Fumbo la kiroho kuhusu hali unayopitia ukikaribia kufa

    • Author, Vishva Samani
    • Nafasi, BBC World Service

"Nilikuwa mjenzi ambaye hakufanikiwa, nikiishiwa na pesa na karibu kufukuzwa kutoka kwa nyumba yangu.". Ilikuwa mwaka 2006 na maisha mjini London haikuwa ikimwendea alivyopanga.

Hali ilivyokuwa mbaya zaidi, David aliamua kwenda kuishi na dada yake nje ya mji mkuu huko Cambridgeshire. David alikuwa ametembelewa na rafiki akaamua kumsindikisha hadi kituo cha treni. Alipokuwa akimuaga sehemu ya koti lake ilifungiwa kwenye milango ya treni

Aliburuzwa kwenye reli na hatimaye aliaanguka na kuachwa na majeraha, ikiwa ni pamoja na kuumia mkono vibaya. Muda mfupi kabla ya David kikimbizwa katika chumba cha upasuaji katika hospitali iliyo karibu, alijipata katika hisia ya kiroho isio ya kawaida na isiotarajiwa.

"Niliacha mwili wangu. Nilitoka katika mazingira ya hospitali. Niliacha Maumivu yote yaliyokuwa yakipita kwenye mwili wangu na nilikuwa katika hali ya utulivu," anasema.

"Nilipotazama juu, niona mwanga mweupe ambao ulikuwa unikinijia polepole. Ulikuwa mwanga mkali lakini ulikuwa mzuri sana hivi kwamba niliweza kuitazama na kuhisi mwanga ukipita polepole katika mwili wangu wote na kuniponya."

Davod pia aliona uwepo wa viumbe wa kimalaika. "Nilihisi walikuwa wakiponya majeraha yote mwilini mwangu na kuondoa aina yote ya maumivu katika maishani mwangu, hadi kufikia kiini cha roho yangu. Nilijiona nimekamilika kwa mara ya kwanza na nikagundua kuwa nilikuwa nikichukua hatua ya maisha."

Lakini kile kilichoibuka kutokana na tukio hilo kwa David ndia cha cha kushangaza zaidi. Anaelezea hisia ya kuwa kati ya nyota na mwezi, akitazama ndani ya handaki yenye mwanga mweupi.

"Niliweza kuhisi kila kitu mwilini mwangu moja baada ya nyingine ikitetemeka kwa nishati hii ya upendo kutoka kwenye handaki hili kubwa la mwanga mweupe. Nilijua nilikuwa nikitazama chanzo cha viumbe vyote. Huyu alikuwa Mungu katika umbo la handaki hili kubwa la mwanga mweupe. Nilijawa na furaha tu."

Madhara ya kuamka kwa David kiroho yalikuwa ya haraka na ya kudumu. Anasema alipata tena matumizi ya mkono wake na haogopi tena kifo.

Bila uzoefu wowote wa hapo awali, David alikuza uwezo wa kutunga simfoni za kitamaduni na kuchora matukio wazi yanayoonyesha uzoefu wake wakati wa kupona kwake. Utunzi wake umeimbwa nchini na moja ya michoro yake kwa sasa imeonyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Biblia huko Washington, Marekani.

Hata hivyo, David hachukulii safari yake kama fumbo la kidini na badala yake anapendelea kujieleza kuwa wa kiroho

Mwamko

Dkt Steve Taylor ni mwanasaikolojia wa kiroho au mtaalamu ambaye anachunguza uhusiano kati ya mateso makali na uzoefu wa kiroho usioelezeka. Anasema kukutana na hali kama ya David ni jambo la kushangaza na imesababisha idadi kubwa ya watu kujitambulisha kuwa wa kiroho.

"Unapokabiliwa na tukio la karibu kufa ni jambo la kushangaza sana, lenye nguvu sana, ni kali zaidi kuliko ufahamu wa kawaida hivi kwamba maono yako ya ukweli yanabadilishwa milele.

"Mara nyingi hutokea kwa watu ambao walikuwa na mtazamo wa kilimwengu wa maisha na hata baadaye sio lazima wawe watu wa kidini kwa njia ya kawaida," anasema Dk Taylor, mhadhiri mkuu katika Chuo Kikuu cha Leeds Beckett.

Anasema baadhi hutafsiri hali kama hiyo kwa maneno ya kidini lakini anasisitiza sio dhana na inahusisha kuacha imani, na kupata nyingine mpya. Nadharia maarufu za kisayansi zinaonyesha kuwa mtu hukaribia kifo kutokana na ukosefu wa oksijeni katika ubongo.

Lakini Dk Taylor anasema utafiti katika eneo hili haujumuishi maelezo madhubuti ya kisayansi. Pia anaangazia mwiko katika kuzijadili kwa sababu zinapingana na mtazamo wa kawaida wa kisayansi wa ukweli.

"Matukio haya yanaonyesha kwamba fahamu si lazima upotee katika bidhaa ya sehemu ya ubongo kwani inaweza kuathiri sehemu ya mwili," anasema Dk Taylor.

Ukosefu wa usaidizi unaopatikana wa kujadili hali kama hiyo na ulionekana kuwa changamoto kwa Gigi Strehler. Yeye ni mwigizaji kutoka London Kaskazini ambaye alianzisha kikundi cha 'Near-Death Experience UK' mnamo 2014 baada ya kukaribia kupoteza uhai hospitalini.

"Nilipata umbwe badala ya kile ambacho mara nyingi hujulikana kama handaki la mwanga. Kwa hivyo sikuwa kitu na mahali popote. Ilijaa amani na hisia ya upendo. Sikuwa Gigi, lakini bado nilikuwepo -bado alikuwa na ufahamu.

"Mahali hapo palikuwa pazuri kuliko ulimwengu huu ambao unahisi kama ulimwengu wa ndoto unaporudi," anasema Gigi.

Baadaye, alipata mabadiliko makubwa ya kibinafsi kama vile kuelewa fizikia. Ilimsukuma kutafuta majibu kutoka kwa desturi za kidini kwa miaka mingi, ili kupata ufumbuzi zaidi.

Lakini hakuna hata mmoja wao aliyemridhisha, na Gigi sasa ana msimamo usio na utata kuhusu dini rasmi.

"Uzoefu wangu ulinifundisha kwamba ufahamu wetu na uwepo wetu unapita miundo yote ya wanadamu. Lakini ninaamini kwamba sote tumeunganishwa kwa njia ya ajabu."

David Ditchfield ana mtazamo sawa. Yeye ni wa kiroho sana na anaheshimu desturi za kidini lakini yeye mwenyewe hajazingatia dini kikamilifu.

Dk Steve Taylor bado anavutiwa na uzoefu wa 'kiroho' wa David na Gigi lakini anakubali kuwa ni wa ajabu sana kwa wengi kukubali.

"Tunapenda kujivunia kama wanadamu kwamba tunaweza kueleza hisia zetu lakini kuna kiwango ambacho tukifika hatuwezi kujieleza tukaeleweka. Kuna baadhi ya mambo ambayo ni ya ajabu sana kuyaelewa."