Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nilimwona mwanariadha akiwaka moto akikimbilia kwangu, jirani aiambia BBC
- Author, Celestine Karoney/Robert Kiptoo
- Nafasi, BBC Eldoret
- Muda wa kusoma: Dakika 3
Onyo: Makala haya yana maelezo ambayo yanaweza kuwatatiza baadhi ya wasomaji
Nje ya nyumba alikoishi mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei, waombolezaji wameweka shada la maua, katika eneo ambalo nyasi ziliungua wakati mwanariadha huyo alipoanguka wakati alipokuwa akijaribu kuokoa maisha yake.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miakaa 33, alifariki siku ya Alhamisi, kutokana na majeraha hayo ya moto.
Mpenzi wake wa zamani anadaiwa kummwagia mafuta ya petroli kisha kumchoma moto, mbele ya watoto wake wawili.
Mti mmoja nje ya nyumba hii iliyoko viungani mwa mji wa Kitale, Magharibi mwa Kenya, unaendelea kuonesha makovu ya shambulio hilo la kikatili. Mti huu uliteketea wakati Rebecca alipokuwa akijaribu kuzima moto ambao ulikuwa umemfunika mwilini mwake.
Bi Agness Barabara ambaye ni jirani wa Rebecca , amesema kuwa wakati wa tukio hilo, alikuwa nyumbani kwake na mara tu akasikia kelele kutoka kwa jirani yake, akiomba usaidizi.
‘’Wakati nilipokwenda kutafuta maji, na kuwaita majirani zaidi waje watusaidie, mpenzi wake naye pia akijitokeza, na kumumwagia petroli zaidi, lakini kwa bahati mbaya naye pia aliungua vibaya.
Alikimbia katika shamba langu ili kujaribu kuzima moto. Sisi Pamoja na majirani wengine tukamsaidia Rebecca.’’ Alisema Bi Barabara.
Jirani mwingine ambaye naye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa familia ya Rebecca imekuwa na malumbano ya mara ya kwa mara, na kuwa hajawahi kuona tukio kama hilo.
Polisi sasa nchini Kenya wamesema kuwa watamfungulia mashtaka ya mauaji mpenzi wake wa zamani.
Polisi pia wamethibitisha kuwa wawili hao wamekuwa na mzozo wa
muda mrefu sana kuhusu umiliki wa kipande cha ardhi ambacho Rebecca alikuwa akiishi.
Mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani, punde tu atakaporuhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitani.
Afisa mkuu wa upelelezi katika kaunti ya Trans Nzoia Kenneddy Apindi amesema kuwa uchunguzi wao, umekamilika na kuwa mshukiwa huyo atawajibishwa kutokana na matendo yake.
Mama yake Rebecca, Agness, amesema kuwa mtoto wake alikuwa mtu mtiifu na mkarimu maishani mwake.
Emmanuel Kimutai ambaye ni rafiki na Jirani ambaye walisoma pamoja na Rebecca amemtaja kama mtu alikuwa na maono na alijitolea kuwasaidia watu katika Kijiji chao.
Rebecca Cheptegei, alizaliwa katika eneo la Kitum, katika mpaka wa Kenya na Uganda, lakini aliamua kuakilisha taifa la Uganda, ili kufanikisha azma yake ya riadha.
Baada ya kujiunga na riadha, Rebecca alisajiliwa kama mwanajeshi wa Jeshi la Uganda UPDF mwaka wa 2008 ambako amepnda cheo na hadi kifo chake alikuwa Sergent.
Katika Maisha yake ya riadha aliwakilisha Uganda katika mashindao ya olimpiki yaliyofanyika mjini Paris mwezi uliopita na kumaliza katika nafasi ya 44.
Licha ya kutoshinda medali yoyote, Rebecca bado ni shujaa katika eneo la Bukwa Mwashariki mwa Uganda, eneo ambalo atazikwa.
Aliishi katika Kijiji cha Chepkum, kilichoka katika eneo la Endebes takribani kilomita 25 kutoka mpaka wa Uganda, eneo ambalo ni maarufu sana kwa kilimo cha nafaka.
Wakaazi wa Kijiji hiki pia ni wafugaji wa mifugo. Eneo hilo la ujumla liko katika kaunti ya Trans Nzoia ambalo lina sifa ya kuzalisha zaidi ya asilimia 85 ya nafaka inayozalishwa nchini Kenya.
Wakaazi katika soko moja karibu na nyumbani kwake, wamesema kifo cha Rebecca ni pigo kwa jamii yao, kwa sababu wamekuwa wakimuona akifanya mazoezi yake kila siku katika barabara za mita yao.
Licha ya kupata ufanisi mkubwa kama mwanariadha, Maisha ya Rebecca, yalijawa na masaibu chungu nzumu.
Wanariadha wenzake, wamesema kuwa matokeo yake katika mashindano ya olimpiki yaliadhiriwa sana na mzozo ya kifamilia uliokuwa ukiendelea, kati yake na mpenzi wake wa zamani ulioanza mwaka uliopita.
‘ walikuwa wakishi Pamoja, lakini maisha yao yalianza Kwenda kombo mwaka uliopita kutokana na masuala ya kifedha’’ amesema ndugye Jacob Jeptegei.
Jacob anasema kuwa mpenzi wake, alikuwa amehoji, mahala dada yangu anakopeleka pes azote amnazo shinda katika mashindano ya riadha ya kimataifa. Lakini Rebecca alimuelexa kuwa fedha hizo n I mali yake na wale sio mali ya família. Aliongeza Jacob.
Polisi mjini Kitale wamesema kuwa wawili hao walikuwa wameripoti kesi kadhaa, katika vituo mbali mbali lakini walibadili misimamo yao ya kuondoa kesi hizo.
Huku familia ya Rebecca, ikisuburi haki, maandalizi ya mazishi ya mwanariadha huyo yanaendelea.
Familia yake sasa imethibitisha kuwa Rebecca atazikiwa tarehe 14 mwezi huu katika eneo LA Bukwo Mashariki mwa Uganda.
Rebecca ni mwariadha wa tatu kuuawa nchini Kenua katika kipindi cha miaka mkitatu iliyopita, matuki ambayo wapenzi wa wanariadha hao ndio washukiwa wakuu wa mauaji.
KUndi la kutetea haki za kibinadam ambalo lilianzishwa na wanariadha, nchini Kenya la Tirop’s Angels, limesema kuwa hali hii ni sharti ikomeshwe.
‘’ Ni jambo la kusitisha sana kwa mtoto yeyote kushuhudia mama yake akishambuliwa kwa moto’’ alisema Joan Jelimo ambaye ni mwanzilkisha wa shirika hili la Tirops Angels.
Dhuluma za kijinsi zimeongezeka sana hasa miongoni mwa wanariadha nchini Kenya, aliongeza mwanariadha mwingine Viola Cheptoo ambaye pia ni msimamizi wa shirika la Tirop’s Angels.