Hivi ni vyakula vinne bora kwa kuboresha kumbukumbu

Na Yusuph Mazimu, BBC Swahili

Memory

Chanzo cha picha, Getty Images

Usahaulifu ama kupoteza kumbukumbu ni tatizo linalokuwa kwa kasi miongoni mwa watu. Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO), kuna wagonjwa takriban milioni 50 wa kupoteza kumbukumbu kote ulimwenguni idadi hii ikitarajiwa kuongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2050.

WHO inasema mbali na kumuathiri mgonjwa mwenyewe, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unaathiri pia familia yake na unaongeza gharama za kiuchumi kwa jamii. Inatarjiwa kwamba ifikapo mwaka 2030 gharama hiyo itafikia dola trilioni 2 kwa mwaka.

Kwa mantiki hii ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote na kwa sababu hakuna tiba kwa sasa WHO inasisitiza umuhimu wa kuzuia kutokana na umuhimu wa kumbukumbu katika Maisha ya binadamu.

Aina za Kumbukumbu

Memory

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanasaikolojia Kimberley Wilson anasema ziko aina tatu za kupoteza kumbukumbu, za muda mfupi, ambapo uwezo wa mtu unamfanya kukumbuka mambo yaliyotokea muda mfupi uliopita. Kwa mfano mtu anakutajia namba ukaipiga bila kuiandika mahali.

Kumbukumbuku ya kazi, inayomfanya mtu kuelewa jambo na kuchangia mawazo kwenye mazungumzo yanayoendelea lakini kumbukumbu za muda mrefu ni zile zinazomfanya mtu kukumbuka matukio ya muda mrefu, hata miaka na miaka.

‘vile tunavyokula vinaathiri viwango vya kumbukumbu zetu zinavyofanya kazi’, anasema Kimberly.

Wazee ni waathirika wakubwa

Memory

Chanzo cha picha, Getty Images

Tatizo la kupoteza kumbukumbu linawakumbua kwa kiasi kikubwa watu wenye umri mkubwa.

‘Ni kweli watu wenue umri mkubwa hasa kuanzia miaka 70 wanapata tatizo hili pia, ingawa kwa wengine wenye umri mdogo wanaweza kulipata ila kwa uchache’, anasema Mwajombe Laurian kutoka Tanzania, mwalimu anayetoa elimu ya lishe kwa afya, ikiwemo kusaidia kumbukumbu.

WHO, Mwajombe aliyezungumza na BBC na hata mwanasaikolojia Kimberley wote wanasisitiza umuhimu wa kushughulikia tatizo hilo na njia iliyorahisi na kuthibitishwa ni kupitia vyakula.

Miongoni mwa vyakula vinavyoweza kukusaidia kwenye kumbukumbu ni hivi vifuatavyo

1. Zabibu za rangi ya zambarau

Memory

Chanzo cha picha, Getty Images

Ziko aina kadhaa za zabibu, ambazo maarufu ni zile zenye rangi ya kijani na za rangi ya zambarau. Watafiti wanathibitisha zabibu za zambarau zinamchango mkubwa kwenye kumbukumbu.

Kwa watu wazima wenye matatizo ya kumbukumbu wwakinywa nusu lita ya juice ya zabibu za rangi ya zambarau kila siku kwa muda wa wiki 12 (miezi mitatu) zitawasaidia.

Zabibu za zambarau zina kitu kinaitwa Anthocyanins na Polyphenols vinavyoipa rangi iliyokolezwa ambayo ni muhimu. Polyphenols pia inapatikana kwenye matunda mengine kama Apple na mapeasi.

Wakati wa mmengenyo wa vyakula hivi baada ya kuliwa vinasaidia kuifanya mishipa ya damu kunyumbulika vizuri na kutembea kwa damu kuelekea kwenye ubongo.

2. Blueberries

Brue berries

Chanzo cha picha, Getty Images

‘Watoto kula gram 240 (kama robo kilo) ya Blueberries wa kila siku zinawasaidia kukumbuka maneno mengi na kuyakumbuka kwa usahihi masaa mawili baadaye’, anasema Kimberley.

Kima ilivyo kwa zabibu za zambarau Blueberries pia zina kitu Anthocyanins na Polyphenols. Kama inavyofanya zabibu kwenye mishipa ya damu, Blueberries pia inaifanya mishipa ya damu kunyumbulika vizuri na kutembea kwa damu kuelekea kwenye ubongo. Hilo linasaidia kuleta nguvu zaidi, virutubishi na oksijeni.

3. Chocolate

chcolate

Chanzo cha picha, Getty Images

‘Taarifa njema kwa wapenda Chokleti, kwa sababu chokleti zina kakao ambayo inaboresha usambazaji wa damu kwenye akili, lakini inapaswa kuwa ‘dark chocolate’ ambayo ina asilimia 70% ya virutubishi vya kakao (Cocoa solids) ili kupata faida yake’, anasema Kimberley.

Lakini wataalamu wanasema muhimu kula mlo kamili wenye mboga za majani, matunda, protini kama samaki na maharage kwa sababu una faida kubwa kwenye ubongo wa mwanadamu.

4. Grean Tea

grean tea

Chanzo cha picha, Getty Images

Ukiacha kusaidia kukulinda na saratani, hatari ya kupata magonjwa ya moyo, unene pia inasaidia kuboresha afya ya akili.

Chai hii inafaida kubwa kwenye kumbukumbu. Hasa wenye tatizo la kumbukumbu za muda mfupi, grean tea, inaweza kuwasaidia sana.