Kwa Picha: Moto mkubwa waathiri California, Marekani

Maelfu ya watu wamelazimika kukimbilia usalama wao katika maeneo yanayokuzwa mizabibu kaskazini mwa California baada ya moto mkubwa wa nyikani kuzuka maeneo hayo.

Moto Oktoba 9, 2017 Glen Ellen, California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Idara ya kuzima moto jimbo hilo imesema moto unawaka maeneo 14 tofauti katika wilaya za Napa, Sonoma na Yuba.
Moto Oktoba 9, 2017

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu walijaribu kuokoa nyumba na mali yao kwa kujaribu kuzima moto huo, ambao umeathiri eka 49,000 (hekari 20,000).
Moto Oktoba 9, 2017 Napa, California

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wilaya za Napa, Sonoma na Yuba hujumuisha eneo maarufu za mizabibu California na hupatikana kaskazini mwa San Francisco.
Moto Oktoba 9, 2017 Napa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Nyumba zaidi ya 1,500 zimeteketea, mkuu wa idara ya misitu na kinga dhidi ya moto California Kim Pimlott, amesema.
Moto Oktoba 9, 2017

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu zaidi ya 10 wamefariki na wengine wengine wengi kujeruhiwa.
Moto Oktoba 9, 2017 Glen Ellen, California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gavana wa California ametangaza hali ya dharura katika maeneo hayo na kusema moto huo unatishia maelfu ya nyumba.ousands of residents".
Moto Oktoba 9, 2017 Glen Ellen, California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Moto huo ni miongoni mwa visa vibaya zaidi vya moto katika jimbo hilo.
Moto Oktoba 9, 2017 Glen Ellen, California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Moto huo umezidishwa kasi na upepo mkubwa pamoja na kiangazi.
Moto Oktoba 9, 2017 Glen Ellen, California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chanzo cha moto huo bado hakijabainika.