Njia nne zinazoweza kukusaidia kuwa na kumbukumbu bora zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Usahaulifu au amnesia kwa lugha ya kitaalamu ni hali inayosababishwa na mtu kutokuwa na afya ambayo watu wengi huugua bila kujua.
Wakati mwingine hugeuka na kuwa ugonjwa unaofahamika kama "Dementia" na kuwa katika aina tofauti.
Professor Richard Restak, anayefundisha sayansi ya ubongo katika Chuo kikuu cha George Washington nchini Marekani, alisema kuwa sababu kubwa ya watu kusahau ni kutokana na kutomakinika au kufuatilia jambo vyema.
Restak, ambaye ni rais wa zamani wa chama cha madaktari wa ubongo nchini Marekani , aliandika makala katika gazeti la Guardian ambapo alisema kuwa kujizoweza kuwa na kukumbuka ni muhimu.
"Kwa mfano unapoenda kwenye sherehe. Iwapo utakuwa bado unafikiria mambo yanayohusiana na kazi na hausikilizi vyema anachoongea mtu anayezungumza na wewe , baadaye unabaini kuwa kwamba haukumbuki jina la mtu yule uliyekuwa ukiongea naye ." Kwanza unakariri taarifa. Lakini kama hautakariri jina, taarifa haitabaki akilini mwako."

Chanzo cha picha, Getty Images
Alisema kuwa yeyote anaweza kukumbuka kwa urahisi mambo ambayo ameyakariri kwa kuyapatia kipaumbele.
Mikakati ya kuimarisha kumbukumbu
Restak anasema kuwa juhusu zinapaswa kufanyika kuboresha kumbukumbu, kwa kuzingatia mambo kadhaa ambayo yanaweza kuimarisha akili na kumbukumbu
ushauri wake unajumuisha:
Epuka vilevi
Vilevi sio vizuri kwa afya ya ubongo, kulingana na hili, profesa anasema chochote kinaweza kuingilia moja kwa moja utendaji kazi wa ubongo au kusababisha kupoteza fahamu. Kitu chochote kinachoweza kusababisha kupote kwa fahamu kinapaswa kuepuka, ili kuweza kuimarisha kumbukumbu ya ubongo wako.
Lala usingizi wa kutosha
Kupata usingizi wa kutosha husaidia ubongo wako kufanya kwazi kwa ubora zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulala kwa muda mfupi wakati wa mchana kila siku, husaidia sana kuboresha kumbukumbu ."Akina mama waliojifungua na wajawazito hulalamikia kutokuwa na kumbukumbu nzuri , kutokana na kuwa macho kwa muda mrefu, jambo linaloathiri utendaji bora wa ubongo ," anasema Restak.
Kipaumbele cha kumbukumbu
Matatizo ya kuona na kusikua yanapaswa kutafutiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo, na kupoteza kumbukumbu ni mambo ambayo hayapaswi kuchukuliwa kwa uzito mdogo.
Kuchangamana na watu katika jamii
Kuwa mtu mwenye kuchangamana na watu katiia jamii, kuepuka upweke na mawazo vinaweza kusaidia kwa kiasi fulani katika kuimarisha kumbukumbu yako.
Lakini, Restak anasema kwamba kwa kufanya haya yote sio hakikisho kwamba unaweza kuwa na kumbukumbu nzuri ."Hakuna yeyote anayeweza kukuahidi kwamba utakapofuata ushauri huu utapata matokeo sahihi, lakini anasema kufuata ushauri huu kunaweza kupunguza hatari ya kupoteza kabisa kumbukumbu yako ," asema.















