Urusi na Ukraine: Ukraine imepata hasara kubwa huko Donbas - Urusi

Ukraine inakabiliwa na "hasara kubwa miongoni mwa wanajeshi wake , silaha na zana za kijeshi" katika eneo la mashariki la Donbas, Urusi imesema katika akaunti yake hivi punde kuhusu vita.

Moja kwa moja

  1. Ukraine yakosoa sera ya nishati ya Merkel

    Bomba la Nord Stream 2 kati ya Urusi na Ujerumani lilikamilika Septemba iliyopita lakini Ujerumani imesitisha kuidhinisha leseni yake ya uendeshaji.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Bomba la Nord Stream 2 kati ya Urusi na Ujerumani lilikamilika Septemba iliyopita lakini Ujerumani imesitisha kuidhinisha leseni yake ya uendeshaji.

    Ukraine imemkosoa kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel baada ya kusema ‘’hakuwa na la kuomba msamaha’’ kuhusu jibu lake kwa hatua ya Urusi kunyakua Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.

    Merkel, ambaye aliondoka madarakani miezi sita iliyopita, alisema Jumanne kwamba Ulaya na Urusi ni majirani ambao hawakuweza kupuuza kila mmoja.

    ‘’Lazima tutafute njia ya kuishi pamoja licha ya tofauti zetu zote,’’ alisema.

    Lakini mshauri wa rais wa Ukraine Mykhaylo Podolyak alisema Merkel ‘’ameisukuma’’ Ulaya kuelekea utegemezi zaidi wa usambazaji wa nishati wa Urusi.

    ‘’Ikiwa Kansela Merkel siku zote alijua kwamba Urusi ilikuwa inapanga vita na lengo la Putin ni kuharibu EU, basi kwa nini [Ujerumani] ingejenga Nord Stream 2,’’ aliandika kwenye Twitter.

    Mrithi wa Merkel Olaf Scholz alisimamisha mradi wa bomba la gesi mwezi Februari baada ya uvamizi huo.

  2. Nchi za Ulaya Kaskazini zinalaani uvamizi wa ‘’kikatili’’

    Ben Wallace alikutana na mawaziri wengine 11 wa ulinzi wa Ulaya mjini Reykjavik

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Ben Wallace alikutana na mawaziri wengine 11 wa ulinzi wa Ulaya mjini Reykjavik

    Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amekutana na viongozi wenzake kutoka nchi nyingine 11 za Ulaya nchini Iceland kujadili changamoto za usalama wa eneo la kaskazini mwa Ulaya kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

    Mataifa ya Kundi la Kaskazini - Denmark, Estonia, Finland, Ujerumani, Iceland, Latvia, Lithuania, Uholanzi, Norway, Poland, Sweden na Uingereza - walitoa tamko la pamoja kulaani uvamizi huo na kukaribisha maamuzi ya Sweden na Finland kuomba kujiunga. Nato.

    Wallace anasema ‘’inaimarisha shutuma zetu zisizo na shaka za uvamizi wa kinyama wa Putin na azimio letu kwamba Ukraine itafaulu.’’

    Pia alitia saini mkataba mpya na Finland unaojenga mkataba wa usalama wa pande zote wa Uingereza na Finland waliokubaliana mwezi Mei.

    Mkataba huo unafanya kila nchi kusaidia nchi nyingine iwapo itashambuliwa.

    Soma zaidi:

  3. Raia wa Kaskazini mwa Uganda wanakabiliwa na njaa huku baa la njaa likiendelea – UN

    Mtama uliovunwa - kama inavyoonekana hapa ukibebwa na wanawake hawa - mara nyingi hutengenezwa kuwa bia huko Karamoja.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mtama uliovunwa - kama inavyoonekana hapa ukibebwa na wanawake hawa - mara nyingi hutengenezwa kuwa bia huko Karamoja.

    Zaidi ya watu nusu milioni katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Uganda la Karamoja wanakabiliwa na hatari kubwa ya baa la njaa, kulingana na utafiti wa mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa.

    Walioathirika ni takriban 40% ya wakazi katika eneo hilo.

    Katika wilaya ya Moroto pekee, zaidi ya nusu ya wakazi wanakosa mlo wowote kwa siku nzima na usiku angalau mara tatu kwa mwezi, utafiti uligundua.

    Mkoa huo pia umeshuhudia kiwango kikubwa cha utapiamlo hasa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

    Katika baadhi ya matukio, akina mama walilazimika kuwalisha watoto wao kwa pombe ya kienyeji iliyotengenezwa kwa mtama.

    Eneo hilo lenye ukame kwa kawaida huwa na msimu mmoja wa mvua kwa mwaka na limekuwa na changamoto za kihistoria za usalama wa chakula.

    Ramani ya Uganda
    Maelezo ya picha, Ramani ya Uganda

    Lakini kuongezeka kwa unyanyasaji unaohusiana na uvamizi wa ngombe na athari za janga la Covid-19 zimezidisha hali hiyo.

    Katika miezi ya hivi karibuni, serikali ya Uganda imezindua upya mpango wa kukamata bunduki kutoka kwa jamii na kurejesha amani katika eneo hilo.

    Lakini imechafuliwa na shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na upinzani kutoka kwa watu wa Karamojong.

  4. Ukraine yarejesha miili ya wanajeshi 50 zaidi

    Wengi wa kundi hilo walikuwa wamepigana kutetea kiwanda cha Azovstal

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wengi wa kundi hilo walikuwa wamepigana kutetea kiwanda cha Azovstal

    Ukraine inasema imepokea miili mingine 50 ya wanajeshi wake waliofariki kufuatia mabadilishano kama hayo na Urusi.

    Biashara hiyo ilifanyika karibu na eneo la mapigano katika mkoa wa Zaporizhzhia, ilisema taarifa ya serikali.

    Miili thelathini na saba kati ya miili hiyo ilikuwa ya watetezi wa kazi za chuma za Azovstal - ambayo ikawa ngome ya mwisho ya upinzani wa Ukraine katika mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol.

    Habari hizi zinafuatia mazungumzo ya mabadilishano mapema wiki hii ambayo yalishuhudia Ukraine na Urusi kila moja ikipokea miili 160 ya wanajeshi wao waliofariki.

    Soma zaidi:

  5. Urusi inapanga ‘kura ya maoni’ katika eneo la Zaporizhzhia

    Berdyansk ni moja ya miji ya eneo chini ya udhibiti wa Urusi

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Berdyansk ni moja ya miji ya eneo chini ya udhibiti wa Urusi

    Urusi imeashiria mipango zaidi ya kuandaa kura katika nia ya kutaka kunyakua eneo linaloshikiliwa na wanajeshi wake kusini mwa Ukraine.

    Afisa aliyewekwa katika eneo la Zaporizhzhia na Kremlin ameliambia shirika la habari la Urusi TASS kuna mipango ya kuandaa kura ya maoni ya kujiunga na Urusi.

    Hakutoa tarehe ya kura yoyote kama hiyo, lakini alisema kura hiyo itakuwa halali ikiwa kungekuwa na asilimia 50 ya watu waliojitokeza kupiga kura.

    Jana, afisa aliyewekwa rasmi na Urusi katika eneo la Kherson, alipendekeza kuwa Moscow inaweza kujaribu kupiga kura kama hiyo huko.

    Waangalizi wanasema hakuna uwezekano kwamba kura yoyote ya maoni inaweza kufanywa katika eneo ambalo uhasama mkubwa unafanyika.

    ‘’Kura ya maoni’’ mwaka wa 2014, ambayo ilishuhudia Urusi ikitwaa rasi ya Crimea ya Ukraine, ililaaniwa na mataifa ya Magharibi kuwa ni kinyume cha sheria na udanganyifu.

    Soma zaidi:

  6. Mji wa Kherson utachukuliwa 'kikamilifu' na Urusi hivi karibuni - Kremlin

    Mji wa bandari ya kusini mwa Ukraine wa Kherson - wa kwanza kuanguka katika vita - ambapo afisa wa Kremlin amesema mpango huo ni kuliweka eneo hilo kwa Urusi haraka iwezekanavyo.

    "Kujumuishwa kwa Kherson katika Shirikisho la Urusi kutakuwa na mamlaka kamili, sawa na kujiandikisha kwa Crimea," Sergei Kiriyenko, naibu mkuu wa kwanza wa utawala wa Moscow, alinukuliwa akisema katika ripoti iliyosambazwa na mbunge wa Urusi Igor Kastyukevich.

    Kiriyenko pia amesema utoaji wa pasipoti za Kirusi utaanza hivi karibuni katika jiji hilo, na utatolewa kwa "kila mkazi wa Kherson ambaye anataka" uraia wa Kirusi.

    Ramani

    Chanzo cha picha, bbc

    Maelezo ya picha, Ramani
  7. Habari za hivi punde, Ukraine imepata hasara kubwa huko Donbas - Urusi

    Ukraine inakabiliwa na "hasara kubwa miongoni mwa wanajeshi wake , silaha na zana za kijeshi" katika eneo la mashariki la Donbas, Urusi imesema katika akaunti yake hivi punde kuhusu vita.

    Wizara yake ya ulinzi inadai:

    Ukraine ilipoteza zaidi ya wanajeshi 300, mizinga sita na magari wakati wa siku tatu za mapambano katika mji wa Svyatogorsk.

    Mashambulizi ya mizinga katika eneo la Zaporizhzhia yamesababisha vifo vya "wananchi" wengine 320 wa Ukraine.

    Ndege mbili zaidi za Ukraine na helikopta zimedunguliwa katika eneo la Mykolaiv

    Makombora ya hali ya juu yamelenga shabaha ikiwa ni pamoja na viwanda na ghala la silaha ndani na karibu na mji wa Kharkiv, kaskazini.

    Haikuwezekana kwa BBC kuthibitisha kwa uhuru madai hayo.

    Urusi imejaribu kuhalalisha uvamizi wake kwa misingi kwamba inawaondoa raia wa Ukraine kutoka kwa madai ambayo yanaonekana na Kyiv na ulimwengu wa nje kama propaganda zisizo na msingi.

  8. Afrika Mashariki inakabiliwa na ‘gharama ya juu zaidi ya maisha’ kuwahi ‘’kushuhudiwa kwa miongo kadhaa’’

    Ukuaji mdogo wa uchumi, na ukosefu wa ajira vinatisha huku mfumuko wa bei ukiendelea kuongezeka
    Maelezo ya picha, Ukuaji mdogo wa uchumi, na ukosefu wa ajira vinatisha huku mfumuko wa bei ukiendelea kuongezeka

    Benki ya Dunia imepunguza kiwango chake cha makadirio ya ukuaji wa uchumi, ikitahadharisha kuwa baadhi ya nchi zinakabiliwa na mporomoko wa uchumi kwasababu ya vita ya Urusi nchini Ukraine bna virusi vya corona.

    Benki hiyo inasema Afrika Mashariki na baadhi ya maeneo ya Ulaya yaliathiriwa.

    Ilisema kuna hatari kubwa kudolola kwa ukuaji wa uchumi, na ukosefu wa ajira huku mfumuko wa bei ukiongezeka – na hali hii inaweza kurejea kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 1970, iliyosababisha kupanda kwa bei za vyakula na mafuta.

    Akizungumza na BBC, Mkuu wa Benki hiyo, David Malpass, alisema ni vigumu kutazama upande mwingine wa mzozo.

    Alisema kuwa baadhi ya nchi zinazoendelea zinakabiliwa na deni kubwa, huku serikali zikishindwa kununua bidhaa.

    Kiwango cha makadirio ya ukuaji mpya wa uchumi wa dunia cha benki hiyo kwa sasa ni cha -2.9% - kiwango hiki kikionyesha kuporomoka kwa uchumi wa dunia ambako hakujawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 80.

  9. Urusi na Ukraine: Uturuki yaweka masharti kumi kwa Sweden na Finland kujiunga na NATO

    "Sweden will strengthen Nato," Swedish PM Magdalena Andersson says

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, "Sweden itaimarisha Nato," alisema Waziri mkuu wa Sweden Magdalena Andersson

    Uturuki itaondoa kura ya veto ya uanachama wa NATO kwa Sweden na Finland iwapo mataifa hayo yatatimiza masharti kumi , limeripoti gazeti la Yeni Şafak.

    Miongoni mwa madai kuhusu Sweden na Finland ni kukataa kuwaunga mkono chama cha wafanyakazi cha kikurdi-Kurdistan Workers' Party na mashirika mengine katika kanda yanayoangaliwa na Uturuki kama magaidi.

    Uturuki inazitaka Finland na Sweden kuwa na mpango kabambe wa ‘’mapambano dhidi ya ugaidi’’, ikiwa ni pamoja na kusitisha mawasiliano na mashirika haya, kufuja mali zake na kupiga marufuku maandamano ya Wakurdi katika nchi hizi.

    Rais wa Uturuki Reccip Taib Erdogan

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais wa Uturuki Reccip Taib Erdogan

    Uturuki pia inadai kuwepo kwa ubadilushanaji wa taarifa za kijasusi na kuondoa masharti kweney sekta ya ulinzi katika mahusiano yake na Uturuki.

    Mwezi Mei, wakati vita vya Ukraine vikiendelea, Finland na Sweden zilituma maombi ya kujiunga na Muungano wa NATO. Uturuki imesema itazuwia kujiunga kwa Finland na Sweden kutokana na mataifa haya kuunga mkono vuguvugu la Wakurdi.

    Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  10. Umoja wa Mataifa wahimiza hatua za haraka kuepusha njaa nchini Somalia

    Mifugo milioni tatu wamekufa kutokana na ukame.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mifugo milioni tatu wamekufa kutokana na ukame.

    Umoja wa Mataifa umeonya kuwa Somalia inaelekea kwenye baa la njaa huku nchi hiyo ikikabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika takriban miongo minne.

    Kwa sasa, karibu nusu ya watu wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

    Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo, Adam Abdelmoula, amesema jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua sasa au watu zaidi watakufa.

    Alisema nchi iko kwenye ukingo wa njaa mbaya na iliyoenea na njaa kubwa ambayo inaweza kuchukua mamia ya maelfu ya maisha.

    Misimu minne ya mvua mfululizo imeshindwa na Umoja wa Mataifa unakadiria ukame mkali uliofuata umeathiri watu milioni saba na wengine zaidi ya 800,000 kuyahama makazi yao.

    Wakati huo huo, bei ya vyakula inapanda kwa kiasi kwa sababu ya vita nchini Ukraine - na usaidizi wa kibinadamu haupatikani kwa wengi kwa sababu ya ukosefu wa usalama na migogoro.

    Mifugo milioni tatu, ambayo ni chanzo kikuu cha maisha, wamekufa kutokana na ukame. Bw Abdelmoula alisema mwitikio kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kufikia sasa haujatosha.

    .Mnamo 2011, ukame mkali ulisababisha njaa ambayo iliua watu robo milioni.

  11. Mfalme wa Ubelgiji kuanzisha mpango wa kurejesha kazi za sanaa za DR Congo

    Mfalme Philippe, Malkia Mathilde na wajumbe wa serikali ya Ubelgij

    Chanzo cha picha, AFP

    Mfalme wa Ubelgiji yuko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ziara ya kihistoria.

    Ataanzisha urejeshaji wa vitu vya kale vilivyoporwa wakati wa utawala wa babu yake - Mfalme Leopold II - ambapo mamilioni walikufa na nchi kuporwa.

    Mfalme Philippe, Malkia Mathilde na wajumbe wa serikali ya Ubelgiji wako katika ziara ya wiki moja nchini humo - ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu awe mfalme mwaka 2013.

    Miaka miwili iliyopita, alieleza kile alichokiita majuto yake makubwa kwa majeraha ya ukoloni, chini ya Mfalme Leopold.

    Mfalme Philippe anatarajiwa kukabidhi kazi ya kwanza kati ya zaidi ya 80,000 zilizoporwa wakati wa ukoloni na kutembelea miji ya kikanda ya Lubumbashi na Bukavu.

  12. Urusi na Ukraine: Zaidi ya watu 4,000 wameuawa Ukraine tangu Februari 24

    Katika ripoti yake mpya, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imesema kuwa takriban watu 4,253 wameuawa nawengine wapatao 5141 wamejeruhiwa nchini Ukraine tangu tarehe 24 Februari.

    Watoto 272 ni mongoni mwa watu waliouawa.

    Katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa vikundi vinavyojiita DPR na LPR, watu 152 wameuawa, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, na wengine 4,001 waliosalia waliuliwa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Ukraine.

    Umoja wa Mataifa katika ripoti zake umekuwa ukisistiza kwamba inawezekana idadi ya waathiriwa ikawa ya juu zaidi kuliko inavyoripotiwa, kwani data hizi hazijakamilika.

    Ripoti hiyo pia imesema vigumu kufikia baadhi ya maeneo yanayodhibitiwa na Urusi, na Umoja huo hauna data sahihi juu ya jinsi raia walivyouawa, mfano katika Mariupol.

    Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  13. Mwanamke wa Marekani akiri kutoa mafunzo kwa wanawake wa IS Syria

    Mwanamke wa Kansas akiri kutoa mafunzo kwa wanawake wa IS Syria

    Chanzo cha picha, ALEXANDRIA SHERIFF'S OFFICE

    Maelezo ya picha, Allison Fluke-Ekren anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela

    Mwanamke Mmarekani amekiri kuongoza batalioni ya wanawake pekee ya wanawake wa kile kinachoitwa kikundi cha Islamic State nchini Syria, pamoja kupanga njama za mashambulizi katika ardhi ya Marekani.

    Allison Fluke-Ekren alikiri shitaka moja la kutoa usaidizi kwa kikundi hicho na akakiri kwamba alitoa mafunzo kwa wanawake na wasichana yatakayowawezesha kufanya mashambulizi.

    Mama na mwalimu aligeuka kuwa kiongozi wa IS na kuondoka nchini Marekani katika mwaka 2011, na kufanya kazi na kikundi hicho cha ugaidi katika taifa la Libya kabla ya kwenda Syria.

    Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela kutokana na hukumu iliyotolewa katika mwezi Oktoba.

    Fluke-Ekren, mwenye umri wa miaka 42, ambaye alikuwa mwanafunzi wa zamani wa baiolojia na mwalimu, alisafiri kwenda Syria kujiunga na kikundi hicho baada ya kuishi Misri na Uturuki.

    Alipokuwa katika IS, aliongoza bataliani yawanawake pekee inayofahamika kama Khatiba Nusaybah, yenye makao yake katika mji wa Raqqa, nchini Syria.

    Kazi yake kuu ilikuwa ni kuwafundisha wanawake na Watoto kutumia silaha, kama vile bunduki ya AK-47 , gurunedi na kutumia fulana za kujilipua, kulingana na maafisa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Allison Fluke-Ekren: Mwanamke wa Marekani anayeshikiliwa kwa kuongoza kikosi cha wanawake cha IS
  14. Merkel: Nilijaribu kuzuia hali ya sasa nchini Ukraine

    Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel

    Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel amesema alijaribu sana wakati alipokuwa uongozini kuzuia kile kinachotokea Ukraine sasa, lakini hajilaumu kwa kutoweza kufanya hivyo.

    Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipoachia wadhifa wa Kansela, katika ukumbi wa michezo wa Berlin, Merkel alisema hakuna uhalali wa vitendo vya kikatili vya Urusi.

    Alipoulizwa kuhusu uamuzi wake wa kupinga ombi la Ukraine la kutaka kujiunga na NATO mwaka wa 2008, alikiri kwamba alihofia hatua hiyo ingfanya Urusi kuidhuru Ukraine.

    Bi Merkel ameshutumiwa kwa kuiacha Ujerumani katika mazingira magumu kwa kuendeleza uhusiano wa kibiashara na Urusi.

    Bomba la Nord Stream 2 la kusafirisha gesi asilia ya Urusi moja kwa moja hadi Ujerumani lilijengwa alipokuwa kansela na kusimamishwa tu na mrithi wake, Kansela Olaf Scholz, muda mfupi kabla ya Urusi kuivamia Ukraine tarehe 24 Februari.

    Chini ya shinikizo la kuwekewa vikwazo vipya kutokana na uvamizi huo, Ujerumani inajitahidi kupunguza utegemezi wake kwa nishati ya Urusi bila kuharibu uchumi wake yenyewe.

    Lakini Bi Merkel alisema Ulaya na Urusi ni majirani ambao hawawezi kupuuzana. "Lazima tutafute njia ya kuishi pamoja licha ya tofauti zetu zote," alisema.

    Taarifa zaidi kuhusu mzozo wa ukraine:

    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Mzozo wa Ukraine: Hii ni mifano ya mbinu ya"bendera feki" vitani
    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
    • Mzozo wa UKraine: Umoja wa Ulaya wagawanyika juu ya msimamo vikwazo kwa Urusi
  15. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 08.06.2022.