'Nilichangisha $200,000 kusomea Harvard - sasa sijui itakuwaje'

    • Author, Waihiga Mwaura, Blessing Aderogba, Debula Kemoli
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Fatou Wurie na jamii yake walichangisha takriban dolla 200,000 za Kimarekani kugharamia masomo yake katika Chuo Kukuu cha Harvard University nchini Marekani na amesalia na miezi kadhaa kukamilisha masomo yake, lakini azma ya mwanafunzi huyo kutoka Sierra Leonean kufikia ndoto yake iko mashakani.

Kupata nafasi ya kusomea Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani ilikuwa hatua ya kujivunia sana kwa Bi. Wurie.

"Ilikuwa fahari kubwa - kwa familia yangu nda jamii nzima kwa ujumla," anasema Bi. Wurie, Mwanafunzi anayesomea shada ya uzamivu katika taasisi ya T.H. Chan ya Chuo Kikuu cha Havard, akijikita zaidi katika tafiti zinazofungamana na athari za uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids) miongoni mwa wanawake Sierra Leone.

Akiwa amesalia na miezi kadhaa kabla yakukamilisha masomo na kuhitimu, juhudi zake zote sasa zinakabiliwa na tishio.

Hii ni baada ya utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza mpango wa kusitisha kwa muda utoaji wa viza ya elimu kwa wanafunzi wa kigeni.

Ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na kiongozi huyo dhidi ya baadhi ya vyuo vikuu vya Marekani, ambazo zinaonekana kuwa huru kupita kiasi.

Alipoulizwa kuhusu uamuzi wa kusitisha visa ya wanafunzi, msemaji wa idara ya serikali Tammy Bruce aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne: "Tunachukulia kwa uzito mkubwa mchakato wa kuhakiki ni nani anayekuja nchini, na tutaendelea kufanya hivyo."

Hatua hiyo imemuacha Bi Wurie na wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kurudi Marekani kumalizia masomo yake na kuhitimu Novemba mwaka huu.

"Hali hii inazua wasiwa mkubwa. Nikiwa mwanafunzi na mwanzilishi, kazi yangu inategemea safari za hapa na pale kwa ajili ya mwendelezo wa mpago wangu. Kusitisha utoaji hati ya usafiri hakutavurugi masomo yangu pekee - bali pia kunadhibiti harakati," anaongeza Bi Wurie ambaye anahisi alijiunga na taasis hiyo ya elimu ya juui "kwa manufaa ya bara zima".

Wanafunzi kama Bi. Wurie mara nyingi wanaweza kupanua programu zao kutokana na sababu za kibinafsi au za kitaaluma. Katika hali kama hizi, kwa kawaida huomba tena I-20 mpya - hati rasmi inayothibitisha kuandikishwa kwa programu ya elimu ya wakati wote na uthibitisho wa ufadhili wa kutosha.

Bi. Wurie tayari amepokea I-20 iliyoidhinishwa, kumaanisha kuwa ametimiza vigezo vyote ya kitaasisi na kifedha ili kurudi Harvard na kukamilisha shahada yake mwezi Novemba mwaka huu.

Lakini licha ya hili, kwa sasa hawezi kuomba miadi ya visa. Ikiwa uamuzi huo utatekelezwa kikamilifu na kudumishwa "itakuwa pigo kubwa," anasema, akiongeza kuwa "utafiti hauwezi kusitishwa".

Harakati ngumu za kutafuta fedha

Bi Wurie anasema kwamba kutafuta pesa za kulipia masomo yake ya Harvard kumemwekea mzigo wa maelfu ya dola yeye na familia yake.

"Nimechukua mikopo, nimefanya kazi kipindi chote cha masomo, na kulipia gharama zisizo na kikomo za - viza, nyumba, huduma za afya. Kando na athari za kifedha, kuna athari ya kihisia ya mifumo ya uhamiaji inayoendelea kila mara na kuhakikisha tunasalia kuwa watiifu na kuheshimu sheria za Marekani. Kila ukichelewa kufikia mahitaji husika inakugharimu zaidi ya dola - unakosa umakini na utulivu wa akili".

Ingawa ilimgharimu Bi. Wurie binafsi, pia ana wasiwasi kuhusu atahari ya hatua hii hii kwa wasomi wa baadaye wa Kiafrika.

"Inaumiza. sio kwangu pekee, bali kwa kile aliye na ndoto ya kupata elimu ya juu. Milango ya elimu ya kimataifa tayari iko wazi kwa wanafunzi wa Kiafrika. Wanapochukua hatua kama hizi, inatuambia uwepo wetu ni wa masharti".

Wanafunzi wa kigeni wanaotaka kusoma Marekani kwa kawaida lazima wapapange miadi katika ubalozi wa Marekani nchini mwao kabla ya kuidhinishwa.

Zaidi ya wanafunzi milioni 1.1 wa kimataifa kutoka zaidi ya nchi 210 walijiunga na vyuo vya Marekani katika mwaka wa 2023-24, kulingana na Open Doors, shirika linalokusanya data za wanafunzi wa kigeni.

Bi.Wurie anafikiri Marekani inahitaji kubuni sera ambazo "zinatambua elimu ya kimataifa kama uwekezaji wa pamoja," akiongeza kuwa Marekani "haipokei tu vipaji - inakua kupitia hilo."

Alipoulizwa ujumbe wake kwa Rais Donald Trump ni upi, Bi Wurie alisema, "Sera zako zinaweza kututenga au kututia moyo. Tulikuja kupata elimu - lakini pia kuongoza, kujenga na kuchangia. Jitahidi historia ikukumbuke kama mtu ambaye aliyefungua milango, sio aliyeifunga."