Watumiaji wa Twitter wageukia Mastodon - lakini hii ni nini?

Mastodon

Chanzo cha picha, NURPHOTO

Baada ya Elon Musk kuchukua uongozi wa Twitter, baadhi ya watumiaji wamekuwa wakitafuta majukwa mbadala. Mnufaikaji mkubwa ni Mastodon. Lakini ni nini?

Mtandao huo wa kijamii unasema sasa ina zaidi ua watumiaji 655,000 us – baada y azadi ya watumiaji 230,000 kujiunga nao wiki iliyopita.

Mastodon inaonekana kama Twitter – watumiaji wanaandika ujumbe (unaoitwa "toots"), ambao unaweza kujibiwa, kupendwa na kushirikishwa, na pia watumiaji kufuatiliana.

Lakini kilichojitokeza ni kwamba, mtandao huu unafanya kazi kwa njia tofauti.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Jukwaa hili limekuwepo kwa miaka sita lakini shughuli yake ya sasa ni ya kipekee na inajitahidi kumudu ongezeko la watumiaji wapya.

Huu hapa ni mwongozo mfupi utakaokusaidia kuelewa mtandao wa Mastodon unavyofanya kazi.

Hizi seva zote ni za nini?

Jambo la kwanza unapaswa kufanya unapojisajili ni kuchagua seva.

Kuna seva nyingi na yote yana mada - zilizogawanywa kwa nchi, jiji au mahitaji - kama vile Uingereza, kijamii, teknolojia, michezo ya kubahatisha na kadhalika.

Haijalishi umejiunga na seva ipi kwa sababu utaweza kufuatilia watumiaji wengine wote, lakini inakujumuisha katika jamii ambayo ya ina uwezekano mkubwa wa kuchapisha mambo ambayo yanayokuvutia pia.

Baadhi ya zile maarufu - kama vile za kijamii na Uingereza - kwa sasa zinaendelea polepole sana kwa sababu ya mahitaji.

Ryan Wild, ambaye anaendesha seva ya MastodonApp.UK kupitia kampuni yake ya Superior Networks, anasema alikuwa na washiriki wapya zaidi ya 6,000 ndani ya saa 24 na ilibidi asitishe usajili.

Unapataje watu?

Seva unayochagua inakuwa sehemu ya jina lako la mtumiaji - kwa mfano, nilitumia utambulisho wangu wa sasa wa Twitter, zsk, na kuchagua seva ya Uingereza, na kufanya jina langu la mtumiaji @zsk@mastodonapp.uk. Na hiyo ndiyo anwani yangu hapo - utafuta nini ili unipate?

Ikiwa uko kwenye seva moja, unaweza kutafuta tu kwa kutumia jina la mtu huyo, lakini ikiwa yuko kwenye seva tofauti utahitaji anwani yake kamili. Tofauti na Twitter, Mastodon haitapendekeza wafuasi ambao unaweza kuwa na hamu.

Ikiwa uko kwenye seva moja, unaweza kutafuta tu kwa kutumia jina la mtu huyo, lakini ikiwa yuko kwenye seva tofauti utahitaji anwani yake kamili.

Tofauti na Twitter, Mastodon haitapendekeza wafuasi ambao unaweza kuwa na hamu. Unaweza pia kutafuta hashtag.

Kwa nini kuna seva?

Hii ni ngumu, lakini nitajaribu kuelezea. Mastodon sio jukwaa moja.

Sio "kitu" kimoja na haimilikiwi na mtu mmoja au kampuni.

Seva hizi zote tofauti huunganishwa pamoja, na kuunda mtandao wa pamoja, lakini zinamilikiwa na watu na mashirika tofauti.

MASTODON

Chanzo cha picha, MASTODON

Mfumo huu unaitwa kugatuliwa, na mashabiki wa majukwaa yaliyogatuliwa kama wao kwa sababu hii haswa - hayawezi kuendeshwa kwa matakwa ya chombo kimoja, kununuliwa au kuuzwa.

Mastodon inawaomba wamiliki wa seva kuwapa watumiaji wao notisi ya miezi mitatu ikiwa wataamua kuifunga.

Mwanzilishi wa awali wa Twitter, Jack Dorsey, anafanya kazi kwenye mtandao mpya uitwao BlueSky, pembeni - na amesema anataka hilo pia kugawanywa.

Mastodon inasimamiwa vipi?

Ni suala tata lakini kwa sasa seva zote zina sheria zao za udhibiti, na zingine hazina.

Baadhi ya seva zinachagua kutounganishwa na zingine ambazo zimejaa roboti au zinaonekana kuwa na idadi kubwa ya maudhui ya chuki - hii inamaanisha kuwa hazitaonekana kwa wale walio kwenye seva ambako zimedhibitiwa. Machapisho yanaweza pia kuripotiwa kwa wamiliki wa seva.

Ikiwa ni matamshi ya chuki au maudhui yanayokiuka sheria basi wamiliki hao wanaweza kuifuta - lakini hiyo si lazima ifute kila mahali.

Litakuwa suala kubwa jukwaa hili likiendelea kukua.

Tayari kuna ripoti za watu kulengwa na maudhui ya chuki na BBC imeona mifano ya unyanyasaji wa wapenzi wa jinsia moja.

Je, kuna matangazo yoyote?

Hapana. Hakuna matangazo ingawa pia hakuna kitu cha kukuzuia kuandika chapisho la kukuza kampuni au bidhaa yako.

Mastodon pia haitoi ujumbe ulioratibiwa kama inavyofanya Twitter bali mtumiaji anapata ujumbe kulingana na jinsi ulivyochapishwa - kwa ujumla unaona kile wafuasi wako wanasema, kama jinsi ilivyo.

Je, ni bure kutumia?

Inategemea umejiunga na seva gani - sbaadhi zinaomba mchango, kwa sababu hawapati malipo lakini huduma ya Mastodon ya ni bure kwa kiwango kikubwa.