Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Man U, Bayern Munich na PSG wanamtaka Yan Diomande

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Yan Diomande wa RB Leipzig akikimbia na mpira wakati wa mechi ya Bundesliga kati ya RB Leipzig na 1. FC Heidenheim 1846 katika Uwanja wa Red Bull Agosti 30, 2025 huko Leipzig, Ujerumani.
Muda wa kusoma: Dakika 3

Beki wa Manchester City mwenye umri wa miaka 30, Nathan Ake, amekataa uhamisho wa kwenda West Ham. City wako tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, ambaye anatakiwa na timu kadhaa za Ligi Kuu England. (Talksport)

Manchester United huenda ikakabiliwa na ushindani kutoka Bayern Munich na Paris St-Germain wakati wa kumsajili winga wa Ivory Coast Yan Diomande, 19, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 52-61 kutoka klabu ya Ujerumani, RB Leipzig. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Tottenham na Wales Brennan Johnson, 24, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Crystal Palace katika saa 24 zijazo baada ya kuingia mkataba wa pauni milioni 35. (Telegraph)

Bournemouth ni mojawapo ya vilabu vya Ligi Kuu England vinavyoonyesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal, Ethan Nwaneri, mwenye umri wa miaka 18. (Mail)

Borussia Dortmund itajaribu kumsajili mshambuliaji wa Norway Oscar Bobb, 22, kwa mkopo kutoka Manchester City ikiwa kiungo wa kati wa Mmarekani, Cole Campbell, 19, au winga wa Ubelgiji, Julien Duranville, 19, wataondoka Januari. (Sky Sports)

Pia unaweza kusoma
k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eddie Nketiah

Mpango wa mshambuliaji wa Crystal Palace, Eddie Nketiah kujiunga na West Ham umepata pigo baada ya mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 kupata jeraha la misuli ya paja. (Talksport)

West Ham wanakaribia kuingia mkataba na mshambuliaji wa Gil, Vicente Pablo, 21, huku Mreno huyo akitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya jijini London. (Guardian)

Brighton inamfuatilia mchezaji wa Nordsjaelland na kiungo wa Ghana mwenye umri wa miaka 19, Caleb Yirenkyi, huku klabu hiyo ikiwa imeshawasajili winga wa Ivory Coast Simon Adingra, 23, na mshambuliaji wa Ghana Ibrahim Osman, 21, kutoka klabu hiyo ya Denmark. (Sky Sports)

Manchester United inavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Ufaransa, ambaye bado hajaongeza mkataba mpya kwa msimu wa joto wa 2027. (Football Insider)

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Manchester United, Manuel Ugarte

Mabingwa wa Uturuki Galatasaray wana nia ya kumsajili kwa mkopo kiungo mkabaji wa Manchester United, Manuel Ugarte, mwenye umri wa miaka 24, raia wa Uruguay. (CaughtOffside)

Celtic wako kwenye mazungumzo na Bournemouth kuhusu mkataba wa mkopo kwa beki Julian Araujo, 24, na wanataka mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico apatikane kwa ajili ya mchezo wao na Rangers hapo Januari 3. (Daily Record)

Beki wa kati wa Tottenham, Luka Vuskovic, mwenye umri wa miaka 18, amevutia macho ya Bayern Munich na RB Leipzig, ingawa Spurs wanasita kuachana na kijana huyo ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Hamburg. (CaughtOffside)

Kiungo wa kati wa Ufaransa, Eduardo Camavinga, 23, anataka kubaki Real Madrid huku Liverpool ikimtaka. (Teamtalk)

West Ham wanajiandaa kutoa dau kwa winga wa Uhispania na Fulham Adama Traore, 29. (Football Insider)