Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 22.11.2024: Manchester United wana nia ya kumsajili tena kiungo wa Uingereza Angel Gomes

Angel Gomes alicheza mechi yake ya kwanza England chini ya Lee Carsley

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Angel Gomes alicheza mechi yake ya kwanza England chini ya Lee Carsley
Muda wa kusoma: Dakika 4

Manchester United wanataka kumrejesha mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Old Trafford kwa uhamisho wa bure, Klabu za Ligi ya Premia vinamuwania mshambuliaji wa Paris St Germain Randal Kolo Muani, Arsenal tayari kumpa Leandro Trossard mkataba mpya.

Manchester United wana nia ya kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 24, kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake na Lille utakapokamilika msimu ujao. (Mail)

Wakati huohuo, United wako tayari kumenyena na Real Madrid kumsajili winga wa Atalanta Ademola Lookman. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 27 anaweza kununuliwa katika majira ya joto. (Caught Offside)

United pia imewasiliana na Paris St-Germain kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 25, kwa mkopo mwezi Januari. (Le 10 Sport - kwa Kifaransa)

Ademola Lookman

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wakati huohuo, United wako tayari kumenyena na Real Madrid kumsajili winga wa Atalanta Ademola Lookman

West Ham na Newcastle ni miongoni mwa klabu nne za Ligi Kuu ya England zinazomtaka mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufarans Kolo Muani, ambaye PSG wanatazamiwa kumuuza kwa mkopo. (Caught Offside)

Klabu hizo mbili, pamoja na wapinzani wa Ligi ya Premia Everton na Nottingham Forest pia zinamfuatilia mshambuliaji wa Brazil Yuri Alberto, 23, wa Corinthians ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 17. (TBR)

Newcastle huenda wakasitisha mpango wa kumnunua mlinzi wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 24, baada ya mlinzi wao Mholanzi Sven Botman kupona jeraha. (Time - usajili unahitajika)

Arsenal wanajadiliana na winga wa Ubelgiji Leandro Trossard, 29, kuhusu kandarasi mpya ambayo itajumuisha nyongeza kubwa ya mishahara. (Mail)

Real Madrid inamatumaini kuwa beki wa Canada Alphonso Davies, 24, atajiunga nao kutoka Bayern Munich kwa uhamisho wa bila malipo msimu huu wajoto licha ya wakala wake kudokeza kwamba anaweza kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Bundesliga. (AS - kwa Kihispania)

Mtendaji mkuu wa zamani wa Liverpool Peter Moore amesema wamiliki wa klabu hiyo wanafanya kazi kwa bidii ili kupata kandarasi mpya zilizokubaliwa na winga wa Misri Mohamed Salah, 32, beki wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, na beki wa kati wa Uholanzi Virgil Van Dijk. , 33. (Sky Sports)

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Edin Terzic, mkufunzi wa zamani wa Denmark Kasper Hjulmand, Sebastian Hoeness wa Stuttgart na Roger Schmidt, aliyewahi kuichezea Bayer Leverkusen na Benfica, wako kwenye orodha ya walioteuliwa na West Ham iwapo wataamua kuchukua nafasi ya Julien Lopetegui. (Mirror)

Leandro Trossard,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal wanajadiliana na winga wa Ubelgiji Leandro Trossard, 29, kuhusu kandarasi mpya

Manchester City wanaweza kusubiri hadi mwisho wa Machi ili kujua uamuzi wa tume ya nidhamu kuhusu mashtaka 115 dhidi yao kwa madai ya kukiuka kanuni za kifedha za Ligi ya Premia. (Football Insider)

Mkataba mpya wa Pep Guardiola na City hauna kipengee cha mapumziko iwapo watashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia endapo watapatikana na hatia ya kufadhili makosa. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kiungo wa Burnley Josh Brownhill, 28, ananyatiwa na Lazio, Fiorentina na Torino huku kandarasi yake huko Turf Moor ikitarajiwa kumalizika msimu ujao. (Calciomercato kupitia Football Italia)

Juventus wanaweza kumsajili beki wa Chelsea Ben Chilwell kwa mkopo mwezi Januari, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akitafuta muda wa kucheza baada ya kuachwa nje ya kikosi cha The Blues na Enzo Maresca. (Barua, nje)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Yusuf Jumah