Je matokeo ya uchaguzi wa Kenya yalichakachuliwa?

Na Peter Mwai & Jake Horton

William Ruto alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Kenya was declared the winner of Kenya's presidential election zaidi ya wiki mbili zilizopita akiwa na asilimia 50.5 ya kura, lakini mpinzani wake Raila Odinga anapinga matoke, akidai kuwa ni ulaghai.

Mawakili wa Bw Odinga wameangazia zaidi ya vituo 40 vya kupigia kura wakisema kuwa jumla ya kura hizo zilivurugwa ili kuongeza kura za Bw Ruto na ili kufikia 50% inayohitajika kushinda.

Tumelinganisha picha za nakala halisi za matokeo kutoka kwa vituo hivi vya kupigia kura na zile zilizosajiliwa kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi.

Je, ni madai gani?

Nchini Kenya mara baada ya shughuli ya kupiga kura kukamilika na kura jizo kuhesabiwa, msimamizi wa uchaguzi katika kila kituo cha kupiga kura anatangaza matokeo hadharani na kujaza fomu inayojulikana kama Fomu 34A.

Fomu hii inasainiwa na wawakilishi wa chama kabla ya kuwasilishwa kwa mfumo wa kielektroniki katika kituo cha kitaifa cha kujumuisha kura.

Fomu hizi zote huwekwa mtandaoni na Tume ya Uchaguzi.

Mawakili wa Bw Odinga wanasema kuwa katika maeneo 41 ya kupigia kura fomu 34a zilizowasilishwa kwa njia ya kielektronikizilibadilishwa ili kuongeza idadi ya kura za Bw Ruto kabla ya kuchapishwa rasmi mtandaoni na Tume ya Uchaguzi.

Hapa kuna sehemu ya ombi kwa Mahakama ya Juu ambapo madai haya yanatolewa:

Ili kutengua mjadala wa kisheria, ombi hilo linadai kuwa ujumlisho katika fomu za kutangaza mshindi zilibadilishwa ili kumpendelea Bw Ruto.

Takwimu zilirekebishwa, inasema, wakati wa kuhakikisha kura zote zilizopigwa zinabaki sawa.

Ombi linaendelea kueleza kuwa kulikuwa na "nakala za kielektroniki" za fomu hizi zilifanyiwa mabadiliko baada ya kutumwa kutoka vituo vya kupigia kura.

Tumegundua nini?

Kwa hivyo tuliazimia kutathmini nakala za awali za kabla ya kutangazwa kwa matokeo kutoka kwa vituo kadhaa vya kupigia kura kadri ya uwezo wetu, ili kuona kama zinatofautiana kwa njia yoyote na fomu zilizowekwa mtandaoni.

Tuligundua kuwa kila fomu iliyotiwa saini ilijumuisha nambari za simu za mawakala wa vyama waliokuwepo wakati wa kujumuisha kura.

Mawakala hawa ni watu walio na ufungamano na vyama tofauti vya siasa ambao hufuatilia shughuli ya kuhesabu kura ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika bila dosari yoyote.

Kisha tukaanza kuwapigia simu wote mmoja baada ya mwingine ili kuwauliza ikiwa wamepiga picha karatasi za matokeo wakati wa tangazo - na ikiwa ni hivyo, tukaomba kama wanaweza kututumia.

Tulipata majibu kutoka kwa maajenti 23, wakiwemo sita kutoka kwa chama cha Bw Odinga mwenyewe, na picha za fomu halisi kutoka maeneo 21 kati ya 41 yalizotambua.

Mawakala wawili walitupatia hesabu walizoandika wakati huo lakini hawakupiga picha.

Kwa kila hali matokeo kutoka kwa vituo vya kupigia kura yalilingana na hesabu rasmi zilizochapishwa na Tume ya Uchaguzi.

Uchunguzi wa fomu kwa karibu

Nakala halisi ya fomu ya kutangaza matokeo inapatikana katika kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi, na mtu yeyote anayeruhusiwa kisheria kuingia kituo cha kupigia kura, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari na waangalizi, anaruhusiwa kupiga picha fomu ya matokeo.

Chini ya kila hati hizi pia kuna majina na nambari za mawakala waliopo. Tumeziba majina ili kulinda utambulisho wao.

Mara nyingi wao hupiga picha ya hati ya mwisho ya kutangaza kura, na hawa ndio watu tuliowasiliana nao katika maeneo 41 ambayo ilikuwa imeangaziwa na timu ya Bw Odinga.

Kisha tuliweza kulinganisha hati asili na ile iliyowekwa rasmi mtandaoni na Tume ya Uchaguzi ili kuona ikiwa jumla ya kura zilikuwa tofauti. Wote walikuwa sawa.

Picha ambazo zilitumwa kwetu, mbali na moja, zina rangi na stempu ya uthibitisho ya zambarau inayoonekana wazi. Kwa hivyo tunaweza kuwa na uhakika kuwa hazikuchukuliwa kutoka kwa tovuti ya tume, ambapo picha zote ziko katika rangi nyeusi na nyeupe.

Lengo letu katika makala haya ilimekuwa kutafuta ushahidi wa kuunga mkono madai ya Bw Odinga kwamba uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu lakini hatujaweza kupata ushahidi wowote.

Tumewasiliana na timu ya Bw Odinga ili kutoa ushahidi wa maandishi kuhusu madai hayo ya udanganyifu, lakini hakuna hata mmoja ambaye amepatikana.

Mahakama ya Juu ya Kenya inatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu ombi hilo siku zijazo.