Tetesi tano kubwa za soka jioni hii

Kipa Dean Henderson amekamilisha vipimo vyake vya afya kabla ya kuondoka Manchester United kwenda Crystal Palace.

Ada inadaiwa kukaribia pauni milioni 20.

Baada ya yote kukamilika, United itashinikiza kukamilisha dili la Altay Bayindir kutoka Fenerbahce kwa takriban £4.3m.

United wanataka suluhu ifikie tarehe ya mwisho ya usajili saa sita mchana Ijumaa ili wasijiache fupi kwa safari ya Jumapili kwenda Arsenal, ambayo itaonyeshwa moja kwa moja kwenye Sky Sports.

Waendesha mashtaka wa Uhispania wanasema wameanzisha uchunguzi wa awali wa unyanyasaji wa kingono dhidi ya rais wa shirikisho la soka la Uhispania Luis Rubiales.

Rubiales, 46, amekosolewa vikali baada ya kumbusu mshambuliaji Jenni Hermoso kwenye midomo kufuatia ushindi wa fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake la Uhispania

Mkufunzi wa Fulham Marco Silva anasema klabu hiyo "inakaribia sana" kumsajili beki wa pembeni Timothy Castagne kutoka Leicester.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hajachezea Leicester msimu huu na ameingia miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake wa Foxes.

Silva alisema: "Haijakamilika kwa asilimia 100.''

Mabingwa wa Qatar Al Duhail wamefanya mazungumzo kuhusu usajili wa Philippe Coutinho kutoka Aston Villa.

Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 31 amepewa ofa kubwa ambayo inazingatiwa.

Coutinho ana kandarasi ya kuinoa Villa hadi 2026.

Villa ilimsajili kwa pauni milioni 17 kutoka Barcelona msimu uliopita baada ya kuonyesha umahiri mkubwa alipokuwa kwa mkopo.

Fulham wanatarajia Willian kusalia licha ya kunyatiwa na klabu moja ya Abu Dhabi.

Klabu ya Saudi Pro League, Al Shabab pia ilijaribu kumsajili Mbrazil huyo mwanzoni mwa mwezi huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alitia saini kandarasi mpya ya mwaka mmoja Fulham mwezi uliopita.

Willian alikosa sare ya 2-2 dhidi ya Arsenal siku ya Jumamosi kwa sababu ya jeraha la misuli.