Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Atrophy: Tatizo la ukavu na kusinyaa kwa uke ni nini na linaweza kuzuiwa vipi ?
Wanawake wengi kote duniani wanaumia kutokana na hali inayosababisha kusinyaa na kukauka na kutokea kwa vidonda kwenye kuta za uke inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama vaginal atrophy. Kati ya asilimia 50 na 90% ya wanawake hupatwa na tatizo hili kulingana na takwimu. Lakini je ni kwanini idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni wengi? Ni kwasababu suala linalohusu ngono huwa halizungumziwi.
“Miaka iliyopita, ilidhaniwa kuwa ni wanawake wachache tu wanaopatwa na hali hii . Lakini sasa imethibitishwa kuwa wanawake wengi ni waathiriwa wa hali hii. Ni ugonjwa wenye dalili ,” anaeleza Laura Cámara,vmtaalamu wa ukunga, elimu ya ngono na mtaalamu katika ngono na afya ya uzazi.
Atrophy ya uke ni ugonjwa ambao una madhara ya kimwili na kisaikolojia yanayompata mwanamke mwenye ugonjwa huu. Bahati nzuri ni kwamba, kuna njia za kuutibu na kuuzuia.
Viwango vya chini vya homoni za estrogen
Kwa lugha ya kimatibabu hali hii genitourinary syndrome of menopause (MSS) kwasababu ugonjwa huu husababisha mabadiliko katika sehemu za siri.
Sasabu kuu ni kushuka kwa viwango vya estrogen. Kundi hili la homoni zinapatikana katika jinsia zote na ni muhimu kwa afya ya moyo, mifupa na ubongo. Estrogen ni kiungo muhimu katika afya ya uzazi ya mwanamke.
Kutokana na ukomo wa hedhi( menopause), uzalishwaji wa estrogen mwilini hupungua . Lakini sio tu katika kipindi hiki tu. Msongo wa mawazo pia ni mojawapo ya sababu zinazosababisha “kuathirika kwa homoni na katika mzunguko wa kawaida wa hedhi”.
“Kushuka kwa estrogen ni tatizo linalojitokeza wakati wa kunyonyesha, wakati unapotumia tembe za kuzuia mimba, na miongoni mwa wagonjwa ambao wana aina fulani ya saratani ya uzazi au uvimbe mwingine ambao matibabu yake yanaathiri kushuka kwa viwango estrogen.
Jambo hili hushuhudiwa kwa kawaida katika kipindi cha ukomo wa hedhi, hakuna anayeliepuka. Ni mabadiliko halisi ya kimwili,” anasema Cámara.
Dalili zinazopuuzwa sana
Wataalamu wa magonjwa ya kingono wanafafanua kuwa dalili ambazo zinajitokeza zaidi ni kukauka kwa uke na maumivu wakati wa shughuli za ngono.
Wataalamu wanasema kwamba 90% ya wanawake wenye hali hii ambao hufika hospitalini wakiwa na tatizo hili hutaja maumivu wakati wanapojamiiana.
“Tatizo ni kwamba maumivu wakati wat endo la kujamiiana huwa yanapuuzwa na kufichwa. Kuna wanawake wengi wenye maumivu ya ngono na hawawezi kuomba msaada , kwani wanasema , ni mada ambayo ni mwiko kuizungumzia ,” anasema Cámara.
Dalili nyingine ambazo hulalamikiwa ni kama vile ukosefu wa vilainishi vya kutosha wakati wa shughuli ya kujamiina, muwasho, na kutokwa damu baada ya kujamiiana. .
Dalili zinazoathiri mfumo wa mkojo ni pamoja na dysuria, mfano kupata ugumu, maumivu na kushindwa kutoka kwa mkojo wote kwenye kibomu, Kwenda haja ndogo mara kwa mara na maambukizi ya mkono yanayojirudia mara kwa mara, kulingana na Muungano wa madaktari bingwa wa afya ya uzazi ya Uhispania (SEGO)
Dalili nyingine ni kuwa na kiwango cha chini cha hamu ya ngono.
“ Atrophy ya uke, huambatana na kukanganyikiwa na wasi wasi na hili husababisha matatizo miongoni mwa wanandoa au wenzi. Wakati kujamiiana kunapokuwa kwa maumivu, mwanamke huwa na wasi wasi kwa kufikiria kuhusu tatizo alilonalo.. Ni vigumu kutoka kwenye rah ana kuingia katika maumivu ,”anasema Cámara.
Mtaalamu huyo wa ngono akumbuka kuzungumzia suala la ngono ni mada ambayo ni mwiko. Wanawake huumia kimya . “Inatokea kwamba wanawake wanakuja kliniki na kuniambia kuwa wamekuwa na maumivu kwa miaka mingi”.
Njia za kuzuia
Kiwango cha chini cha homoni za estrogen hutokea kwa wanawake. Kwahiyo, wataalamu wanashauri miongozo inayoweza kuzuia hali ya atrophy ya uke.
Kwanza kabisa SEGO inashauri mabadiliko ya mtindo wa maisha miaka ya kabla mwanamke hajafikia ukomo wa hedhi(menopause) ili kuzuia na kuepuka ugonjwa huu. Unafaa kuwa na uzito wa kawaida wa mwili, fanya mazoezi ya mara kwa mara na ule chakula chenye virutubisho vya kiafya.
Kuepuka au acha kuvuta sigara, kama vile tobacco “huongeza kiwango cha ujwezo au nguvu za homoniestrogen ,” unasema muungano wa SEGO.
Kuongeza usambaaji wa damu katika sehemu zetu za siri ni njia yenye ufanisi ya kuzuia ugonjwa huu.
Na ni vipi unaweza kufanikiwa kwa hili ?
Kwa shughuli za mara kwa mara za kujamiiana.
Zaidi huongeza oksijeni, na kuboresha uwezo wa kupanuka na vilainishi vya uke.
Kama mtaalamu wa masuala ya ngono, Camara anasisitiza kwamba pia ni muhimu kufanya mabadiliko ya jinsi unavyofanya tendo la kujamiiana.
"Ni lazima ufikirie kila mara mwenza wako na ufanye kila liwezekanalo kumfurahisha."
Suala ambalo ni mwiko kuzungumzwa
Kama tulivyosema kuanzia mwanzo, ni wanawake wachache wanaozungumzia kuhusu ugonjwa huu, hii ikiwa ndio maana tunawapata wagonjwa wachache wanaotembelea kliniki yetu.
Matokeo yake wanawake wengi huumia kimwili na kisaikolojia ili hali kuna tiba mbali mbali zinazoweza kumsaidia mgonjwa kupata nafuu.
Vilainishi vya uke na mafuta maalum kwa ajili ya sehemu za siri yapo, kulingana na SEGO. Kuna bidhaa ambazo hazina homoni, ambazo zinawea kukusanya maji na kuyatoa taratibu, na ni salama kwa afya.
"Tunaweza kuanza kuzitumia mara tunapoona kuwa hali ya kukauka kwa uke inajitokeza. Ni sawa na kulainisha tu Ngozi ya mwili," anaeleza Laura Cámara.
Hatua ya pili inahusisha tiba ya homoni inayotolewa na daktarik. Hizi zinaweza kuwa ni estrgen za muundo wa mafuta aina ya krimu,vidonge au pete za uke ambazo huingizwa ndani ya uke na kuachiuliwa homoni.
Pia kuna teknolojia ya tiba ya leza. Kupaka Kaboni diokside, asidi ya hyaluronic na radiofrequency ili kuamsha collagen na kupanuka kwa uke.
Hatahivyo, SEGO linasema kuwa kwa tiba ya Leza ya ukuta wa nje wa uke au tiba ya radiofrequency, ingawa tafiti nyingi hazijatoa matokeo ya kuridhisha, athari zake za muda mrefu hazijulikani .
Badala yake, inapendekeza njia nyingi za tiba zinazohusisha usaidizi wa elimu ya ngono.
“Ukomo wa hedhi ni lazima kwa mwanamke. Ndio maana elimu bora ya ngono inaweza kusaidia ‘’.