Tetesi Ulaya Jumamosi: Rodrygo atakiwa Arsenal, Morgan, Nwaneri Chelsea

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Winga wa Brazil Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, anataka kuondoka Real Madrid akifuatiliwa na vilabu vya Arsenal, Manchester City na Liverpool. (AS – Spain)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili Carlos Baleba, kiungo wa Brighton mwenye miaka 21, lakini wanaweza kusubiri hadi majira ya kiangazi kabla ya kuwasilisha ofa rasmi kwa kiungo huyo raia wa Cameroon. (Sky Sports)

West Ham United wako kwenye mazungumzo ya kumsajili Taty Castellanos, mshambuliaji wa Lazio na Argentina mwenye miaka 27, kwa ada ya pauni milioni 25.(Daily Mail)

Beki wa kati pia ni kipaumbele kwa West Ham, ambao bado wana nia ya kumsajili Charlie Cresswell, beki wa Toulouse mwenye miaka 23 ambaye amewahi kuichezea timu ya vijana ya England chini ya miaka 21. (The Guardian)

Liverpool, Manchester United na Newcastle United wote wanaendelea kumfuatilia kwa karibu Othmane Maamma, mshambuliaji wa Watford na timu ya vijana ya Morocco chini ya miaka 20. (TeamTalk)

Chelsea wanapanga kusajili Morgan Rogers, kiungo wa Aston Villa na England mwenye miaka 23, pamoja na Ethan Nwaneri, kiungo mshambuliaji chipukizi wa Arsenal mwenye miaka 18. (CaughtOffside)

S

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wamewasiliana na West Ham kuulizia upatikanaji wa Guido Rodriguez, kiungo wa Argentina mwenye miaka 31, huku wakiendelea kutathmini nyota wengine katika dirisha la usajili la majira ya baridi. (La Gazzetta dello Sport)

Crystal Palace, Leeds United na Nottingham Forest wanapambana kumsajili Joe Willock, kiungo wa Newcastle mwenye miaka 26 kutoka England. (i Paper)

Newcastle United wanataka kumsajili Dayann Methalie, beki wa Ufaransa mwenye miaka 19 aliyecheza mechi yake ya kwanza na kikosi cha kwanza cha Toulouse mwaka 2025. (The Sun)

Eintracht Frankfurt wana imani kubwa kuwa watamsajili Arnaud Kalimuendo, mshambuliaji wa Ufaransa mwenye miaka 23, kwa mkopo kutoka Nottingham Forest. (The Athletic)

Fulham wanakabiliwa na ugumu mkubwa katika harakati zao za kumsajili Ricardo Pepi, mshambuliaji wa Marekani mwenye miaka 22 anayeichezea PSV. (TeamTalk)

Manchester United wako tayari kumruhusu Sam Mather, winga wa England mwenye miaka 21, kuondoka mwezi huu huku klabu kutoka Uturuki na MLS zikionyesha nia ya kumsajili. (The Sun)