Mambo matano ya kuzingatia unapotumia bidhaa za urembo za kuzuia uzee

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika miongo ya hivi, shinikizo la kutaka kuwa uso usio na mikunyanzi na dalili zingine za kuzeeka limeongezeka: asidi ya hyaluronic, dutu ambayo inaweza kutumika kwa sehemu za ndani za ngozi ili kukuza unyevu, kunyoosha ngozi kuupatia uso muonekano unaohitajika hasa kwenye kidevu. mashavu, midomo na kope.
Bidhaa maarufu ya "kuhuisha ngozi ya uso" imekuw akinadiwa kama krimu ya urembo na matangazo ya kliniki ya urembo.
Lakini je inaweza kutumiwa na kila mtu? Je kuna madhara yanayotokana na utumizi wa bidhaa hii ya urembo? Na je kuna tofauti gani kati ya krimu zinazouzwa madukani na sindano zinazotolewa na madaktari?
Kwa kujibu maswali haya matano tunaelezea ni changamoto zinazohusiana bidhaa hii.
1. Asidi ya hyaluronic ni nini?
Hyaluronic acid ni dutu inayotengenezwa na miili yetu yenyewe na ya baadhi ya wanyama.
Ina kazi ya kudumisha unyevu wa asili wa seli zinazounda tabaka za ndani za ngozi, na pia kusaidia na kujaza tishu hii.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kwa miaka mingi kutokana na mchakato wa kuzeeka, tunapoteza ngozi ya ziada, ambayo inakuwa nyembamba na huru," anaelezea daktari Alessandra Grassi Salles, mratibu wa Kikundi cha Upasuaji wa Urembo, Vipodozi na Laser katika idara ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Sao Paulo (USP), nchini Brazil.
Hii "ngozi ya ziada" iliyotajwa na mtaalamu inalingana kwa usahihi na vitu vyote "hujaza" ngozi na kushikilia seli za ngozi pamoja.
Kadri miaka inavyosonga na kupngua kwa asili ya asidi hii muhmu inayotolewa na mwili, ni kawaida kwa sehemu ya juu ya mwili wetu kulegea, kupata makunyanzi na mwishowe kuwa nyembamba.
Kwa kupita kwa miaka na kupungua kwa asili kwa misombo hii, ni kawaida kwa safu ya juu ya mwili wetu kuwa dhaifu, kupata makunyanzi na mwishowe kuwa nyembamba.
Hapa ndipo kuna haja ya kupaka asidi ya hyaluronic: lengo ni kuhuisha mwili na kuongeza kiwango dutu hii, ili kuweka ngozi katika hali inayohitajika.
2. Kuna tofauti gani kati ya krimu na sindano?
"Tatizo kubwa la asidi ya hyaluronic ambayo inatolewa na mwili haidumu kwa muda mrefu. Mwili huifyonza kwa chini ya saa 48," anasema Dkt. Daniel Boro, wa Jumuiya ya Upasuaji wa Umbo nchini Brazil.
"Sekta hiyo ilitengeneza aina nyingine ya dutu hii ambayo ni sugu zaidi na iliyo na uwezo wa kubaki kwenye mwili kwa miezi."

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa sasa, asidi ya hyaluronic hudungwa katika taratibu unaofahamika kama aesthetic ambayo hupatikana kupitia njia ya usindikaji wa baadhi ya viumbe vinavyoweza kuonekana tu kupitia darubini.
Krimu huwa na toleo la synthetic ya kiungo hiki. Jinsi uso wako unavyozeeka na umri kuongezeka ndivyo unavyopata (makunyanzi zaidi).
Mbali na ujenzi, aina mbili za bidhaa zina tofauti za kimsingi katika utaratibu wa utendaji.
"Kazi ya msingi ya krimu ni kukuza unyevu wa juu sana wa ngozi. Sindano zina kazi ya kujaza, kusaidia na uso kung'aa," anasema Dkt. Alessandra Ribeiro Romiti, mshauri wa Idara ya Vipodozi vya mwili kutoka Jumuiya ya Brazil ya masuala ya ngozi.
Wataalamu wanaelezea kuwa krimu hutoa molekuli kubwa ambazo haziwezi kupitia sehemu ya kwanza za ngozi.
Kwa hili, hakuna uwezekano kwamba asidi ya hyaluronic ambayo ni sehemu ya uundaji inazidi na kujaza matrix ya ziada ya seli iliyotajwa hapo juu.
Athari sawa ya unyevu, kwa njia, huzingatiwa katika vidonge ambavyo pia vina kiungo hiki.
Hata hivyo, kabla ya kuanza kutumia yoyote ya vipengele hivi, ni bora kutafuta mwongozo wa mtaalam.
"Iwapo mtu huyo ana ngozi ya mafuta na anatumia cream nyingi, kuna hatari ya tabia hii kuziba vinyweleo vya ngozi na kusababisha chunusi," anaeleza Salles.
3. Asidi ya hyaluronic inafaa kutumiwa na nani?
Kwa ujumla, hakuna mapendekezo ambayo yanafaa watu wote.
"Tunaweza kupaka asidi ya hyaluronic mwilini kama sehemu ya kudhibiti mchakato wa ngozi kuzeeka," anasema Boro.
Kulingana na Romiti, kila kitu kitategemea kile mgonjwa anachotafuta na sifa zake za kibinafsi.
"Hakuna umri sahihi wa kuanza matibabu. Kuna watu Salles anaongeza kuwa, pamoja na uwezekano wa kurekebisha vipengele fulani vya uso kupitia teknolojia mpya za urembo kama vile asidi ya hyaluronic, mtaalamu wa afya anahitaji kuelewa msukumu wa kila mtu.
"Ni kosa kubwa kufikiria kuwa tunahitaji kuwa na uso wa miaka 30 ili kuwa na furaha. Tusipogundua kinachoendelea kwa mgonjwa anaweza kuwa na sura mpya, lakini hataridhika kikamilifu," anasema
4. Je matokeo ya baada ya kupaka ni ya mwisho?
La. Asidi ya Hyaluronic inayotumiwa katika utaratibu huu hudumu kwa muda mrefu, na inafyonzwa mwilini pole pole. "Yote inategemea aina ya gel na itapakwa sehemu gani ya uso," Boro anajibu.
"Kwa ujumla, hukaa kwenye tabaka za ngozi kwa muda wa mwaka mmoja, lakini wakati huu kwa kawaida hutofautiana kati ya miezi sita na 18."
Inafaa kufafanua hapa kuwa sio asidi yote ya hyaluronic ni sawa: kuna uundaji thabiti zaidi na zingine ambazo zinaweza kuharibika zaidi.
Wataalamu wanachagua aina inayofaa kulingana na sehemu ya uso na matokeo yanayorajiwa.
Kwa kidevu au taya, kwa mfano, jeli maaluma inaweza kuwa muhimu, wakati juu ya midomo au kope, ni bora kutumia bidhaa rahisi na, ambayo itawawezesha harakati zaidi ya asili ya kinywa au macho.
Mbali na uthabiti, sababu nyingine inayoingilia muda wa asidi ya hyaluronic ni harakati ya miundo ya uso.
Huelekea kwenda haraka katika sehemu zinazosonga sana, kama vile midomo na macho, na hukaa kwa muda mrefu katika sehemu ambazo hazisogei, kama kidevu.
Lakini bila shaka, wataalam hawasubiri hadi asidi ya hyaluronic imechoka kabisa ili kuonyesha maombi mapya.
"Tunafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na tuna itifaki za kufanya mabadiliko, kama inavyohitajika," anasema Bor
5. Je kuna hatari ya kupata madhara baada ya kufanya utaratibu huu?
Athari mbaya zinaweza kutokea na ni muhimu kwamba wataalamu na wagonjwa wajue jinsi ya kuzitambua ili kuchukua hatua haraka na kuwa na uharibifu.
Mojawapo ya hatari inayoogopa zaidi hutokea wakati bidhaa inapoingizwa kwenye sehemu isiyofaa ya uso.
Kwa hili, asidi ya hyaluronic inaweza kukwama kwenye mishipa ya damu inayosaidia uso, hali ambayo itasababisha kufa kwa tishu katika sehemu za pua, midomo au hata upofu.
"Ili kupunguza hatari hii, ni muhimu kufanya utaratibu huu na wataalamu ambao wana uzoefu mkubwa," anasema Salles.
"Hili sio jambo unalojifunza katika kozi ya mwishoni mwa wiki. Inachukua miaka ya kujifunza kuelewa tofauti zote za anatomia ya uso. Na hata wataalamu wenye ujuzi zaidi wanaweza kufanya makosa".
Ili kupunguza uharibifu, inawezekana kutumia enzyme inayoitwa hyaluronidase, ambayo ina kazi ya kunyonya asidi ya hyaluronic iliyotumiwa vibaya.















