Ukifuata haya, mende hawataingia nyumbani kwako

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wengi hasa wanawake wanaogopa mende.
Nilipokuwa na umri wa miaka sita, nilikuwa nikitoa chupa jikoni, mende aliporuka na kutua kwenye shingo yangu. Nilipiga kelele kwa woga na kudondosha chupa ikavunjika. Kabla pia niliona mende.
Nyumbani kwetu, kaka na dada zangu hucheza na mende. Ukweli nachukizwa.
Kwa kweli, inavyoonekana sasa ni kwamba watu hawahitaji kuogopa mende.
Kwa sababu hawanywi damu yetu kama mbu na wadudu wengine.
Hata hivyo, anasema Bronoy, mtaalamu wa wadudu katika Taasisi ya Utafiti wa Ikolojia ya Misitu, mende hao huishi katika maeneo yenye uchafu.
“Kwa kawaida mende hupatikana sehemu chafu, za takataka, vyooni n.k ndiyo maana wanachukiwa na watu wengi,” alisema Bronoy.
Bronoy alisema hofu ya magonjwa kutoka kwa mende ilianzia Ugiriki ya kale.
"Wakati wa Wagiriki wa kale, mende walihofiwa kusababisha magonjwa. Mende wana protini inayoitwa tropomyosin. Protini hii kwenye kinyesi cha mende, ngozi na sehemu za mwili inaweza kusababisha mzio kwa binadamu," alisema Bronoy.
Wamisri wa kale waliabudu miungu ili kuwafukuza mende.
Katika maneno ya kimatibabu hofu au kuchukia mende hujulikana kama 'Catasaridaphobia'.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, magonjwa huenezwaje na mende?
Selvamuthukumaran, Profesa Mshiriki wa Idara ya Entomolojia, anasema kwamba mende hawaambukizi moja kwa moja ugonjwa wowote kwa wanadamu.
Malaria, dengue na magonjwa mengine huenezwa na mbu. Kipindupindu huenezwa na nzi. Lakini mende hawasambazi magonjwa moja kwa moja kwa wanadamu. Walakini, vitu vinavyooza ambavyo mende hula vina vijidudu. Baada ya kula hivi vitu, mende wanapoingia kwenye chakula tunachokula, vijidudu hivi huchanganyika na vyakula vyetu na kutusababishia magonjwa,” alisema Selva.

Chanzo cha picha, Getty Images
Namna ya kudhibiti mende kuingia kwenye nyumba?
Selvamuthukumaran anaeleza kuwa mende haishi vyema mahali penye chakula na mazingira yenye unyevunyevu, na kwamba usafi ukifuatwa, hawatakuja.
- Osha sahani zilizoliwa chakula mara moja. Chakula chochote kilichobaki kinapaswa kutupwa mara moja.
- Hakikisha kwamba takataka hazikusanyiki ndani ya nyumba. Makopo ya takataka unayotumia yanapaswa kufungwa. Yanapaswa kuwekwa nje ya nyumba usiku.
- Mende wanaweza kuingia kupitia madirishani na milangoni. Kwa hivyo unapaswa kufunga milango na madirisha wakati hauitumii.
- Makabati na masanduku ya mbao ni kivutio kwa mende, chunga sana, kwa sababu kuna aina ya mbao kwao ni chakula bora kwa mende.
- Mende wengi huingia majumbani kupitia karo za vyombo. Kwa hivyo, ni bora kuzitunza na kuzifunika wakati wa usiku.
- Dawa za kupuliza hutumiwa kufukuza mende kutoka ndani ya nyumba. Hata hivyo, matumizi zaidi ya dawa za aina hizi yanaweza pia kuwa na madhara kwa wanadamu.












