Uchaguzi wa Marekani 2024: Je, Harris anaweza kumshinda Trump ikiwa Biden atajiondoa?

sdx

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Courtney Subramanian
    • Nafasi, BBC

Wafuasi wa chama cha Democratic wana hofu, wakitaka Joe Biden mwenye umri wa miaka 81, ajiondoe katika uchaguzi wa Novemba kufuatia utendaji mbovu katika mdahalo dhidi ya Donald Trump.

Idadi ya wanahabari wanaomfuata Kamala Harris, Makamu wa Rais katika ziara zake inazidi kuongezeka na kufikia dazeni.

Akiwa jukwaani siku ya Jumapili katika tamasha la utamaduni wa watu weusi, huko New Orleans, makamu wa rais hakujibu maswali ya iwapo Biden anapaswa kujiondoa na kumkabidhi kijiti.

Tangu mdahalo mbaya kwa Biden, kupitia CNN tarehe 27 Juni, amekuwa akimtetea bosi wake mara kwa mara, akisema kuwa rekodi yake kama rais haipaswi kufunikwa na dakika 90 kwenye jukwaa la mdahalo. Biden mwenyewe amekuwa mbishi na kusisitiza atasalia kuwa mgombea.

Huku wito ukiongezeka kwa rais kujiuzulu, baadhi ya wafuasi wa ngazi ya juu wa chama chake, wanamuunga mkono Harris mwenye umri wa miaka 59 kuwa mgombea na kuchukua nafasi ya Biden.

Siku ya Jumapili, Mbunge Adam Schiff wa California aliliambia jarida la Meet the Press la NBC kwamba, ima Biden awe na uwezo wa "kushinda kwa wingi au amwachie mgombea mwingine. Aliongeza kwa kusema, “Kamala Harris anaweza kushinda kwa kishindo dhidi ya Trump.”

Hilo ni pendekezo ambalo limezua taharuki miongoni mwa wanachama, wakiwemo washirika wa Biden, ambao wanamwona Harris hafai kwani alishindwa katika mpango wake wa uteuzi wa chama 2020, hata kabla ya kura ya kwanza kupigwa na amekuwa na rekodi ya chini ya kukubalika katika muda wake wote akiwa katika Ikulu ya White House.

Hata hivyo, wabunge maarufu wa chama cha Democratic kama Schiff na Mbunge wa Jimbo la South Carolina, Jim Clyburn wamekuwa wakimwelezea Harris kama mrithi aliye wazi iwapo Biden atakubali shinikizo la chama la kujiuzulu.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wapo wanaopendekeza kwamba anaweza kufanya vyema zaidi kuliko rais katika mdahalo dhidi ya Donald Trump, na wanasema kuwa ana wasifu mzuri kitaifa, katika upigaji kampeni na kuungwa mkono na wapiga kura chipukizi.

Jamal Simmons, mwanamikakati wa muda mrefu wa Democratic na mkurugenzi wa zamani wa mawasiliano wa Harris, anasema Hariss amepuuzwa kwa muda mrefu.

Tangu mdahalo na mtafaruku wake, Harris amebadilisha ratiba yake ili kushikamana na rais. Alionekana kwenye mkutano uliofuatiliwa sana Jumatano iliyopita ambapo Biden alitaka kuwahakikishia magavana wenye nguvu kuhusu kufaa kwake kushika wadhifa huo.

Na siku moja baadaye, tarehe 4, Julai - Siku ya Uhuru wa Marekani - aliacha utamaduni wake wa kufanya tafrija na maafisa wa zima moto na maafisa wa Secret Service nyumbani kwake Los Angeles, ili kuwa karibu na Biden kwenye sherehe za White House.

Harris, mwendesha mashtaka mkuu wa zamani amemkosoa Trump hadharani tangu mjadala huo, akisisitiza kwa wapiga kura kuwa wanapaswa kujua Trump ni tishio kwa demokrasia na haki za wanawake.

Pia unaweza kusoma
zx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya vigogo wa chama cha Democratic wanamuunga mkono Kamala Harris iwapo Joe Biden atajiuzulu

Kamala Harris, hata hivyo, sio mtu pekee anayejadiliwa kumrithi Biden. Kuna orodha ya magavana maarufu - Gretchen Whitmer wa Michigan, Gavin Newsom wa California, Josh Shapiro wa Pennsylvania na JB Pritzker wa Illinois - hadi Waziri wa Uchukuzi Pete Buttigieg na Mbunge wa California Ro Khanna.

Harris na wafanyakazi wake wamekataa kujihusisha na uvumi. Lakini timu yake inafahamu vyema mazungumzo ya nyuma ya pazia yanayofanyika huku baadhi ya wanachama wakimuunga mkono.

Taarifa iliyosambazwa mtandaoni, inayodaiwa kuandikwa na watendaji wa chama cha Democratic, ilitoa hoja ya kumuunga mkono Bi Harris licha ya "udhaifu wake wa kisiasa."

“Kujaribu kuchagua mtu mwingine na kumuacha yeye kunaweza kusababisha mkanganyiko wa kampeni na mabishano katika vyombo vya habari kwa miezi kadhaa,” inasema taarifa hiyo.

Anaweza kumshinda Trump?

sazx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuwa na ushawishi mdogo kama makamu wa rais unaleta wasiwasi kwa Democratic kama anaweza kumshinda Donald Trump.

Lakini swali pekee muhimu kwa Wana-demokratic wengi - ikiwa ni pamoja na wafadhili wenye fedha nyingi - ni ikiwa ana nafasi nzuri ya kumshinda Trump kuliko Joe Biden. Na hilo halina uhakika kabisa.

Wafuasi wa Harris wanagusia kura ya maoni ya hivi karibuni ya CNN iliyopendekeza, atafanya vyema kuliko rais dhidi ya Trump mwezi Novemba.

Katika kinyang'anyiro cha ana kwa ana, kura hiyo inaonyesha Harris alimfuata Trump kwa pointi mbili nyuma, huku Biden akisalia kwa pointi sita nyuma yake.

Kura hiyo pia ilipendekeza Harris alifanya vyema zaidi kuliko Biden miongoni mwa wapiga kura huru na wanawake.

Wataalam wengi, wanapuuzilia mbali tafiti zinazo muweka chini Harris, wakisema hisia za wapiga kura zitabadilika ikiwa Biden ataamua kujiondoa na Democratic kumkaribisha mgombea mwingine.

Mtafiti mmoja wa chama cha Democratic aliye karibu na kampeni ya Biden alikiri kwamba Bi Harris anaweza kuwa na uwezo zaidi wa kupanua ushawishi kwa wapiga kura wa chama kuliko rais.

Tafiti zinazomuweka chini dhidi ya Trump katika hatua hii "hazina maana yoyote," alisema mtu huyo, ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa sababu hawakuidhinishwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Bi Harris, mtoto wa mama wa Kihindi na baba wa Jamaika, anafanya vyema zaidi katika tafiti kuliko Biden kwa wapiga kura weusi, Walatino na vijana - hayo ni makundi muhimu katika uchaguzi.

Iwapo ataweza kuongeza idadi ya wapiga kura vijana, hilo ni swali lingine lisilo na uhakika. "Huu ni wakati wa kungoja tu na kuona," mchaguzi alisema.

as

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kamala Harris akiwa katika mdahalo na Makamu wa zamani wa Trump, Mike Pence wakati wa uchaguzi wa rais wa 2020 baada ya Joe Biden kumfanya mgombea mwenza wake.

Iwapo atachukua nafasi hiyo, baadhi ya Wana-democratic wamependekeza kwamba Gavana Josh Shapiro wa Pennsylvania au Gavana Roy Cooper wa North Carolina wanaweza kuchaguliwa kama mgombea mwenza ili kupata wapiga kura walio na msimamo wa wastani katika majimbo ya Katikati Magharibi.

Katika kampeni, ameunga mkono masuala mengine yanawahusu wapiga kura vijana, ikiwa ni pamoja na msamaha wa madeni ya wanafunzi, mabadiliko ya hali ya hewa na kudhibiti bunduki.

Bado, anakabiliwa na changamoto kubwa ya kubadilisha mashaka ya muda mrefu ya wapigakura, ikiwa Biden mwenyewe atakubali shinikizo la chama linaloongezeka la kujiuzulu.

Katika tamasha la Essence huko New Orleans, Iam Christian Tucker, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 41 kutoka New Orleans, alisema hajali, ni nani atakayeteuliwa.

Alisema anampenda Kamala Harris, lakini hana uhakika kama rais mwanamke-mweusi ataweza kushinda uchaguzi.

"Ninapiga kura dhidi ya Donald Trump," aliiambia BBC.

Greg Hovel, 67, aliyehudhuria mkutano wa hadhara wa Rais Biden huko Madison, Wisconsin, wiki iliyopita, alisema alimuunga mkono Harris katika mchujo wa 2020 na "bado anamuunga mkono.”

"Nadhani atakuwa rais bora," Hovel alisema. "Ingawa bado nadhani Biden anaweza kushinda."

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Yusuf Jumah