Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukraine imepata ndege za kivita za Uingereza za Vita vya Pili vya Dunia nje ya Kyiv
Mabaki ya kutu ya ndege nane za kivita za Uingereza za Vita vya Pili vya Dunia zimepatikana zikiwa zimezikwa msituni nchini Ukraine.
Ndege hizo zilitumwa kwa Umoja wa Kisovieti na Uingereza baada ya Ujerumani wakati wa vita vya Nazi kuivamia nchi hiyo mwaka wa 1941.
Zilikuwa sehemu ya msaada wa kijeshi wa washirika wa USSR, uliolipwa na Marekani chini ya mpango wa kukodisha.
Sheria sawia inatumiwa na serikali ya Marekani hii leo kutuma msaada wa kijeshi kwa Ukraine inapojaribu kuwafukuza wanajeshi wa Urusi nchini mwake.
Wataalamu wa masuala ya usafiri wa anga wanasema hii ni mara ya kwanza kwa mabaki ya ndege za Kivita za Hurricane kupatikana nchini Ukraine.
"Ni nadra sana kupata ndege hii nchini Ukraine," anasema Oleks Shtan, rubani wa zamani wa shirika la ndege ambaye anaongoza uchimbaji huo.
"Ni muhimu sana kwa historia yetu ya usafiri wa anga kwa sababu hakuna ndege ya chini ya sheria ya kukodisha iliyopatikana hapa hapo awali."
Ndege ya kivita ya Hurricane Hawker ilikuwa muhimu sana wakati wa Vita vya Uingereza - kampeni ya anga ya 1940 wakati Jeshi la Royal Air Force (RAF) lilishinda majaribio ya Wajerumani kuivamia Uingereza.
Ingawa jukumu lake mara nyingi limezibwa na ndege mpya zaidi na inayoweza kubadilika mno ya Spitfire, Hurricane ilidungua zaidi ya nusu ya ndege zote za adui wakati wa vita.
"Ndege Hurricane ilikuwa mashine yenye nguvu na rahisi kuruka," Bw Shtan asema.
"Ilikuwa imara kama bunduki na nzuri zaidi kwa marubani wasio na uzoefu. Ndege ya kivita ya kutegemewa."
Kwa jumla, karibu ndege za kivita za Hurricane 3,000 vilitumwa kwa USSR kati ya 1941 na 1944 kusaidia juhudi za vita vya Soviet.
Nyingi ziliharibiwa katika mapigano au zilisambaratishwa baadaye.
Lakini ndege nyingi za Hurricane ziliharibiwa kimakusudi na kuzikwa baada ya vita, kwa hivyo Wasovieti hawakulazimika kulipa Marekani.
Chini ya sheria ya Kukodisha, USSR ilitakiwa kulipia vifaa vyovyote vya kijeshi vilivyotolewa ambavyo vilibakia baada ya uhasama kumalizika.
Hii ilikuwa hatima ya ndege Hurricane nane zilizopatikana zimezikwa kwenye msitu kusini mwa Kyiv - sasa mji mkuu wa Ukraine ulio huru.
Walikuwa wamenyang'anywa zana zao, redio, bunduki za rashasha na chuma chakavu chochote muhimu.
Kisha ziliburutwa na matrekta kutoka uwanja wa ndege wa karibu, zikavunjwa na kudondoshwa bila sherehe kwenye bonde lisilo na kina.
Inafikiriwa wakati huo zilifunikwa na udongo na tingatinga.
Mabaki hayo yaligunduliwa hivi majuzi baada ya bomu ambalo halikulipuka kutoka vitani kupatikana karibu.
Sehemu iliyobaki ya korongo ilikaguliwa kwa kutumia vifaa vya kugundua chuma na mabaki hayo ya ndege Hurricane yakapatikana.
Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Usafiri wa Anga la Ukraine sasa liko katika harakati za kuchimba eneo hilo kwa mikono.
Wafanyakazi huko wanalenga kutambua ndege nyingi iwezekanavyo ili ziweze kuunganishwa na kuwekwa kwenye maonyesho.
Valerii Romanenko, mkuu wa utafiti katika jumba hilo la makumbusho, anasema ndege za kivita za Hurricane zilikuwa na jukumu muhimu katika historia ya Ukraine.
"Hurricane ni ishara ya usaidizi wa Uingereza wakati wa miaka ya Vita vya Pili vya Dunia, kama vile tunavyothamini sana msaada wa Uingereza siku hizi," anasema.
"Uingereza ni mojawapo ya wauzaji wakubwa wa vifaa vya kijeshi kwa nchi yetu sasa."
"Mwaka 1941 Uingereza ilikuwa ya kwanza kusambaza ndege za kivita kwa Umoja wa Kisovieti kwa wingi. Sasa Uingereza ni nchi ya kwanza ambayo inatoa makombora ya Storm Shadow kwa vikosi vyetu."
Inadhaniwa kuna ndege Hurricane 14 tu zilizorejeshwa zinazoweza kuruka duniani leo.
Baada ya uvamizi wa Wajerumani, USSR ilipoteza ndege nyingi na ilikuwa ikihitaji sana ndege za kivita.
Awali, ndege kadhaa za RAF Hurricane zilitumwa Arctic kusaidia.
Lakini baada ya muda mfupi marubani wa Uingereza waliondoka na ndege zikachukuliwa na wanahewa wa Soviet.
Rekodi zinaonyesha kuwa wengi hawakupenda ndege Hurricane, ikizingatia kuwa haina nguvu, na ni yenye ulinzi duni.
Mwisho wa vita ilionekana kuwa ya kizamani na ilitumiwa haswa kwa kazi ya ulinzi wa anga.
Ndege za kivita Hurricane nane zilizopatikana kusini mwa Kyiv zilitumika kutetea vituo vikuu vya usafiri - hasa vituo vya reli na makutano.