Je ni aina gani za upasuaji wa urembo unazozifahamu miongoni mwa wanaume ?

Moja ya upasuaiji wa urembo unaofanywa sana na wanaume nchini Marekani ni upausiaji wa kuondoa mafuta

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Moja ya upasuaiji wa urembo unaofanywa sana na wanaume nchini Marekani ni upausiaji wa kuondoa mafuta

Shinikizo la kutaka kuwa na muonekano mzuri ni kubwa kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake wengi wakiishia kufanyiwa upasuaji wa urembo ili kulifikia hilo.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika moja la wataalamu Uingereza wanaofanikisha urembo huo kwa wanaume.

Idadi ya wanaume wanaotafuta urembo kupitia njia za upasuaji inaongezeka na wataalamu wanasema ni jambo la kawaida maana ni mtindo unaoshudiwa kote duniani.

Nchini Kenya kwa mfano hamu ya kuwa na umbo dogo la mwili, rangi nyeupe ya ngozi au tabasamu la kuvutia ni jambo la kawaida kutokana na idadi ya wateja wanaotembelea kliniki za urembo huo mfano madaktari wa meno kusafisha au kuchubua rangi ya meno yatakate zaidi.

aNa dhamira ni sawa kwa wote, sio tu Kenya lakini hata katika maenoe mengine Afrika, wanaume hutafuta urembo huo kupata muonekano mzuri na kuvutia zaidi.

Kuna wanaopendelea kubadilisha umbo lao, kuvutia wapenzi wapya, au kumtia gere mpenzi ulioachana naye.

Wengine ni kuiga mifano ya maisha ya nyota wa mataifa ya magharibi, kuiga mitindo na huenda likachukuliwa kuwa jambo lisilo na maana lakini kwa wateja kuna sababu kuu ya mtu kuamua kupitia kisu cha mpasuaji.

Na urembo huu huwafanya baadhi hata kusafiri kwenda nchi za nje kama Ulaya na hata bara Asia kufanyiwa upasuaji.

Katika utafiti wa BBC uliohusisha wanaume 2,000 na wanawake, waliulizwa ni sehemu ipi ya mwili waliopenda kuibadili - 34% ya wanaume wengi walisema tumbo lao na kifua.

Diren Kartel mkufunzi binafsi wa mazoezi ya mwili anasema hashangazwi na chaguo hilo kwa wanaume.

"Hata mimi nilipoanza kufanya mazoezi nilitaka kuwa na msuli tumboni uliokazana. Nilipokuwa kijana nilitaka kuwa na tumbo gumu lenye msuli, ndilo jambo ambalo kila mwanamume angependa kuwa nalo.."

Kufikia mwaka 2016, karibu watu 10 waliotaka kufanyiwa upasuaji wa urembo nchini Marekani walikua wanaume (9.3%), kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni kutoka Chama cha Upasuaji wa Urembo nchini Marekani.

Nchini Uhispania, takwimu ya upasuaji wa urembo kwa wanaume ni karibu asilimia 12.2% kwa ujumla.

Huko Uingereza mwaka 2016 asilimia nane ya wanaume walifanyiwa upasuaji wa urembo, ijapokuwa kiwango cha upasuaji wa aina hiyo kilishuka kwa wanaume na mwaka 2016 baada ya kupanda mwaka 2015, kulingana na data kutoka Chama cha Wafanya Upasuaji wa Urembo nchini Uingereza.(BAAPS).

Upasuaji unaopendwa sana na wanaume ni upi?

Kulingana na wataalamu wa upasuaji wa urembo kuna aina sita ya upasuaji unaowavutia wanaume:

  • 1. Liposuction upasuaji wa kuondoa mafuta (Asilimia 24 ya upasuaji huu hufanyiwa wanaume )
  • 2. Kupunguza ukubwa wa matiti - kutibu gynecomastia (17%)
  • 3. Upasuaji wa kope (15%)
  • 4. Upasuaji wa pua (14%)
  • 5. kuondoa mikunjo usoni (7%)
  • 6. Upasuaji wa masikio(5%)

Katika chi zingine kama, Uhispania na Uingereza, upasuaji wa aina hii hufanyiwa wanaume, ingawa kuna tofauti kidogo katika katika mpangilio maalum.

Kuongezeka kwa mtindo huo

Kwa mujibu wa Dkt. Ainhoa Placer Lainez, mtaalamu wa upasuaji wa urembo, kiwango cha upasuaji wa aina hiyo kimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa mtazamo wake, mtindo huo huenda ukaongezeka zaidi siku zijazo.

"Naamini wanaume wana unyenyekevu kidogo linapokuja suala kushauriana kuhusu urembo au kufanyiwa mataibabu yoyote au upasuaji" alisemaka Dkt Placer.

Kupungiza ukubwa wa matiti

Kupunguza ukubwa wa matiti ni moja ya upasuaji wa urembo unaopendwa miongoni mwa wanaume.

Mwaka 2016 ulikuwa nambari mbili nchini Marekani na ya nne nchini Uhispania

Ayo Adesina alikuwa na matati makubwa alipokuwa mtoto

Chanzo cha picha, AYO ADESINA

Maelezo ya picha, Ayo Adesina alikuwa na matati makubwa alipokuwa mtoto

Upasuaji wa aina hii hufanywa kutibu ugonjwa wa gynecomastia, hali ya kukua kwa titi moja au au yote mawili kwanza wanaume.

Gynecomastia mara nyingi hutokana na unene kupita kiasi au homoni kutofanya kazi kwa usawa kutokana na mabadiliko ya asili ya homoni.

Baadhi ya magonjwa hutibiwa kwa kutumia steroids, ambazo huwa na athari kwa mwili kutokana na tibia za aina fulani kama vile saratani

Asilimia saba ya upasuaji wa aina hiyo mwaka 2016 ulihusisha vijana walio na umri wa chini ya miaka 19.

Kulingana na Dkt. Placer Lainez, upasuaji wa kupunguza ukubwa wa matiti kwa wanaume (gynecomastia)unaweza kufanyiwa watu wa rika zote, lakini pia unaweza kufanyiwa watoto wadogo kwa idhini ya wazazi.

"Hii inafanyika wakati mgonjwa ameathiriwa vibaya katika jamii kutokana kutojiamini," alielezea mpasuaji huyo.

Hata hivyo upasuaji wa urembo uliofanywa zaidi , kwa wanawake na wanaume ni liposuction.