Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanajeshi waliochoka wa Ukraine nchini Urusi waambiwa wavumilie wakimsubiri Trump
"Hali inazidi kuwa mbaya kila siku." “Hatuoni mbele. Ardhi yetu haipo hapa.”
Takribani miezi minne baada ya wanajeshi wa Ukraine kuanzisha mashambulizi katika eneo la Kursk nchini Urusi, ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa wanajeshi wanaopigana huko unatoa picha mbaya ya vita ambavyo hawavielewi vizuri na wanahofia kuwa wanaweza kushindwa.
Tumekuwa tukiwasiliana, kupitia Telegram, na wanajeshi kadhaa wanaohudumu Kursk, mmoja wao ameondoka hivi karibuni. Tumekubali kutomtambua yeyote kati yao.
Hakuna jina katika makala haya na ni makala halisi.
Wanazungumza juu ya hali mbaya ya hewa na ukosefu wa usingizi wa kudumu unaosababishwa na mabomu ya mara kwa mara ya Urusi, ambayo ni pamoja na matumizi ya mabomu ya kutisha ya 3,000kg.
Pia wako katika mafungo, huku majeshi ya Urusi yakichukua tena eneo lao polepole.
"Mtindo huu utaendelea," Pavlo aliandika mnamo 26 Novemba. "Ni suala la muda tu."
Pavlo alizungumza kuhusu uchovu mkubwa, ukosefu wa silaha na kuwasili kwa vitengo, vilivyoundwa kwa kiasi kikubwa na wanaume wa makamo, walioletwa moja kwa moja kutoka kwa pande nyingine bila wakati mdogo au bila kupumzika katikati.
Kusikia askari wakilalamika, kuhusu maofisa wao wakuu, amri na ukosefu wa vifaa, si kawaida. Askari mara nyingi hufanya nini katika hali ngumu?
Chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa adui na majira ya baridi yakianza, itakuwa jambo la kushangaza kusikia matumaini mengi.
Lakini ujumbe ambao tumepokea unakaribia kuwa mbaya, ukieleza kuwa motisha ni tatizo.
Baadhi walihoji ikiwa mojawapo ya malengo ya awali ya operesheni hiyo, kuwaelekeza wanajeshi wa Urusi kutoka eneo la mashariki mwa Ukraine, lilifanya kazi.
Maagizo sasa, walisema, yalikuwa ya kusalia kwenye eneo hili dogo la ardhi ya Urusi hadi rais mpya wa Marekani, na sera mpya, atakapowasili katika Ikulu ya White House mwishoni mwa Januari.
"Kazi kuu inayotukabili ni kuvumilia zaidi hadi kuapishwa kwa Trump na kuanza kwa mazungumzo," Pavlo alisema.
"Nina hakika kwamba [Putin] anataka kutuondoa ifikapo tarehe 20 Januari," alisema.
"Ni muhimu sana kwake kuonesha kwamba anadhibiti hali hiyo. Lakini hadhibiti hali hiyo.”
Katika juhudi za kuisaidia Ukraine kuzuia mashambulizi ya Urusi huko Kursk, Marekani, Uingereza na Ufaransa zote zimeiruhusu Kyiv kutumia silaha za masafa marefu kulenga shabaha ndani ya Urusi.
"Hakuna mtu anayekaa kwenye mtaro wa baridi na kuombea makombora," Pavlo alisema.
"Tunaishi na kupigana hapa. Na makombora yanaruka mahali pengine."
Mnamo Oktoba pekee, Urusi iliweza kuchukua takribani kilomita za mraba 500 za eneo la Ukraine, idadi kubwa zaidi iliyochukuliwa tangu siku za mwanzo za uvamizi kamili wa 2022.
Kinyume chake, Ukraine tayari imepoteza karibu 40% ya eneo ambalo liliteka eneo la Kursk mnamo Agosti.
"Jambo kuu sio kukamata lakini kushikilia," Vadym alisema, "na tunapambana na hilo."
Licha ya hasara, Vadym anafikiri kampeni ya Kursk bado ni muhimu.
"Iliweza kugeuza baadhi ya vikosi vya [Urusi] kutoka mikoa ya Zaporizhzhia na Kharkiv," alisema.
Lakini baadhi ya wanajeshi tuliozungumza nao walisema walihisi kuwa walikuwa mahali pasipofaa, kwamba ilikuwa muhimu zaidi kuwa upande wa mashariki wa Ukraine, badala ya kukalia sehemu ya Urusi.
"Sehemu yetu inapaswa kuwa huko [mashariki mwa Ukraine], sio hapa katika ardhi ya mtu mwingine," Pavlo alisema. "Hatuhitaji misitu hii ya Kursk.
Na licha ya wiki kadhaa za ripoti kueleza kwamba wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini wamepelekwa Kursk kujiunga na uvamizi wa Urusi, wanajeshi ambao tumekuwa tukiwasiliana nao bado hawajakutana nao.
"Sijaona au kusikia chochote kuhusu Wakorea, wakiwa hai au wamekufa," Vadym alijibu tulipouliza kuhusu ripoti hizo.
Jeshi la Ukraine limetoa rekodi ambazo linasema kuwa ni njia za mawasiliano ya redio ya Korea Kaskazini.
Wanajeshi walisema walikuwa wameambiwa wamkamate angalau mfungwa mmoja wa Korea Kaskazini, ikiwezekana na nyaraka.
Walizungumza juu zawasi ya ndege zisizo na rubani au likizo ya ziada, kutolewa kwa mtu yeyote ambaye amefanikiwa kumkamata mwanajeshi wa Korea Kaskazini.
"Ni vigumu sana kupata Mkorea katika msitu wa Kursk," Pavlo alisema kwa kejeli. "Hasa kama hayupo."
Kuanzia Oktoba 2023 hadi Julai mwaka huu, vikosi vya Ukraine vilijaribu kushikilia daraja dogo huko Krynky, kwenye ukingo wa kushoto wa Mto Dnipro, takribani maili 25 (40km) juu ya mto kutoka mji uliokombolewa wa Kherson.
Operesheni hiyo ilikuwa ya gharama kubwa. Kiasi cha wanajeshi 1,000 wa Ukraine wanakisiwa kuuawa au kutoweka.
Wachambuzi wa kijeshi wanasisitiza kwamba pamoja na shida zote, kampeni ya Kursk inaendelea kuwa jukumu muhimu.
"Ni eneo pekee ambalo tunadumisha mpango huo," Serhiy Kuzan, wa Kituo cha Usalama na Ushirikiano cha Kiukreni, aliniambia.
Alikiri kwamba vikosi vya Kiukreni vinakabiliwa na "hali ngumu sana" huko Kursk, lakini alisema Urusi ilikuwa ikitumia rasilimali nyingi kuwaondoa, rasilimali ambazo ingependelea kutumia mahali pengine.
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Seif Abdalla