Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Roma inataka kumsajili Mohamed Salah

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool inatarajiwa kusajili beki ya klub Brugge wa Ecuador Joel Ordonez, 21, Januari hii kwa takribani £43m. (Mirror)
Roma ina nia ya kumsajili tena winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 33 kutoka Misri Mohamed Salah lakini huenda ikasubiri hadi msimu wa joto. (La Repubblica - kwa Kiitaliano)
Manchester United inavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa Jean-Philippe Mateta mwenye umri wa miaka 28 na beki wa Rennes Mfaransa Jeremy Jacquet. (Sky Sports)
Manchester United ina mpango wa kumuuza kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Ureno Bruno Fernandes, 31, na kuna uwezekano huenda akaondoka Januari hii. (Football Insider)
West Ham bado inamfuatilia winga wa Fulham wa Uhispania Adama Traore, 29, lakini mshahara anaodai inaweza kuwa kikwazo. (Telegraph - usajili unahitajika)
Real Madrid inatarajiwa kuanza tena mazungumzo ya mkataba na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 25, ambaye ana nia ya kusalia kwenye klabu hiyo. (AS - kwa Kihispania)
West Ham imekubali kumsajili mshambuliaji wa Lazio na Argentina Taty Castellanos mwenye umri wa miaka 27 kwa euro 29m (£25m). (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Nottingham Forest inamtaka mshambuliaji wa Wolves wa Norway Jorgen Strand Larsen. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia yuko kwenye rada za Crystal Palace. (Telegraph - usajili unahitajika)
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Chelsea inafikiria kuwasilisha dau la kumsajili mlinzi wa Santos Mbrazil Souza mwenye umri wa miaka 19, lakini AC Milan inaoongoza mbio ya kuwania saini yake. (AS - kwa Kihispania)
Fulham, Crystal Palace na Sunderland inamfuatilia kiungo wa kati wa Paris FC wa Algeria Ilan Kebbal, 27. (Football Insider)
Chelsea inavutiwa na kiungo wa Ugiriki na klabu ya Genk Konstantinos Karetsas, 18, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal. (Mirror)
Inter Milan wanataka kubadilisha mkopo wa mlinzi wa Uswizi Manuel Akanji kutoka Manchester City mwenye umri wa miaka 30 kuwa uhamisho wa kudumu. (Gazzetta - kwa Kiitaliano)
Manchester United hawana mpango wa kumrejesha mlinzi Mwingereza Harry Amass mwenye umri wa miaka 18 kutoka Sheffield Wednesday ambako amekuwa akicheza kwa mkopo. (Sun)
Newcastle inatarajiwa kuwasiliana na Toulouse kuhusu mpango wa kumsajili beki wa Ufaransa Dayann Methalie, 19. (Mail)
West Ham ina nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Raheem Sterling, 31. (Talksport)















