Kwanini wagonjwa wa dengue wanapaswa kuongezewa damu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Idadi ya machapisho ya kuomba damu kwa wagonjwa wa dengue kwenye mitandao ya kijamii inaonesha jinsi hali imekuwa ngumu. Uhitaji wa damu huongezeka kutokana na kupungua kwa viwango vya seli ya damu katika mwili wa mtu aliyeambukizwa na ugonjwa huu wa mbu.
Seli hizo husaidia kuganda kwa damu na kuacha kutokwa na damu. Kiwango cha seli hizo kwa mwili wa binadamu ni kati ya 150,000 hadi 450,000.
Ikiwa hesabu ya seli iko chini ya kiwango hiki, damu haiwezi kuganda. Matokeo yake, kuna hatari ya kutokwa na damu.
Sio tu dengue, lakini magonjwa mengine yanaweza kupunguza idadi ya seli katika damu yenye maambuki.
Mtaalamu wa tiba wa Chuo cha afya cha Chittagong, Dkt. Aniruddha Ghosh anasema, ikiwa hesabu ya seli za damu itashuka chini ya 20,000, damu inaweza kutoka bila jeraha lolote. Wakati kama huo kuna hatari kubwa ya kutokwa na damu kutoka kwa sehemu yoyote ya mwili.
Mtaalamu wa dawa, Profesa ABM Abdullah alisema kuwa si lazima kuongeza damu ikiwa seli zimepunguzwa.
"Kwa sababu kwa wagonjwa wa dengue, upungufu wa chembe za damu sio tatizo pekee, bali upunguzaji wa plazima ya mwili, upunguzaji wa shinikizo la damu pia inaweza kufanya hali kuwa ngumu.
Katika hali hiyo, ikiwa mgonjwa atatibiwa kulingana na dalili, inawezekana kumponya mgonjwa. Katika kesi hii, inaweza kuwa sio lazima kuongezewa damu, "alisema.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Anasema, “wagonjwa wengi wa dengi hawahitaji damu. Idadi ya seli katika damu hupungua kwa muda mfupi sana - labda siku mbili au tatu. Kisha seli huanza kuongezeka. Kwa hiyo hatupendekezi kutiwa damu mishipani.”
"Pia tuna wagonjwa ambao wameshuka seli 10,000, lakini hiyo haitoshi. Mgonjwa amepata nafuu. Ikiwa damu ya mgonjwa iko juu, plazma iko chini, shinikizo la damu liko chini, basi hapo anaweza kuongezewa damu," alisema Profesa ABM Abdullah.
Mara nyingi kitengo kimoja cha seli ya damu huhitaji damu kutoka kwa wafadhili wanne. Uwekaji damu mishipani ni utaratibu wa gharama na mgumu. Sio hospitali zote nchini Bangladesh zilizo na mashine za kufanya hivyo.
Kwa sababu hii, ikiwa kuna mgonjwa wa dengue ndani ya nyumba, ni muhimu kujua mapema ikiwa hospitali iliyo karibu ina mfumo wa kuongeza damu.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani, homa ya dengue ina sifa kadhaa. Kwanza kabisa, seli za damu zitakuwa chini ya laki moja, protini ya kusukuma damu hupungua, kutakuwa na matatizo ya kuondoka kwa plazma kutoka kwa mishipa ya damu.
Wakati gani wa kuongeza damu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika homa ya dengue mashimo madogo katika kuta za mishipa ya damu ya mgonjwa huongezeka. Katika hili, sehemu ya maji ya damu au plazma hutoka nje kupitia ukuta wa mishipa ya damu.
Kutokana na baadhi ya sababu nyingine ikiwa ni pamoja na kupungua kwa seli, mgonjwa ana hatari ya kutokwa na damu katika ubongo, figo, moyo. Mshtuko wa moyo unaweza hata kusababisha kifo. Katika suala hili, alishauri kuchukua hatua za haraka.
Alisema, “iwapo tunaona damu inatoka na chembe za damu zimeshuka chini ya 20,000, basi tunashauri kuongeza damu kulingana na hali ya mgonjwa. Hata hivyo, tatizo kuu kwa wagonjwa wa dengue sio kupungua kwa seli. Eneo la wasiwasi hapa ni kushuka kwa shinikizo la damu la mgonjwa. Kwa sababu wakati shinikizo linapungua, mwili hukosa oksijeni. Hii huongeza hatari ya maambukizo ya viungo mbalimbali vya mwili."
Mbali na matatizo haya, ikiwa shinikizo la damu la mgonjwa hupungua sana, kiwango cha mapigo ya moyo huongezeka. Baadhi ya dalili ambazo madaktari wanaweza kupendekeza kupima damu:
* Dalili za kupungua kwa seli za damu.
*Kutokwa na damu chini ya ngozi.
*Upele mwekundu au mweusi huonekana kwenye mwili.
*Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi.
*Kutokwa na damu kutoka kwa mdomo, ufizi au pua.
*Kutokwa na damu katika mkojo au kinyesi.
*Kutokwa na damu kwa muda mrefu katika majeraha.
*Uchovu kupita kiasi na upungufu wa maji mwilini.
Vyakula vinavyoongeza damu

Chanzo cha picha, Getty Images
Madaktari wamewashauri wagonjwa wanaougua homa ya dengue kula chakula maalumu. Hata hivyo, kuna baadhi ya vyakula vinavyoweza kutumika kurejesha seli za damu zilizopunguzwa katika damu. Vyakula vitano ni:
1. Vitamin A kwenye maboga matamu tamu na mbegu zake husaidia kutengeneza seli kwenye damu. Kwa hivyo, ikiwa seli katika damu ya mgonjwa wa dengue hupunguzwa, wanaweza kula maboga tamu.
2. Kiasi kikubwa cha vitamini C katika maji ya limao huongeza kiasi cha seli katika damu. Pia huongeza kinga ya mwili. Kwa hivyo wagonjwa wa dengu wanapaswa kutumia maji mengi ya limao.
3. Matunda ya amalaki pia ina vitamini C nyingi. Amalaki huongeza kinga na kuzuia uharibifu wa chembe.
4. Mshubiri pia ni muhimu sana katika kusafisha maambukizi yoyote ya damu. Matumizi ya mara kwa mara ya juisi yake huongeza seli za damu.
5. Komamanga ina utajiri wa madini ya chuma. Ambayo hufanya kazi vizuri sana kuongeza seli kwenye damu na kuondoa udhaifu wa mwili. Kwa hivyo mpe mgonjwa juisi ya makomamanga ya kawaida.
Utafiti wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Asia, taasisi ya utafiti nchini Malaysia, umebaini kuwa juisi ya majani ya papai na juisi ya papai husaidia kuongeza idadi ya chembe za damu kwenye damu ya wagonjwa wa homa ya dengu.
Wataalam wanapendekeza kula mboga za kijani, matunda yenye vitamini C au juisi safi ya matunda, pamoja na vyakula vyenye vitamini B, protini, vitamini K, E.
Katika kesi hii, inashauriwa kujiepusha na chakula kilichowekwa kwenye vifurushi na vyakula vya vilivyokolezwa viungo.












