Mashambulizi ya jeshi la anga la Sudan yaua mamia katika miji, masoko na shule - Ripoti

Vichwa na mabega ya wanawake watatu wamesimama karibu pamoja kwenye foleni. Wamevaa hijabu - moja ya chungwa, moja nyeusi na moja ya kijani na mbili zimetazamana na kamera na mmoja anaitazama.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Mamilioni ya watu wamekimbia mapigano yaliyoanza Aprili 2023
    • Author, Barbara Plett Usher
    • Nafasi, Africa correspondent
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Jeshi la anga la Sudan limefanya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya angalau raia 1,700 katika maeneo ya makazi, masoko, shule na kambi za wakimbizi wa ndani, kulingana na uchunguzi kuhusu mashambulizi ya angani katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Mradi wa Sudan Witness unasema umeandaa seti kubwa zaidi inayojulikana ya takwimu za mashambulizi ya anga tangu vita vilipoanza Aprili 2023. Uchambuzi wake unaonyesha kuwa jeshi la anga limetumia mabomu yasiyokuwa na eneo linalolengwa katika maeneo yenye watu wengi.

Data hizo zinazingatia mashambulizi ya ndege za kivita, ambazo ni Jeshi la Sudan (SAF) pekee lina uwezo wa kuzitumia. Hasimu wake, Kikosi cha (RSF), hakina ndege za kivita. Kinategemea droni, lakini mashambulizi ya droni hayakujumuishwa katika utafiti.

RSF imekosolewa kimataifa kwa madai ya kufanya mauaji ya kikabila katika eneo la Darfur Magharibi, hatua iliyosababisha Marekani kuituhumu kwa mauaji ya kimbari.

"RSF wanawajibika kwa uharibifu mwingi na ukiukwaji, na nafikiri haki inatendeka," anasema Mark Snoeck, aliyesimamia mradi. "Lakini pia SAF lazima wawajibike."

Jeshi la Sudan nalo limekosolewa kimataifa kwa mashambulizi yasiyolenga walengwa.

Halikujibu ombi la BBC la kutoa maoni, ingawa mara kadhaa limekanusha madai ya kulenga raia, likisema mashambulizi yake "yanalenga tu maeneo ya RSF yanayotambulika kama malengo halali ya kijeshi."

Sudan Witness ni mpango wa Center for Information Resilience (CIR), shirika lisilo la faida linalofichua ukiukaji wa haki za binadamu. Mradi huu ulifadhiliwa na wizara ya mambo ya nje ya Uingereza.

Sudan Witness ni mpango wa Kituo cha Kustahimili Taarifa (CIR), kikundi kisicho cha faida ambacho kinafanya kazi kufichua ukiukaji wa haki za binadamu. Ilipokea ufadhili kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Uingereza kwa mradi huu.

Kulingana na nakala ya mapema ya ripoti hiyo iliyopatikana na BBC, Sudan Witness ilichambua mashambulizi 384 ya anga yaliyofanywa kati ya mwezi Aprili 2023 na Julai 2025.

Mada zinazohusiana;
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Zaidi ya raia 1,700 waliripotiwa kuuawa na wengine 1,120 kujeruhiwa katika matukio walioyatathmini.

Kundi hilo linasema takwimu hizo ni kiasi kwa sababu hurekodi idadi ya chini zaidi inayoripotiwa.

Mashambulizi 135 yalihusisha maeneo ya makazi, na uharibifu wa nyumba na miundombinu ya raia ulithibitishwa.

Katika matukio 35, mabomu yalipiga masoko na maeneo ya biashara, mara nyingi yakiwa yamejaa watu.

Mashambulizi mengine 19 yaliathiri makundi yenye uhitaji mkubwa katika vituo vya afya, kambi za wakimbizi wa ndani na taasisi za elimu.

Sudan Witness inakiri kuwa utafiti wake haukamiliki kutokana na changamoto za kupata taarifa sahihi kutoka maeneo ya vita, hasa kutokana na mawasiliano duni na ugumu wa kuthibitisha vyanzo.

Inaeleza kuwa mashambulizi dhidi ya malengo ya kijeshi huenda yakawa hayakuripotiwa kwa kiasi stahiki.

Hata hivyo, kupitia mbinu makini, imeweza kujenga taswira pana ya kampeni za anga, ikiwa ni pamoja na ramani shirikishi inayoonyesha ukubwa wa mashambulizi na athari kwa raia.

"Kwa sisi kuthibitisha moja kwa moja kuwa SAF ilifanya shambulio fulani, tungehitaji video inayowaonyesha wakitekeleza shambulio hilo na ushahidi wa aina hiyo ni nadra sana Sudan," anasema Snoeck. "Ndiyo maana tumetegemea uchambuzi wa mamia ya madai ili kujenga picha jumuishi."

Mwenendo mkuu unaojitokeza ni mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo ya makazi na masoko, pamoja na idadi kubwa ya mashambulizi yanayodaiwa kulenga vituo muhimu vya kibinadamu na vya matibabu.

"Nafikiri mifumo hii inaonyesha wazi kuwa SAF haifanyi vya kutosha kulinda raia," anasema Snoeck.

Justin Lynch, mkurugenzi mtendaji wa Conflict Insights Group, kundi ambalo hufuatilia usambazaji wa zana za vita zinazoingizwa Sudan aliambia BBC kuwa raia wa Sudan ndio wanaobeba mzigo wa mapigano kati ya jeshi la Sudan na RSF.

"Mgogoro wa Sudan kimsingi ni vita dhidi ya raia," anasema. "Nguvu ya anga na silaha nzito zinawalenga zaidi raia kuliko kambi za kijeshi."

Sudan Witness inakadiria uaminifu wa taarifa za mashambulizi kwa kutumia taarifa za wazi, ikitathmini uaminifu wa chanzo, video za mitandaoni na picha za satelaiti.

Katika baadhi ya matukio, ushahidi uliopatikana uliwezesha kuthibitisha mashambulizi kwa kiwango cha chini hadi cha kati cha uhakika.

Baadhi ya matukio mengine yalionyesha moja kwa moja mabaki ya mabomu, mashimo ya mlipuko au uharibifu wa marisau ya kombora au risasi.

Katika tukio moja, Sudan Witness ilithibitisha video kadhaa zilizoonyesha shimo la mlipuko na bomu ambalo halikulipuka katika kambi ya Zamzam, Darfur Kaskazini. Bomu hilo lilifanana na SH-250, linalotengenezwa na shirika la kijeshi la Sudan.

Inatathmini uaminifu wa chanzo, uwezo wa kuchanganua eneo kupitia video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, na picha zinazopatikana za setilaiti.

Baadhi ya matukio yaliyochunguzwa na Sudan Witness yanaweza kutegemea ripoti pekee.

Lakini kikundi kinaangazia matukio ambapo risasi, volkeno za athari au uharibifu wa marisau ya risasi hutambuliwa.

Katika tukio moja kama hilo, Sudan Witness ilithibitisha video na picha nyingi zinazoonyesha volkeno yenye bomu ambalo halijalipuka katika kambi ya Zamzam kwa watu waliokimbia makazi yao huko Darfur Kaskazini.

Ganda lililopinda la bomu limefunikwa na vumbi na liko kwenye shimo.

Chanzo cha picha, Facebook

Maelezo ya picha, Mpiga picha katika kambi ya Zamzam alinasa picha hii ya bomu ambalo halikulipuka lililoanguka hapo mwaka jana

Bomu hilo lilifanana na SH-250, linalotengenezwa na shirika la kijeshi la Sudan.

"Hili ni moja ya matokeo yanayonishtua zaidi," anasema Snoeck. "Kwa nini kudondosha bomu lisilokuwa na eneo linalenga katika kambi ya wakimbizi wa ndani? Eneo hilo halikuwa hata chini ya RSF wakati wa tukio na sababu yake bado haieleweki."

Katika shambulio jingine, video nadra ilionyesha ndege ikatoa kishindo kikubwa kabla ya milipuko mingi kutokea huku raia wakikimbilia kujificha.

Zaidi ya watu 30 waliuawa na 100 kujeruhiwa katika soko la Hamrat al-Sheikh, Kordofan Kaskazini kulingana na ripoti.

Mashambulizi mengi yanayohusishwa na SAF yametokea Darfur, eneo linalodhibitiwa na RSF.

Mojawapo ni shambulio la Agosti 2024 katika hospitali ya el-Daein, mji mkuu wa kihistoria wa watu wa Rizeigat wanaounda sehemu kubwa ya RSF.

Sudan Witness ilithibitisha video iliyoonyesha marisau ya risasi yalivyoharibu makaazi.

Kwa mujibu wa WHO na Unicef, raia 16 waliuawa, wakiwemo watoto watatu na mfanyakazi mmoja wa afya. Hata kundi la waasi linaloiunga mkono serikali lilikosoa shambulio hilo.

Gazeti la Sudan Tribune, tovuti huru ya habari za mtandaoni, lilimnukuu msemaji wa vuguvugu la Justice and Equality Movement, ambaye alisema wananchi walishangazwa na mashambulizi ya anga ya kiholela yaliyolenga hospitali na makaazi ya raia wa kawaida.

Jiji la Nyala, Darfur Kusini, limekuwa ni eneo linalolengwa mara kwa mara. Uwanja wake wa ndege unadaiwa kutumika kupokea silaha za RSF, ikiwemo droni za kisasa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, ­ma­dai ambayo UAE imekanusha.

SAF inadai inalenga vifaa vya kijeshi, lakini Sudan War Monitor inasema jeshi halina uwezo wa kulenga kwa usahihi katika maeneo yenye msongamano.

Sudan Witness ilichambua msururu wa mashambulizi ya Februari mwaka huu, ambayo pia yalirekodiwa na shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch, yaliyoua angalau watu 63 katika maeneo ya makazi na duka la vyakula karibu na hospitali ya macho.

Mashambulizi katika masoko na vituo vya biashara yanaharibu maisha ya raia na kuyumbisha uchumi, na hivyo kuzidisha mgogoro wa kibinadamu.

Oktoba mwaka jana, angalau watu 65 waliuawa na 200 kujeruhiwa katika shambulio lililoharibu Soko la al-Kuma, Darfur Kaskazini. Picha za satelaiti zilionyesha alama mpya za uharibifu.

Bidhaa za mchuuzi wa matunda zimewekwa mbele ya jengo lililoharibiwa kidogo. Mtu anatazama matunda na watu wengine wanazunguka kwenye ardhi iliyojaa vumbi.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Mabomu ambayo yameanguka kwenye masoko yameua raia na pia kutatiza maisha ya wengine wengi.

Sudan Witness ilithibitisha eneo la picha za soko lililoharibiwa na kulithibitisha kwa picha za satelaiti zinazoonyesha alama mpya za uharibifu wa moto katika eneo hilo.

Al-Kuma iko umbali wa kilomita 80 (maili 50) kaskazini-mashariki mwa el-Fasher, hadi hivi majuzi kitovu cha vita vikali, na imekumbwa na mzozo wa mashambulizi ya anga ya SAF dhidi ya RSF.

"Haiwezekani kwa jeshi la nchi kuwalipua watu kwa mabomu kwa kutumia jeshi lake la anga na kudai kuwa linafanya hivyo ili kulinda nchi," afisa wa eneo hilo alimwambia Dabanga, mtangazaji huru wa Sudan.

Chanzo kingine cha habari kilisema mji huo umekumbwa na mashambulizi ya anga zaidi ya 30 tangu kuanza kwa vita.

"Ushahidi huu wa mashambulizi ya anga ya kijeshi kwenye soko na maeneo mengine ya kiraia, unaonyesha kutojali kwa wazi na kusikokubalika kwa usalama wa raia wasio na hatia wa Sudan," alisema afisa wa ofisi ya nje ya Uingereza. "Kwa upande wowote wa mzozo walioko, wahusika wa uhalifu huu mbaya lazima wawajibishwe."

Sudan Witness inaendelea kufuatilia mashambulizi ya angani yaliyofanyika mwezi Julai 2025, na inaona mwelekeo mpya wa matumizi ya droni na pande zote mbili.

Sudan War Monitor inaripoti kwamba mashambulizi hayo sasa mara nyingine hulenga makundi yanayoonekana kuunga mkono upande pinzani, ikiwa ni pamoja na shambulio la SAF la Oktoba linalodaiwa kuelekezwa katika hadhira ya nyumba ya kiongozi wa kidini mjini al-Kuma.

Mji huo unakaliwa na jamii ya Waziyadiya, moja ya makundi ya Kiarabu wahamaji wanaounga mkono RSF. Wiki hiyo hiyo RSF ilizindua mashambulizi ya droni na mizinga el-Fasher yaliyolenga kituo cha wakimbizi wa ndani na kuua watu takriban raia 60.

El-Fasher inakaliwa zaidi na makundi yasiyo ya Kiarabu kama Wazaghawa, ambao RSF huwafananisha na makundi ya kijeshi yanayolinda mji.

"Pande zote mbili hazitumii droni na nguvu za anga kulenga kambi za kijeshi; mashambulizi yao ni ya kiholela au yanakusudiwa kutisha raia na hayo ni uhalifu wa kivita," anasema Lynch.

SAF inadai kuwa RSF inajificha katika maeneo ya makazi na kwamba linafuata kwa makini sheria za kimataifa za kibinadamu, likiwalinda raia na mali zao.

Hata hivyo, pande zote mbili zimetuhumiwa kwa uhalifu wa kivita.

Wiki hii RSF na washirika wake wa Sudan Liberation Movement-North wameshtumiwa kwa mashambulizi ya droni katika chekechea na hospitali mjini Kalogi, Kordofan Kusini. WHO iliripoti vifo vya watu 114, wakiwemo watoto 63.

Lynch anasema raia wanaendelea kuteseka ilhali hakuna upande unaofaulu katika vita vya anga.

"SAF walisaidiwa na mashambulizi ya anga kuchukua Khartoum, lakini kando na hilo, wamesababisha vifo vingi bila mafanikio ya kijeshi," alisema.

"Vivyo hivyo, RSF wanatumia mamluki wa kigeni wanaoungwa mkono na UAE kuendesha droni, lakini mafanikio yao yamekuwa machache."

Ramani ya Sudan inayoonyesha udhibiti wa maeneo kufikia tarehe 28 Oktoba 2025. Maeneo yanayodhibitiwa na jeshi na makundi washirika yametiwa alama nyekundu, RSF na makundi washirika kwa rangi ya buluu, na makundi mengine yenye silaha kwa rangi ya njano. Miji muhimu kama vile Khartoum, el-Fasher, Tawila na al-Dabbah imepewa lebo. Mto Nile pia umeonyeshwa. Chanzo: Mradi wa Vitisho Vikuu katika Taasisi ya Biashara ya Marekani.
Soma pia:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid