Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ulimwengu wa siri wa Diddy wafichuliwa kwenye video na ujumbe wa sauti
- Author, Na Rianna Croxford & Larissa Kennelly
- Nafasi, Uchunguzi wa BBC
- Muda wa kusoma: Dakika 6
"Vipi, unaweza kurekebisha hapa? Haionekani ya kifahari,"Sean"Diddy" Combs anasema katika ujumbe wa sauti kwa wasaidizi wake binafsi huku muziki wa R&B ukicheza chinichini.
Saa kadhaa kabla, kile kinachojulikana kama "Freak -off" - sherehe inayohusisha mambo ya ajabu ikiwa ni pamoja na ngono iliyochochewa na dawa za kulevya pia inajulikana kama "Wild King Night"- ilikuwa imepamba moto. Sasa, wafanyikazi walikuwa wakiitwa kufanya usafi.
"PD alisema atahitaji usafishaji wa dharura hotelini," mkuu wake wa wafanyikazi anatuma ujumbe baada ya tukio lingine la aina hiyo. "Mletee kitu cha kuondoa kwenye (kiti na kochi) na mifuko nyeusi ya kuzoa taka. Na baking powder, alisema."
BBC imepata ujumbe na rekodi kutoka kwa wafanyakazi wa zamani wa nyumbani kwa Combs. Wafanyakazi hao pia wametoa maelezo ya kina kuhusu jinsi ilivyokuwa kufanya kazi katika boti za kifahari za kukodisha za nguli huyo wa muziki wa RnB na ndani ya makazi yake makubwa kote Marekani - huko Hamptons, Beverly Hills na kwenye Star Island huko Miami.
Walihudumu miaka mitano hadi 10 iliyopita, kipindi ambacho kilikuwa kinachunguzwa wakati wa kesi ya jinai ya Combs huko New York.
Katika hitimisho la kesi siku ya Jumatano, Diddi mwenye umri wa miaka 55 alifutiwa mashtaka makubwa zaidi - ulaghai, na makosa mawili ya biashara ya ngono yanayohusiana na mpenzi wa zamani Casandra Ventura na mwanamke mwingine anayejulikana kama "Jane".
Lakini majaji walimpata na hatia ya makosa mengine mawili yanayohusiana na usafirishaji na kujihusisha na ukahaba na wanawake wote wawili. Hukumu dhidi yake itatolewa baadaye.
Tumeonyeshwa nyenzo ambazo zinatoa picha ya bosi "wa kutisha" na asiyetabirika, ambaye angesimamia "majaribio ya uaminifu" ya kushangaza, na ambaye madai yake yaliongezeka zaidi na zaidi.
Wafanyikazi wameelezea jinsi sherehe "freak-offs" zake za wakati mwingine zilifanyika katika maeneo kote ulimwenguni, huku rapper huyo akitarajia wafanyikazi kuandaa begi lenye "mafuta ya watoto, mafuta na taa nyekundu" - kutengeza mazingira yenye rangi nyekundu ya Combs inayoyapenda - pamoja na dawa za hali ya juu popote anaposafiri.
'Wild King Nights'
Ndani ya jumba lake la kifahari la Miami, eneo la $48m (£36m) lililo kwenye kisiwa cha kipekee kilichotengenezwa na binadamu, tumefahamishwa kwamba Combs iliwadhibiti sana wandani wake.
"Sitakaribia kuwa muwazi kwenu nyote," mfanyakazi moja wa kampuni ya Combs aliweka ujumbe uliorekodiwa na tajiri yao kwenye kikundi cha WhatsApp cha wafanyakazi mnamo 2020." Kuna sehemu za mbaya za giza ambazo [SIRI ambazo hungependa kufika bora ubaki mahali ulipo."
Wafanyikazi wanasema alikuwa mkali, mkandamizaji, huku wengine wakihusisha kutotabirika kwake kutokana na mtindo wa maisha unachochewa na dawa za kulevya. Mauzo ya wafanyikazi yalikuwa juu na Combs alikuwa na wasimamizi tofauti zaidi ya 20 ambao walijiunga na kampuni yake na kuliondoa ndani ya miaka miwili, msimamizi mmoja wa zamani wa maeneo ya makazi yalitua alituambia.
Phil Pines, 40, ambaye alifanya kazi kwa Combs kama msaidizi mkuu mtendaji kutoka 2019-2021, ameiambia BBC kwamba bwana huyo hakusema neno naye alipoanza kazi yake kwa mara ya kwanza.
"Ilikuwa kama jando," anaelezea. "Hatukuzungumza kwa siku 30."
Msaidizi mwingine wa hivi majuzi, Ethan (si jina lake halisi), anakumbuka: "Alikuwa mtu wa tabia za ajabu, mara mkali kupitiliza na wakati mwingine anakuwa mtulivu."
Tumebadili jina la Ethan kwa sababu, kama wafanyikazi wengi wa zamani, bado anafanya kazi katika tasnia ya utalii ya thamani ya juu na kuhofia kusema lolote kumhusu Combs kutaathiri kazi yake.
Ethan anatuonyesha kovu ndogo kwenye paji la uso wake. Anasema hii ilitokana na Combs kumpiga ngumi usoni na kumbamiza kwenye ukuta kwa hasira.
Phil Pines na Ethan walikuwa sehemu ya kikundi kidogo cha wasaidizi wanaoaminiwa wa Combs na wanasema mara nyingi alikuwa akiwafanyia majaribio ya uaminifu wafanyakazi wake ili kubaini uaminifu wao kwake .
Ethan anakumbuka moja ya majaribio ya uaminifu ya Combs - wakati nyota huyo alipovua moja ya pete zake na kuitupa kwenye Bahari ya Atlantiki. Kisha akamgeukia Ethan na kumwambia lazima aingie kwenye maji ili kuyachukua.
Walikuwa kwenye hafla rasmi na Ethan, kama bosi wake, alikuwa amevaa suti nadhifu. Anasema hii haikumzuia kuruka mara moja ili kuiokoa.
Katika tukio lingine, Pines anasema Combs alimwita kwenye makazi yake baada ya saa sita usiku, ili tu achukue rimoti ya TV kutoka chini ya kitanda alichokuwa na mgeni wa kike.
"Unaona? Yeye ni mwaminifu na sasa anaweza kurudi nyumbani," anakumbuka Combs akimwambia. Pines anasema alijisikia kama mnyama.
Lakini The Wild King Nights - kama mkuu wa wafanyikazi wa rappa, Kristina Khorram, alivyowataja - alifichua upande mbaya zaidi wa kufanya kazi kwa Combs.
"Niliombwa nitengeneze orodha ya nguo atakazovaa," anasema Pines. "Na nilijiuliza, kwa nini hakuna mtu yeyote alinielezea hili mwanzoni?"
Katika mojawapo ya mawasiliano yao yaliyoonekana na BBC, Khorram alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi kumuarifu kuwa unastahili kupanga amavazi yake kwa ajili ya Wild King Night ndani ya saa mbili. Katika ujumbe mwingine, aliomba "kupelekewa" chupa saba za mafuta ya watoto na chupa saba za vilainishi.
Ujumbe wa Khorram, uliotumwa miezi kadhaa iliyopita, unaonyesha jinsi wafanyikazi walivyotakiwa kujiandaa kwa 'Night Kings' mara kwa mara na kufanya usafi baadaye.
"Kupanga mafuta ya watoto na vilainishi vingine kwenye rafu ni jambo la kufedhehesha sana. Kila mara ningejifanya kama nilikuwa kwenye simu," Pines anatuambia.
Katika kesi nyingine ya Combs 'mwendesha mashtaka aliwasilisha ushahidi wa vifaa alivyosema vilinunuliwa kwa ajili ya"freak-offs". Polisi walipofanya msako kwenye kwenye jumba la Combs huko Los Angeles walipata dawa za kulevya na zaidi ya chupa 1,000 za mafuta ya watoto.
Baada ya kufanya kazi kwa miezi mitatu, Pines alianza kuwa na wasiwasi kuhusu vitu hivyo alivyoombwa kuwasilisha mara kwa mara. "Ikawa kila siku, wakati mwingine mara mbili kwa siku, kila siku, na kila wiki."
Pines anasema wanawake wadogo walitembelea nyumba za Combs - kufanya ngono hadharani. Vijana pia walialikwa kwenye sherehe hizo, anasema Ethan.
Baadhi ya vijana hawa wangeonekana kuwa marafiki wa wana wa nyota huyo, Pines anatuambia, huku baadhi ya wanawake baadaye wakionekana "wakitoka" na Combs.
Pines anasema pia alikuwa na wasiwasi kwamba baadhi ya wageni hao- ambao alikadiria kuwa na umri wa miaka 20 - walikuwa "wachanga" na "waliovutia" kwa bosi wake mwenye umri wa miaka 50.
"Ningeona baadhi ya wanawake wakiwa na mfadhaiko au walionekana kana kwamba walikuwa na usiku wenye shughuli nyingi," anasema Pines.
Mwanamke aliyekuwa na dripu ya sindano kwa kawaida angelikuja siku iliyofuata, anasema, kuwasaidia wageni kupata nafuu baada ya kushiriki "ngono" kwa saa 24 mfululizo bila chakula.
Pines anakumbuka mgeni mmoja mchanga aliyemwambia kwa huzuni: "Sijawahi kufanya jambo kama hilo maishani mwangu."
Aliagizwa kumpeleka nyumbani kwake kutoka kwa makazi ya Combs' Miami:"Alikuwa anatetemeka, kuashiria dawa kali zilizokuwa mwilini zimeaza kupungua ."
Suala la utumiaji wa dawa za kulevya kupita kiasi katika sherehe hizi mara kwa mara ulijitokeza wakati wa kesi ya Combs '.
Casandra Ventura, mpenzi wake wa zamani kwa zaidi ya muongo mmoja, alisema kwamba alivumilia miaka kadhaa ya kulazimishwa kufanya ngono na kiume tofauti huku Combs akirekodi matukio hayo. Alisema hafla hizo wakati mwingine ziliendelea kwa siku kadhaa na Combs alimtaka anywe dawa nyingi ili aweze kukesha.
Mwanamke mwingine, ambaye alichumbiana na Combs kutoka 2021 hadi kukamatwa kwake Septemba paka jana, alitoa ushahidi kwamba alihisi kushinikizwa kutimiza matakwa yake kwa sababu alikuwa akimlipa kodi, na alisema kukutana kwake kulimwacha "amechukizwa" na maumivu ya mwili.
Katika utetezi wake katika kesi, wakili wa Combs 'alikiri kwa unyanyasaji wa nyumbani, lakini alisema waliokubali kufanya ngono wote walikuwa rimeridia, na kwamba Combs alikishi "maisha ya ajabu".
BBC ime mfanyakazi mmoja aliombwa kutafuta mtandaoni kwa wasindikizaji kushiriki katika usiku wa Wild King. Picha za skrini za wasindikizaji zilitumwa kwa Combs ili kuidhinishwa.
Pines anasema hajui kilichotokea katika hafla hizo, lakini aliombwa kushughulikia athari zake.
Ilikuwa "balaa", anasema. "Mafuta sakafuni. Mabaki ya bangi kila mahali... nilikuwa navalia glavu....barakoa ili kusausafi."
"Yeye [Combs] angeamka, akavaa kofia yake na kutoka nje ya mlango," Pines anasema, akiwaacha wafanyikazi wakisafisha chumba.