Unajua matope yanaimarisha kinga yako ya mwili?

Mud

Chanzo cha picha, Getty Images

Kawaida watoto wanapenda kujichafua. Wanavutiwa na madimbwi yenye matope, bila kujali wana viatu ama hawana viatu au rangi ya mavazi yao. Lakini kujichafua kunaweza kuwa na athari kubwa kwa ustawi wao pia.

"Usijichafuke!" kwa hapo zamani kujichafua kuliwachukiza mara kwa mara familia, huku wazazi wakichukizwa kuona watoto wao wakichafua nguo zao nzuri.

Iwe walikuwa wakikimbia katika mashamba, kupanda miti au kukamata viluwiluwi, ilikuwa ni lazima kwamba nguzo za watoto hao zingegeuka rangi ya kahawia kabla ya siku kuisha.

Leo, wazazi wengi wanaweza kutamani kwa siri kwamba watoto wao wapate nafasi ya kuvumilia hali fulani mbaya. Pamoja na kuongezeka kwa maendeleo mijini na kuongezeka kwa michezo ya video na mitandao ya kijamii, kuwa karibu na asili ni nadra sana kwa sasa kuliko siku za nyuma. Kwa wengi, hakuna tena fursa ya kujichafua na matope.

Hofu ya bili kubwa kutokana na kufua uchafu kinaweza kuwa sio kitu katika ustawi wa mtoto. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi majuzi, uchafu wa nje unashirikiana na vijidudu rafiki ambavyo vinaweza kuelekeza mfumo wa kinga na kujenga uwezo wa kukabiliana na magonjwa anuwai, pamoja na mzio, pumu na hata uchovu na wasiwasi.

Matokeo haya yanaonyesha kuwa mazoezi ya nje sio tu yana manufaa kwa sababu ya nafasi ya kufanyika bila malipo - lakini uwepo wa nyenzo fulani za asili, kama vile udongo na matope, pia zina vijidudu vyenye nguvu ya kushangaza ambavyo tunaanza kuelewa kikamilifu athari zao chanya kwa afya ya watoto.

Kuboresha akili

Mud

Chanzo cha picha, Getty Images

Faida nyingi za kisaikolojia za kucheza nje tayari zimeonyeshwa vizuri. Ubongo wetu ulibadilika katika mandhari ya asili, na mifumo yetu ya utambuzi inafaa haswa tukiwa sehemu za nje, mfano za mwituni.

Hii ina maana kwamba matukio ya asili hutoa kiwango kamili cha kusisimua, ambacho hufikiriwa kusaidia kuchaji ubongo wakati umechoka na unaweza kuvurugika kwa urahisi.

Ikiunga mkono nadharia hii, utafiti mmoja wa mwaka wa 2009 uligundua kuwa watoto walio na ugonjwa wa kuhangaikia-deficit hyperactivity (ADHD) waliweza kuzingatia vyema kufuatia kutembea kwa dakika 20 katika bustani, ikilinganishwa na kutembea kwa dakika 20 kwenye mitaa ya barabara iliyohifadhiwa vizuri katika eneo la mjini.

Kuwa karibu na nyasi na miti kulionekana kuwa na matokeo yenye manufaa kwenye akili zao. Waandishi walipendekeza kutumia "dozi za asili" kama njia salama na inayoweza kufikiwa ya kusaidia watoto walio na ADHD, pamoja na zana zingine. Kando na athari hizi za uboreshaji akili, watoto kucheza nje kunaweza kutoa uzoefu muhimu wa kujifunza.

Mud

Chanzo cha picha, Getty Images

Linapokuja suala la afya ya kimwili ya mtoto, faida ya wazi inayonekana zaidi kwa mtoto anayecheza nje inaweza kuwa ni mazoezi. Mtoto anaweza kupata urahisi wa kujenga nguvu na stamina katika eneo kubwa la wazi na hivyo kusababisha kupunguza hatari ya kunenepa kupita kiasi, kulingana na utafiti mmoja ulioongozwa na Elizabeth Gershoff, profesa wa maendeleo ya binadamu na sayansi ya familia katika Chuo Kikuu cha Texas huko Austin, Marekani.

Matokeo ya hivi punde, hata hivyo, yanapendekeza kwamba kunaweza kuwa na faida nyingi za kucheza katika mazingira asilia - na siri inaweza kuwa hai na inazunguka-zunguka kwenye matope yenyewe.

Mud

Chanzo cha picha, Getty Images

Nadharia ya usafi

Mud

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti mpya unatoa maoni mapya juu ya "nadharia ya usafi", iliyopendekezwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa miaka ya 1980.

Kulingana na wazo hili, upunguzaji mkubwa wa maambukizo ya utotoni katika Karne ya 20 ulikuwa na athari isiyofaa kwa mifumo ya kinga ya watu, na hivyo kusababisha kuongezeka kwa pumu, homa na mizio ya chakula.

Wanasayansi wengi sasa hawapendi neno nadharia ya usafi, hata hivyo, kwa kuwa ilionekana kukatisha tamaa tabia muhimu kama kunawa mikono. Na wanapinga wazo kwamba maambukizo, kwa kila mtu, yana faida kwa watoto.

Watu wanaokulia mashambani kwa ujumla wana uwezekano mdogo wa kupata pumu, mizio, au matatizo ya kinga-kama ugonjwa wa Crohn kutokana na kushiriki kwenye asili ikiwemo uchafu wa matope na kuboreesha mfumo wa kinga.

Mwili wenye afya, akili yenye afya

Mud

Chanzo cha picha, Getty Images

Tunapohisi hatari na kutishiwa, mfumo wa kinga huanza kuinua mwili wetu kuvimba. Kwa kuwa kuvimba ni mojawapo ya njia za kwanza za ulinzi dhidi ya maambukizi, jibu hili liliibuka kama njia ya kuutayarisha mwili kwa ajili ya jeraha linaloweza kutokea kutokana na tishio ambalo tulikuwa tukikabili - lakini halifai kwa aina za mifadhaiko ambayo watu wengi hukabili leo.

Watafiti wanapendekeza zaidi kwamba matibabu mengi ya spa - ikiwa ni pamoja na bafu la matope na bafu ya maji ya madini - inaweza kuboresha afya yetu kwa kuanzisha viumbe vyenye manufaa kwa ngozi.