Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, ni wachezaji gani wa bei ghali zaidi waliowahi kusajiliwa?
Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza (Premier League) vinapanga mikataba ya bei ghali msimu huu wa joto huku Declan Rice na Josko Gvardiol wakiwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuhama.
Wakati rikodi za uhamisho zikionekana kushuka, BBC imeangalia baadhi ya wachezaji wa bei ghali zaidi kwa nafasi, ligi na utaifa. Kwa ajili ya uwazi, tunatumia ada za awali.
Walinda milango
Wengi wa makipa wa bei ghali zaidi wamekwenda kwenye timu za ligi kuu ya Uingereza, Chelsea ikiongoza kwa dau la pauni milioni 71, walimnunua Kepa Arrizabalaga wa Athletic Bilbao mwaka 2018.
Uhamisho wa Alisson wa pauni milioni 66.8 kwenda Liverpool kutoka Roma msimu huohuo unashika nafasi ya pili, ikifuatiwa na usajili wa Manchester City 2017 wa Ederson wa Benfica kwa pauni milioni 35.
Uhamisho huo wa Ederson ulihitimisha utawala wa miaka 16 wa Gianluigi Buffon kama kipa ghali zaidi duniani - kwa uhamisho wake wa pauni milioni 32.6 mwaka 2001 kutoka Parma kwenda Juventus.
Kuhamishwa kwa Thibaut Courtois kutoka Chelsea kwenda Real Madrid kunamweka katika nafasi ya tano bora, kwa ada ya dili ikiripotiwa kuwa na thamani ya hadi pauni milioni 35.
Walinzi
Wachezaji watatu bora katika nafasi hii wote walisajiliwa katika ligi kuu ya Uingereza kutoka vilabu vingine vya Uingereza. Mauzo ya The Foxes ya pauni milioni 80m ya Harry Maguire kwa Manchester United mwaka 2019 inasalia kuwa rekodi ya dunia.
Uhamisho wa Virgil van Dijk wa pauni milioni 75 kutoka Southampton kwenda Liverpool unashika nafasi ya pili, huku safari ya Wesley Fofana ya pauni milioni 70 kutoka King Power kwenda Chelsea mwaka jana ikishika nafasi ya tatu kwenye orodha hiyo.
Usajili wa Bayern Munich wa Lucas Hernandez kutoka Atletico Madrid kwa pauni milioni 68 mwaka 2019 na Matthijs de Ligt kutoka Juventus kwa pauni milioni 65.6m mwaka 2022.
Iwapo Gvardiol wa Croatia atahama kwa pauni milioni 86 kutoka RB Leipzig kwenda Manchester City, kama ilivyoripotiwa, basi ataongoza orodha hii.
Wachezaji wa Kati
Enzo Fernandez amekuwa kiungo ghali zaidi kuwahi kutokea kwa uhamisho wake pauni milioni 107 kutoka Benfica kwenda Chelsea mnamo Februari 1.
Mauzo ya Philippe Coutinho 2018 kutoka Liverpool kwenda Barcelona yalikuwa ya pauni milioni 105, wakati Jack Grealish aliigharimu Manchester City pauni milioni 100 kutoka Aston Villa mnamo 2021.
Ikiwa Arsenal watamsajili Rice wa West Ham kwa pauni milioni 105, ataingia katika nafasi ya pili.
Wanaokamilisha tano bora ni Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United kwa pauni milioni 89m mwaka 2016 na uhamisho wa Jude Bellingham msimu huu kutoka Borussia Dortmund kwenda Real Madrid kwa pauni milioni 88.5.
Wachezaji wa mbele
Wanasoka wawili ghali zaidi wote walijiunga na Paris St-Germain wakati wa majira ya joto. PSG walitumia pauni milioni 200 kumnunua Neymar wa Barcelona mwaka 2017 na baadaye Kylian Mbappe wa Monaco, kwa mkopo wa wa pauni milioni 165.7.
Uhamisho wa Atletico Madrid wa pauni milioni 113 kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Benfica Joao Felix mwaka 2019 ni wa tatu, ukiwaondoa Coutinho na Ousmane Dembele wa Barcelona.
Inayofuata ni ile ya pauni milioni 107 ambayo Barcelona ililipa Atletico kumnunua Antoine Griezmann, mwaka wa 2019, na kisha uhamisho wa Romelu Lukaku wa pauni milioni 97.5 kutoka Inter Milan kwenda Chelsea mnamo 2021.
Lukaku wa Ubelgiji anashikilia rekodi ya kipekee kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 294.5, akijiunga na Chelsea mara mbili, Everton, Manchester United na Inter.
La Liga ya Hispania
Vilabu vya Uhispania vimesajili wanne kati ya wachezaji 10 bora waliosajiliwa kwa bei ghali zaidi, ingawa labda cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyehusika na Real Madrid.
Uhamisho wa Atletico wa Felix ni nambari moja. Mengine ni mikataba ya Barcelona kwa Griezmann, Coutinho na Dembele - ambayo ni pauni milioni 97 kutoka Borussia Dortmund mnamo 2017.
Usajili mkubwa zaidi wa Real unabaki kuwa pauni milioni 89 walizolipa Chelsea kwa Eden Hazard mwaka 2019.
Ligue 1 ya Ufaransa
Paris St-Germain wana wachezaji wawili waliosajiliwa kwa bei ghali zaidi – ni Neymar na Mbappe.
Edinson Cavani ndiye anayefuata na uhamisho wake wa 2013 kutoka Napoli kwenda PSG kwa pauni milioni 55.
Monaco, ambao walilipa kitita cha pauni milioni 50 kwa Radamel Falcao wa Atletico Madrid mwaka 2013, ndio timu pekee ya Ufaransa iliyowahi kutumia zaidi ya pauni milioni 30 kununua mchezaji.
Premier League ya Uingereza
Dili la Chelsea la pauni milioni 107 kumnunua Fernandez ni rekodi ya Uingereza, ikifuatiwa na Manchester City kumnunua Grealish kwa pauni milioni 100.
Chelsea pia inashika nafasi ya tatu kwa kumsajili Lukaku kwa pauni milioni 97.5, huku Manchester United ikiwa imemsajili Pogba kwa pauni milioni 89m, winga wa Ajax Antony pauni milioni 82, Maguire pauni milioni 80m na mshambuliaji wa Everton Lukaku pauni milioni 75, akifuata Van Dijk wa Liverpool akigharimu pauni milioni 75.
Usajili wa gharama zaidi Uingereza: Grealish ndiye mwanasoka ghali zaidi wa Uingereza kuwahi kutokea, ingawa anaweza kupitwa na Rice siku yoyote kutoka sasa.
Mchezaji mwenzake wa Uingereza Bellingham anashika nafasi ya pili, akifuatiwa na winga wa Wales, Gareth Bale ambaye alihama kutoka Tottenham kwenda Real Madrid mwaka 2013 kwa pauni milioni 85.
Maguire, kwa pauni milioni 80, anafuatwa na Jadon Sancho ambaye alihama mwaka 2021 kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United. Mason Mount ndiye atakayefuata wakati uhamisho wake wa pauni milioni 55 kutoka Chelsea kwenda United utakapokamilika.
Kieran Tierney ndiye Mskoti ghali zaidi kuwahi kutokea, akijiunga na Arsenal kutoka Celtic kwa pauni milioni 25m mwaka wa 2019. Mchezaji wa thamani zaidi wa Ireland Kaskazini anasalia kuwa Jamal Lewis, ambaye alihamishwa kwa pauni milioni 15 kutoka Norwich kwenda Newcastle mnamo 2020.
Serie A ya Italia
Rekodi ya usajili wa ligi hiyo ya Italia ilikuwa ya mchezaji mwenye umri wa miaka 33, Juventus ikilipa pauni milioni 99.2 mwaka 2018 kumnunua Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Kilichofuata ni usajili wa Juve wa pauni milioni 75.3 wa mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain mnamo 2016 na kisha uhamisho wa pauni milioni 74 kwa Lukaku kutoka Manchester United Kwenda Inter mwaka 2019.
Juve wanafuata pia, Matthijs de Ligt aligharimu pauni milioni 67.5 kutoka Ajax mnamo 2019.
Bundesliga ya Ujerumani
Kama inavyotarajiwa, Bayern Munich wanahusika kwa wachezaji wengi waliosajiliwa Ujerumani. Rekodi inasalia kwa Lucas Hernandez kutoka Atletico Madrid mwaka 2019 kwa pauni milioni 68, ikifuatiwa na usajili wa mwaka jana wa De Ligt kutoka Juventus kwa pauni milioni 65.6.
Bayern ililipa pauni milioni 44.7 kwa winga wa Manchester City, Leroy Sane mwaka 2020 ambayo ni ya tatu kwenye orodha hiyo.
Ligi na nchi nyingine
Usajili mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na timu nje ya ligi tano bora za Ulaya ni usajili wa Shanghai SIPG wa pauni milioni 60 wa kiungo wa Chelsea Oscar mnamo 2017.
Usajili mkubwa zaidi wa vilabu visivyo vya Ulaya ulifanywa nchini China kati ya 2016 na 2019.
Hata hivyo, vilabu vya Saudi Arabia vinaweza kuanza kutishia hilo, huku Al-Hilal wakilipa pauni milioni 47 kwa nahodha wa Wolves Ruben Neves msimu huu wa joto.
Wachezaji wanane kati ya rekodi zilizosajiliwa kutoka nchi 10 bora kwenye viwango vya ubora vya kimataifa vya Fifa tayari wametajwa kufikia sasa.
Wa Argentina ni Fernandez, wa Ufaransa ni Mbappe, wa Brazil ni Neymar, wa Uingereza ni Grealish na wa Ubelgiji ni Lukaku.
Van Dijk anaongoza kwa wachezaji wa Uholanzi, Ronaldo akiwa juu kwa Ureno na Kepa ndiye Mhispania ghali zaidi.
Mchezaji wa bei ya juu zaidi wa Kroatia anasalia kuwa Luka Modric, kufuatia uhamisho wake wa pauni milioni 30 kutoka Tottenham kwenda Real Madrid miaka 11 iliyopita - ingawa Gvardiol ataishinda ikiwa atajiunga na washindi wa Ligi ya Mabingwa City msimu huu wa joto.
Sandro Tonali amekuwa Muitaliano ghali zaidi baada ya kusajiliwa na Newcastle kwa dau la pauni milioni 55 kutoka AC Milan.