Je,visa vya moto wa msituni vinakuwa jambo la kawaida?

Chanzo cha picha, Getty Images
Melfu ya watu wamelazimika kuikimbia mioto katika Ufaransa France,Ureno, na Uhispania. Mioto hiyo pia imeibuka katika Alaska, kaskazini mwa Arctic , na katika maeneo yote ya kaskazini mwa Canada, na sio muda mrefu tangu moshi kuonekana ukitanda katika maeneo yaliyoungua ya misitu ya Argentina mchana na katika mji mkuu wa Paraguay. Mioto ya nyikani imekuwa ni ya kawaida zaidi – na je mataifa yana vifaa vya kutosha kuweza kukabiliana nayo?
Wataalamu wanasema kwamba"mioto isiyo ya kawaida inayotokana na hali ya hewa isiyo ya kawaida" -hali ya hewa inayosababisha hali za ukosefu wa mvua na upepo mkavu zinasababisha kuibuka kwa mioto ya nyikani - na kuifanya kuwa ya mara kwa mara zaidi na kutokuwa ya kawaida, katika karibu maeneo yote ya dunia.
Mabadiliko ya hali ya tabia nchi, wanasema, yanaifanya mimea kuwa rahisi zaidi kuungua na udongo kuwa mkavu zaidi , na mara kwa mara hali hii inapotokea huwa ya muda mrefu na , kubwa na mbaya zaidi.
Lakini athari hutofautiana kwa kila kanda na nyingine na inaweza kusababishwa na mambo mengine.
Mwandishi wa makala ya hivi karibuni ya tathmini katika fizikia ya jiografia anasema baadhi ya maeneo yenye misitu katitudo ya juu yalishuhudia ongezeko la 50% au zaidi la eneo linaloungua katika miongo miwili ya kwanza ya karne.
Hatahivyo, katika maeneo ya joto ya Afrika idadi ya mioto ya nyikaniilipunguakatika kipindi hicho hicho, kutokana namabadiliko ya matumizi ya ardhi, ikiwa ni pamoja na kupanuka kwa ukulima. Na hili, wataalamu wanasema inapunguza kwa ujumla idadi ya mioto ya nyikani kote duniani, na eneo linaloungua kwa ujumla.
"Maeneo ya Savana nayabakia kuwa yenye kutawanyika na ndio maana yanashuhudia mioto michache," anasema Dkt Niels Andela, mwanasayansi anachunguza maeneo ya mbali yanayoweza kukabiliwa na mioto katika taasisi ya BeZero Carbon. "Na kwasababu yanachukua hadi 70% ya mioto ya dunia, tunashuhudia kupungua kwa jumla ya matukio ya mioto ya nyikani ya dunia."
Huku kukiwa na ongezeko la ziada la joto, tatizo la moto wa nyikani linatarajiwa kuwa baya zaidi katika maeneo mengine.
Ripoti Mpango wa mazingira wa Umoja wa Mataifailiyochpishwa mapema mwaka huu ilitabiri ongezeko la ‘’mioto mikubwa’’ ya dunia hadi 14% ifikapo mwaka 2030, na 50% kufikia mwisho wa karne.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ilikuwa tu baada ya kufikia moto walipogundua ni kwa kiwango gani ni mkubwa," mwanakijiji, Ghulam Sakhi. "Upepo ulikuwa mkali sana na ilikuwa inasamabaza miali ya moto ."
Binamu zake Sakhi, Kalaa Khan, 35, na Mohammad Noor, 30, walijipata wakizuiwa kuona kutokana na moshi mkubwa. Kwa kukanganyikiwa walijipata wakitembea kuelekea usawa wa moto, na wakashinda kuudhibiti, anasema mjane ambaye lazima sasa alazimike kujaribu kuishi bila mume wa kumsaidia kuitunza familia.
"Hatuna usaidizi, hatuna raslimali za kupambana na mioto ya aina hiyo ya nyikani ," anasema Bw Sakhi,
Maafisa wa udhibiti wa maafa hawakufahamu kuhusu moto, anasema mwanaharakati wa mabadiliko ya hali ya hewa Salmeen Khpalwak, na mwanzoni hakujibu ombi la usaidizi.
Siku kadhaa baadaye helikopta ilitumwa kumwaga maji kwenye moto, bila mafanikio.
Ilikuwa tu pale Iran ilipotuma ndege yenye uwezo wa kumwaga maelfu ya maji ndipo sehemu kubwa ya moto ilipozima. Kwa hatua hii takriban 40% ya hekari 26,000 ya msitu imeangamia, vyanzo vya eneo hilo viliiambia BBC.

Chanzo cha picha, Getty Images
Zaheer Mirza, ambaye anafanya kazi katika mbuga ya wanyama ya Margalla Hills karibu na mji mkuu wa Pakistani, Islamabad, anasema wafanyakazi pale pia wana ukosefu wa ujuzi na vifaa vya kuzima moto.
Kuuzima moto, kwa kiasi ki[kubwa hutegemea vizima moto vya kujitengenezea nyumbani, asnasema . Kuzuia mioto kusambaa hutengeneza breki za mioto, " lakini vifaa hivi vimeonyesha kuwa havifai na mioto inaendela kuwa mibaya zaidi ".
Katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi mara nyingi huwa linazungumziwa suala la uwepo wa fedha zilizotumiwa kuzuia – kupunguza kiwango cha hewa ya kaboni na gesi nyingine zinazoongeza joto angani – na ni machache sana yaliyotekelezwa, au kusaidia nchi kufanya mabadiliko yanayoweza kuzisaidia kukabiliana na athari za tabia nchi.
Na kuhusu pesa zilizotumiwa katika utekelezaji, ni chache zilizoelekezwa katika kusaidia kukabiliana na mioto ya nyikani, anasema Duncan Macqueen wa taasisi ya kimataifa ya mazingra na maendeleo. Wakati alipokuwa akifanya kazi mjini Belize miaka michache iliyopita, Bw Macqueen alifahamu kwamba kulikuwa na mradi mmoja tu wa mafunzo ya mioto ya nyikani, yaliyodhaminiwa na Huduma za misitu za Marekani.












