Aliyekuwa mfanya usafi sasa ni Makamu wa rais wa Colombia

Kinachokuja hapa ni mabadiliko halisi, mabadiliko halisi ," Rais mpya wa Colombia, Gustavo Petro, aliwaahidi wafuasi wake waliokuwa wakimshangilia wakati alipokuwa akitoa hotuba ya ushindi Jumapili usiku.

Akiwa ndiye kiongozi wa kwanza wa mrengo wa kushito kuwahi kuchaguliwa- na mgombea mwenza, Francia Márquez, ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais -Bw Petro anaamini kuwa Colombia imepiga kura ya mabadiliko na ni vigumu kupinga hilo.

Kikundi hicho kilishika silaha dhidi ya kile kilichoonekana kama ukosefu wa usawa na katika mwaka 1985 kilifanya mashambulizi katika kasri ya sheria mjini Bogotá, kwa lengo lililoelezewa la kumshtaki aliyekuwa rais wa nchi hiyo.

Serikali iliwatuma wanajeshi na vita vya umwagaji damu vilifuatia ambapo watu karibu 100 waliuawa.

Bw Petro alijiunga na kikundi hicho wakati alipokuwa na umri wa miaka 17 na alikuwa mjumbe wake kwa miaka 10.

Alifungwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kwasababu ya kuhusika nao, na alizungumzia kuhusu jinsi alivyoteswa na maafisa wakati alipokuwa gerezani.

Mbele na kati ya kampeni za Gustavo Petro amekuwa Bi Francia Márquez, mgombea mwenza wa kiti cha Makamu. Bi Márquez, ambaye ni Mcolombia mwenye asili ya weusi ambaye alikuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa usafi, atakuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo.

Mwanakampeni thabiti ameweza kuwa mfano ambao umewatia moyo Wacolombia wengi kwa jinsi alivyopanda kutoka kuwa masikini hadi kuwa Makamu wa rais,hadithi ya nadra katika nchi ambayo kazi ya siasa limekuwa ndio chaguo la watu wengi wenye uhusiano na wenye nacho.

Bi Márquez alikuwa tayari ni mwanamazingira anayefahamika vyema nchini Colombia. Mnamo mwaka 2014,aliongoza kampeni dhidi ya uchimbaji haramu wa madini katika jamii ya La Toma,ambako alikulia.

Aliongoza kundi la wanawake 80 katika matembezi ya kilomita 560 (maili 350) kutoka Bogotá, kuiwekea serikali shinikizo ichukue hatua.

Kikosi kazi, kiliundwa na serikali mwaka 2015, kilisaidia kumaliza uchimbaji haramu wa madini, huku Bi Márquez akishinda tuzo kwa kazi yake.

Haiba yake na maisha yake ya awali vilimsaidia Bi Márquez kuwasiliana na baadhi ya makundi mengi ya nchi hiyo ya watu waliosahaulika kimaendeleo, ikiwemo jamii ya Wacolombia wenye asili ya Afrika, jamii anayotoka yeye.

"Alimsaidia Gustavo Petro kufikia sekta za nchi ambazo zilihisi kutengwa na siasa na jamii kwasababu ya ubaguzi wa rangi na kutengwa," alisema Bw Fajardo.

Bw Petro na Bi Márquez wanakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwa ni pamoja na bunge la congress lililogawanyika na wafanyabiashara wasomi ambao baadhi yao hawana imani na sera zao.

Lakini kwa sasa, wafuasi wao watahisi kwamba mabadiliko halisi yako njiani kuwafikia.