Phil Foden v Jude Bellingham: Vita vya kuwania nambari 10 ya England

Manchester City na Real Madrid zilicheza mechi yao ya robo fainali ambapo City waliondolewa katika michuano hiyo na Real Madrid.

Mechi hiyo hatahivyo ilikuwa kubwa kuwapima wachezaji wawili wa England wanaopigania jezi moja ya England, Phil Foden wa Manchester City na Jude Belligham wa Real Madrid.

Phil Foden ameng’aa katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu kwa kiwango chake akiwa na City, huku kiwango cha Jude Bellingham akiwa na Real Madrid kikivutia kote Ulaya.

Wachezaji wote wawili watakuwa muhimu kwa England kwenye Euro 2024, lakini kocha Gareth Southgate ana mtanziko - ni nani atacheza nafasi ya namba 10?

Wote wawili walicheza namba kumi katika vilabu vyao katika mechi ya kwanza iliyovutia mno, ambayo ilimalizika kwa mabao 3-3 mjini Madrid wiki iliyopita.

Foden alichezaji vizuri sana, akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi baada ya kufunga katika kipindi cha pili, akicheza katika nafasi ambayo amecheza mara tisa akiwa na City msimu huu.

Bellingham amecheza mechi 24 kwenye nafasi hiyo akiwa na Real na ana uwezekano wa kucheza tena nafasi hiyo katika mechi ya marudiano Jumatano. Lakini wachezaji hao wanalingana vipi kitakwimu?

Je, takwimu zinasema nini?

Tovuti ya takwimu za kandanda WhoScored Foden ana mabao saba na pasi za mwisho tatu katika mechi 10, na kuchangia mabao zaidi (12) kutoka upande wa kulia, ambapo amecheza mara 18 katika mashindano yote kwa klabu na nchi.

Bellingham amechangia mabao 24 (mabao 16, pasi za mwisho nane) kama kiungo mshambuliaji, lakini amecheza mara nyingi zaidi katika nafasi hiyo kuliko Foden msimu huu.

Nyota huyo wa Real Madrid kwa ujumla anaonekana kufanya vyema zaidi katikati - pia ana mabao mawili na pasi ya mwisho moja katika mechi 12 katika nafasi ya kiungo wa kati.

Kwa England, Bellingham amekuwa ndio namba 10 msimu huu. Ameanza mechi nne kama kiungo mshambuliaji, mchezo mmoja upande wa kushoto na alipumzishwa katika mechi ya kirafiki ya Oktoba dhidi ya Australia.

Bellingham aliumia mwezi Novemba, Foden alianza dhidi ya Macedonia Kaskazini akiwa na jezi namba 10 - mara yake ya kwanza kuvaa hivyo chini ya Southgate msimu huu.

Msimamo bora wa Foden ni upi unabaki kuwa mjadala, ingawa alisema mwaka huu "100%" anapendelea kucheza nambari 10.

Beki wa zamani wa Manchester City, Micah Richards aliiambia BBC "Wakati mwingine ninapomtazama Phil Foden akicheza mbali na katikati, nahisi kama anatengwa.

"Lakini yeye huchagua nafasi za kati kati kama safu ya kiungo na safu ya ulinzi. Hata akiwa mlinzi hushuka sana, anaweza kufika katikati ya uwanja na kupiga pasi. Kwa hivyo napenda awe katikati."

Alipoulizwa kuhusu kumtumia mara nyingi zaidi, kocha wa England Southgate alisema: "Hhachezi mara nyingi kwa klabu yake. Inawezekana kuna sababu. Inategemea kiwango cha mchezo.

"Katikati ya uwanja, kila mtu anataka kuzungumza juu ya "na mpira" lakini kuna maelezo mengi bila mpira.

"Itabidi uzungumze na Pep [Guardiola], ambaye ni kocha bora zaidi duniani, anayemchezesha kutoka pembeni."

Ingawa Bellingham kuna nyakati amekuwa akicheza nafasi ya kiungo mlinzi kwa sababu ya uwezo wake wa kujilinda, Southgate anamuona wazi kama nambari 10, ambapo amefanikiwa kwa Real Madrid.

Kabla ya mkondo wa kwanza wa mchujo wao wa robo fainali, bosi wa City Guardiola alisema Bellingham amekuwa na "athari kubwa" tangu kuhamia Uhispania.

"Real Madrid nit imu tofauti na msimu uliopita. Athari yake ni kubwa, na inabidi tujaribu kugundua anachofanya ili kuidhibiti."

Je, unadhani nani anafaa kuwa namba 10 wa England?