Ukraine na Urusi: Je ni mpango gani wa Putin unaofuata kwa Ukraine?

Chanzo cha picha, Reuters
Wanajeshi wa Urusi "wamechoka"? Je, Putin amemaliza "operesheni maalum ya kijeshi"? Je, nini kinafuata?
Na Urusi imesonga mbele tena. Ukraine wamerudi nyuma tena.
Kwa mujibu wa gavana wa mkoa wa Lisichansk, vita vikali na vya muda mrefu vilivyotabiriwa huko vilizuiwa na mkakati wa kurudi nyuma.
Sergei Gaidai alisema: "Urusi ina ubora katika silaha na risasi. Wangeiharibu kutoka mbali, kwa hiyo hapakuwa na maana ya kukaa."
Hii inaonekana kuwa sawa na taarifa kutoka Urusi kuhusu kuteka kwa jiji hilo, kwamba iliiuchukua jiji hilo bila upinzani wowote. Video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumapili zilionyesha wapiganaji wa Chechnya wakicheza katika maeneo ya kati.
Wanaweza kusherehekea. Kutekwa kwa mji wa Lisichansk kunamaanisha kuwa Urusi imetwaa vilivyo eneo lote la Luhansk, ambalo ndilo lengo kuu la kimkakati la uvamizi wa rais Putin nchini Ukraine.
Hii inamaanisha nini kwa Donbass na vita kwa ujumla?
Wacha tuanze na Ukraine. Jambo kuu kwao lilikuwa kuondokana na kuzingirwa, kama huko Mariupol. Ingawa ulinzi wao wa mji wa bandari wa kusini ulipunguza kasi ya Urusi kwa wiki kadhaa, matokeo ya mwisho yalikuwa kifo au kukamatwa kwa maelfu ya askari wenye uwezo zaidi wa jeshi la Ukraine. Ukraine inataka kuepuka hili kwa hali yoyote.
Rais Zelensky alisisitiza hili waziwazi katika hotuba yake wakati wa usiku. "Tutarejesha kuta, tutarudisha ardhi, lakini kwanza tunahitaji kuokoa watu," aliwaambia watu.
Sergey Gaidai pia alisema vivyo hivyo: "Wanajeshi wetu walirudi kwenye nafasi zilizoimarishwa zaidi ... Walilinda Luhansk kwa miezi mitano. Wakati ulinzi huu ukiendelea, tulijenga ngome mpya katika eneo la Donetsk. Sasa askari wamekwenda upande huo."

Chanzo cha picha, RUSSIAN MINISTRY OF DEFENCE
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Saa chache baada ya kuanguka kwa Lisichansk, mshauri wa rais Aleksey Arestovich aliita utetezi wa Eneo la Lisichansk-Severodonetsk "operesheni ya kijeshi iliyofanikiwa".
Kwa sasa bendera ya Urusi inapepea katika miji yote miwili, mantiki hii inaweza kuonekana imepotoshwa kidogo, lakini anaamini wamekuwa wakicheza mchezo muhimu kwa muda mrefu.
Ili kuelewa mantiki hii, unahitaji kuelewa umuhimu wa silaha za Magharibi kwa upinzani kwa Ukraine. Kwa kifupi, bila msaada wa NATO, wangekabiliwa na matatizo zaidi kuliko sasa.
Kadri wanavyochelewesha Urusi kusonga mbele, ndivyo mifumo ya juu zaidi ya makombora na ufundi wataweza kutumia katika vita.
Inasemekana kuwa HIMARS iliyowasilishwa na USA tayari inafanya kazi na itabadilisha kwa kiasi kikubwa usawa wa mzozo.
Muda zaidi unamaanisha kwamba vifaa vingi vitawasili, ambavyo vitaweka mizani sawa kwa faida yao, haswa wakati Urusi inajitahidi kubadilisha vifaa vyao vya kale na risasi chini ya vikwazo.
Sasa hebu tutathmini hali hiyo kutoka upande wa Urusi. Lengo lao ni kuiteka Donbass ili "kuikomboa". Kutekwa kwa Luhansk ni hatua ya karibu na hii.
Hakika, umuhimu wake unaweza kuonekana leo wakati Rais Putin akiwatunuku wale walioongoza mashambulizi na "shujaa wa Urusi" tuzo ya juu zaidi.
Lakini nini kitafuata? Wanajaribu kuchukua karibu maeneo mengine ya Donbass, haswa miji ya Slavyansk na Kramatorsk, ambayo ilipigwa makombora katika siku za hivi karibuni.
Inasemekana kuwa Sloyansk ina umuhimu wa kipekee tangu vuguvugu la kwanza la waasi lilitokea 2014.
Kwa kuongezea, mkakati mpana wa Urusi haueleweki. Mengi yatategemea hali ya vikosi vyao vya kijeshi baada ya kuichukua Donbass.
Leo, Rais Putin alikiri hili kimyakimya na kusema: "Vitengo vilivyoshiriki katika operesheni za kupambana na mafanikio na ushindi katika mwelekeo wa Luhansk, bila shaka, vinapaswa kupumzika na kuongeza uwezo wao wa kupambana."
Ikiwa bado wanasonga mbele kwa kasi, wanaweza kuendelea na mashambulizi yao ya kuchukua sehemu zote za kusini mwa Ukraine, ikiwemo Dnieper au jiji lolote kubwa zaidi ya hapo.
Walakini, ikiwa watachoka, kama wachambuzi wengi walivyotabiri na Putin amedokeza, wanaweza kutangaza mwisho wa "operesheni maalum ya kijeshi."
Wanatumaini kwamba usitishaji vita wa upande mmoja utadhoofisha uungwaji mkono wa kimataifa kwa Ukraine na wengine wanaweza hata wanatumaini kuwa hata Ufaransa na Ujerumani zitatafuta amani.
Ukraine bila shaka itaendelea kupigana, lakini bila silaha imara, hali inaweza kuegeuka katika mgogoro waliohifadhiwa kama mwaka 2014 na 2022.
Kwa sasa, hakuna uhakika, kwa sababu pande zote mbili zinadai ubora wao. Hakika, ingawa Ukraine ipoi nyuma huko Donbass, imepata mafanikio katika siku za hivi karibuni, hasa katika kutwaa tena kisiwa cha Ilon ambako bendera za bluu na njano zimewekwa tena leo.
Tunaweza kusema kwa ujasiri kwamba vita hii haitamalizika katika siku za hivi karibuni na wakazi wa mkoa Donetsk watateseka kutokana na athari za mapambano.















