Enzi ambayo watoto wa Marekani walisafirishwa kwa posta kama 'barua'

Kulikuwa na wakati ambapo barua ziliweza kutumwa Ulaya kupitia posta za Marekani pekee lakini uwasilishaji wa barua ulipoanza kupatikana mwaka wa 1913, maeneo ya mashambani yalitumia fursa hii kikamilifu.

Badala ya safari za gharama kubwa hadi miji ya mbali, walipata kituo chao cha kutoa huduma za posta ambacho watu walitumia kusafirisha bidhaa kama siagi, mayai, kuku, vifaranga, huwezi kuamini hata watoto wao wadogo kutoka sehemu moja au jiji hadi jingine.

Ndio. Huu ni ukweli mtupu. Watoto walikuwa wakisafirishwa kwa namna hii kama vifurushi na wazazi wao si tu kwa sababu ya imani yao katika Huduma ya Posta ya Marekani, bali pia kwa sababu walikuwa wakitafuta njia ya usafiri ya gharama ya chini.

Kwa kweli, kwa wazazi wengine, usafiri wa reli au basi ulikuwa wa gharama kubwa, kwa hivyo walifikiri kwa nini wasitumie huduma hii mpya iliyokuwa tu ndio imeanzishwa na kuwajumuisha watoto kama mzigo.

Kulingana na utafiti wa Joe Silvia, wanandoa wa Beagle katika jimbo la Ohio nchini Marekani walikuwa karibu kumpeleka mtoto wao mchanga kwa bibi yake umbali wa maili moja kwa njia hii ya posta.

Vernon O'Little mhudumu wa posta alimwasilisha mtoto wao salama hadi mahali alipotakiwa kupelekwa, ambapo familia ya Beagle ililazimika kulipa tu ada iliyopunguzwa ya senti 15, lakini kwa bima ya $50.

Tukio hilo liliripotiwa katika gazeti la New York Times.

Habari ilikuwa kwamba 'mhudumu wa posta alipofika kumchukua mtoto, alikuwa amefungwa vizuri na tayari kutumwa kama barua.

Bw. Little (mhudumu wa posta) alimpeleka mvulana huyo salama kwenye anwani iliyokuwa imewekwa katika kadi, ambayo ni nyumbani kwa bibi ya mvulana huyo, Bi. Louise Beagle.

Habari hizi zilipochapishwa, Mkuu wa posta wa Marekani Frank Hitchcock alipokea ombi kutoka kwa mtu mmoja ambaye alitaka kuasili mtoto huyo.

Ombi hilo lilisomeka hivi, 'Naomba niulize ni masharti gani yaliyopo ya kifurushi cha (mtoto) kulingana na kanuni kiasi cha kuruhusiwa kusafirishwa kama kifurushi, kwani barua zinazowasilishwa kwa njia ya haraka zinashughulikiwa vibaya sana.

Kufuatia ombi hili kutoka Pennsylvania, ofisi ya Mkuu wa Posta Marekani ililazimika kutoa taarifa kwamba ''watoto, kwa maoni ya Mkuu huyo, si wa kundi la nyuki na wadudu, viumbe hai tu ambavyo vinaweza kusafirishwa kwa njia ya posta.''

Lakini bado kesi zaidi za kutuma watoto kwa njia ya barua ziliendelea kujitokeza.

Mwanamke mmoja huko Oklahoma alipomtuma mjukuu wake wa miaka miwili kwa shangazi yake eneo la Wellington, Kansas, gazeti la New York Times liliripoti kwamba 'mvulana huyo alikuwa na utambulisho shingoni ukionyesha kwamba ana umri wa miezi 18 alipotumiwa.

Alisafiri maili 25 kwa barabara kabla ya kufikia njia za reli. Alisafiri pamoja na wahudumu wa posta, akala nao chakula cha mchana pamoja na kuwasilishwa alipokuwa kielekea akiwa katika hali nzuri.

Tukio la kufurahisha lilitokea mnamo Juni 1914 wakati mwanamke 'alipomtuma' mtoto wake wa miaka miwili kwa baba yake, Henry Euler, huko La Porte.

Mamake Euler alikataa kumkubali 'mtoto' huyo kama kifurushi kwa sababu binti-mkwe wake alikuwa ametalakiwa. Kesi ilifunguliwa.

Mtoto huyo akawa amekwama katika ofisi ya posta kaunti ya LaPorte eneo la mashambani.

The Star iliandika, 'Inaonekana alitakiwa kwenda kwa ofisi ya posta lakini mtafaruku huo ulimalizika pale Euler alipodai mtot wake.

Haya hivyo, mtoto alifurahia safari hiyo, labda kwa sababu alisafirishwa kwa gari.'

Kesi maarufu zaidi ya watoto kusafirishwa kama vifurushi ni ile ya Charlotte May Pierstorff, ambaye alitumwa kwa gari-moshi Februari 19, 1914, kwa babu na bibi yake, walioishi umbali wa maili 73.

Alexandra Denzer aliandika kwamba 'May alitamani sana kukutana na bibi yake Mary, ambaye alisema aliishi maili milioni moja katika milima ya zamani ya Idaho.'

Lakini familia ya May haikuweza kumudu tikiti ya gari moshi ili kutimiza ndoto hii, kwa hivyo walipata suluhu la kumpeleka May nyumbani kwa babu yake huko Grangeville, Idaho.

Baada ya tukio hili, Mkuu wa posta wa Marekani Burleson alipiga marufuku kutuma watoto kwa barua.

Hata hivyo, mwezi mmoja tu baada ya tangazo hilo, mhudumu wa posta BH Kniper alimwasilisha mtoto mwenye uzito wa pauni 14 nyumbani kwa mama yake huko Clear Spring, Maryland, maili 12 kutoka nyumbani kwa bibi yake.

Mnamo Februari 25, 1915, mhudumu wa posta Missouri Charles Hayes alimkabidhi binti wa Combs Helen kupitia njia ya posta kwa senti 10 kwa bibi yake, ambaye nyumba yake ilikuwa njiani.

Kulingana na Alexandra Danzer, sababu iliyofanya mtindo huo kuendelea ni kwa sababu usafiri wa treni ulikuwa ghali sana,

Pili, watu walikuwa na imani na wafanyakazi wa huduma za posta.

Historia pia inasema msichana wa miaka 9 ambaye alienda kwenye ofisi ya posta huko Washington City mwenyewe ili kutumwa Kentucky, lakini alikataliwa.