Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Manchester United mbioni kumsajili Victor Osimhen

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United wamemfanya mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray, kuwa mlengwa wao mkuu wa uhamisho wa wachezaji mwishoni mwa msimu huu. (Mirror).

Manchester United inapanga kumlipa Matheus Cunha pauni za Uingereza milioni 62.5 kwa awamu, huku Wolves wakiwa tayari kufikia malipo yanayohitajika kumpata mshambuliaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph).

Klabu za Arsenal, Newcastle na Nottingham Forest zina nia ya kumsajili Cunha. (Sportsport)

Aston Villa ipo tayari kupambana na Arsenal na Manchester City katika usajili wa kiungo wa kati wa Rosenborg raia wa Norway wa umri chini ya miaka 21 Sverre Nypan, 18. (Times - usajili).

Manchester United pia inapanga kutumia kipengele cha kutolewa kwa pauni milioni 30 katika kandarasi ya mshambuliaji wa Ipswich, Muingereza Liam Delap, 22. (Mail- usajili unahitajika).

Kocha Ange Postecoglou huenda akaondoka Tottenham hata kama klabu hiyo itashinda Ligi ya Europa na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. (Telegraph - usajili unahitajika).

Mkufunzi wa Bournemouth Andoni Iraola, Marco Silva wa Fulham na Scott Parker wa Burnley wanatarajiwa kurithi mikoba ya Postecoglou. (Mail).

Bayer Leverkusen wamefanya mazungumzo na Manchester City kuhusu mkataba wa kumnunua mshambuliaji raia wa Uingereza James McAtee, 22. (Florian Plettenberg)

Bayer Leverkusen imefanya mazungumzo na Manchester City kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Uingereza James McAtee, 22. (Florian Plettenberg)

Lee Carsley, Danny Rohl na Russell Martin wako kwenye orodha ya walioteuliwa na Leicester iwapo wataamua kumtimua kocha Ruud van Nistelrooy. (Sky Sports)

Chelsea imejiunga na kinyang'anyiro cha kumnasa mlinda lango wa Porto Diogo Costa, 25, na watashindana na Manchester United kuwania saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno. (Team talk)

Manchester City pia wanamfuatilia Costa kama mbadala wa kipa wa Brazil Ederson, 31, ambaye anajadiliana na klabu za Saudi Arabia. (Florian Plettenberg)

Newcastle inavutiwa na mshambuliaji wa Strasbourg Mholanzi Emanuel Emegha, 22. (L'Equipe - kwa Kifaransa, usajili unahitajika)

Everton inamnyatia beki wa Feyenoord na Slovakia David Hancko, 27, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Juventus, Atletico Madrid na Bayer Leverkusen. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano)

Winga wa West Ham na Ghana Mohammed Kudus, 24, analengwa zaidi na klabu ya Saudia ya Al-Nassr. (Football Insider)

Klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal inavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 28 wa Brazil Raphinha. (Sport - kwa Kihispania)

Klabu za Manchester City, Liverpool na Arsenal zinamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen wa Ujerumani Florian Wirtz, ambaye thamani yake ni takriban pauni milioni 103. (CaughtOffside)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi