapoendelea kusomea diploma ya uhandisi wa umeme katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Durban.

Mbali na kusaidia gridi ya taifa ya umeme, anasema kuwa paneli za jua zinaweza kuleta umeme katika nyumba nyingi za vijijini ambazo hazina umeme.

"Ninataka kufungua tawi la kampuni ya Art Solar huko Ulundi [alikokulia], na kupeleka nishati ya jua katika kijiji changu," asema Bi Zulu.

"Ni nafuu na bora zaidi kuliko jinsi tunavyoishi kupitia ugawaji wa umeme, na itabadilisha maisha ya watu wengi."

Kampuni ya Art Solar yenye makao yake Durban ilianza miaka 12 iliyopita, ikijenga paneli za jua chini ya leseni kutoka kwa kampuni ya Ujerumani ya Bosch.

Sasa inatengeneza paneli kwa ushirikiano na kampuni nyingine ya Ujerumani ya Talesun kwa soko la Afrika Kusini na kimataifa.

Meneja mkuu Viren Gosai anasema kuwa msukumo wa jua wa serikali umeipa kampuni imani ya kufungua kituo kipya ambacho kinaweza kutoa paneli 650,000 kwa mwaka.

Pia hutoa huduma hii kwa nyumba za kibinafsi na biashara, licha ya paneli zake kuwa ghali zaidi kuliko zinazoagizwa nje yan chi zenye ubora wa chini ambazo hazikabiliani na ushuru wowote.

"Hatua za kutotoka nje za Covid-19 zilikuwa na athri mbayakwa njia nyingi," anasema Bw Gosai.

"Lakini jambo moja chanya nililoliona ni kwamba lilifanya watu wawe wazalendo."Mkataba mmoja wa hivi majuzi wa Art Solar ulikuwa ukitoa paneli za jua mwaka jana kwa hospitali ya kibinafsi huko Durban.

Ina maana kwamba Hospitali ya Ahmed Al-Kadi imelindwa kutokana na hatari ya kukatika kwa umeme.

Huku katika nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Tanzania, kampuni nyingine ya nishati ya jua ya Zola Electric ina suluhisho la usambazaji wa umeme ambalo linapuuza gridi za taifa.

Badala ya kuunganisha mashamba ya paneli za miale ya jua na mifumo ya umeme ya nchi nzima, inataka kuunda "gridi ndogo" zinazojitegemea kwa vijiji na jamii zingine.

Mtendaji mkuu wa Zola Bill Lenihan anasema tunahitaji "kuvuka njia za zamani za kufikiria juu ya upatikanaji wa nishati, haswa barani Afrika".

Anaongeza kuwa katika masoko yanayoibukia, kando na kuhama kutoka kwa nishati ya mafuta hadi yanayoweza kurejeshwa, watu wanafikiri kuwa na gridi ya nishati moja kunaweza kusifanye kazi.

"Kila mtu akilini mwake alikuwa akisema: Tutajenga gridi ya taifa.

Miaka mia moja baadaye katika maeneo kama Afrika watu hawana huduma ya gridi zinazofanya kazi, na hawatapata gridi zinazofanya kazi, kwa sababu ni teknolojia mbovu kwa masoko yanayoibukia.

Hili halina utata kusema hivyo tena. "Huko Afrika Kusini, Jay Naidoo, waziri wa zamani wa serikali chini ya Nelson Mandela, anashabikia wazo la kuwa na gridi ndogo tofauti kwa asilimia 20 ya kaya za Afrika Kusini ambazo hazijaunganishwa kwa gridi ya kampuni ya nishati ya serikali Eskom.

Leo yeye ni mdhamini na mkazi wa Earthrise Trust, mradi wa kilimo-ikolojia katika mkoa wa Free State.

"Lengo letu ni kuwezesha jamii za vijijini, haswa wanawake na vijana wanaochangia ukuaji wa uchumi," anasema Bw Naidoo.

"Umeme ingawa bado ni suala linalozua gumzo, "Fikiria kama tungeweza kuwa na gridi ya jua inayomilikiwa na jamii ndogo na kukidhi mahitaji yetu wenyewe? Inaweza kuwezesha umeme kwa jamii nyingi na kufanya ziwe na mali."