Mazungumzo ya Kim Jong Un na Putin: Je, kuna mafanikio?

fd

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Rais Putin (kushoto) na Kim Jong Un

Katika karamu yao ya kifahari, walikunywa divai ya Kirusi na kukumbatiana na kogengesha glasi. Na kabla ya kuondoka, walibadilishana bunduki kama zawadi - bunduki za kisasa kutoka katika ghala la silaha za kila mmoja. Haya yote yanaashiria uhusiano wao unazidi kuimarika.

Alisafiri kwa masaa katika treni yake ya kivita. Kiongozi wa Korea Kaskazini alitumia siku kadhaa nchini Urusi kuzuru maeneo ya meli, viwanda vya ndege na maeneo mengine ya kijeshi kabla ya kurejea nyumbani.

Aliwaacha Wamagharibi wakisema hili na lile kwa masaa 40 kabla hajafika ya kufika Vostochny Cosmodrome - kituo cha anga cha mashariki ya Urusi. Hata wakati huo, haikujulikana ni nini hasa wawili hao wanegezungumza. Na onyo la White House wiki iliyopita kwamba Korea Kaskazini inaweza kuiuzia Urusi silaha likazidi kuzua hofu.

rfd

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Eneo la kurushia satalaiti

Putin alikuwa ametanguliza tafrija ya kumkaribisha Kim wakati treni yake ilipoingia Urusi. Ngazi zenye zulia jekundu ziliwekwa, zikisubiri treni ifike na kiongozi wa Korea Kaskazini atoke nje.

Putin alikuwa akingoja Kim alipowasili la gari lake. Kabla kamera hazijawashwa viongozi hao wawili walipeana mikono - picha zikapeperushwa mara moja katika vyombo vya habari vya serikali.

"Viongozi wote wawili wanajua nguvu ya kujionesha, lakini Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini, kama anavyojulikana Kim, ni shabiki wa sherehe. Yeye ni wa tatu katika nasaba ya viongozi wakuu," anasema Sarah Son, mtaalam wa Korea Kaskazini katika Chuo Kikuu cha Sheffield.

"Ni muhimu sana kwa Kim kuwa na mikutano ya moja kwa moja na viongozi wa nchi nyingine ili macho yote yawe kwake, na kuifanya Korea Kaskazini ionekane kama mdau muhimu wa kimataifa."

"Vikwazo bila shaka vinasalia kuwa vikali sana na hitaji la Urusi la silaha linatoa fursa ya kufikia malengo mawili ya ziada: mapato kwa taifa la Korea Kaskazini na ushahidi kwamba Kim anastahili kuzingatiwa na kiongozi wa mamlaka kuu ya kimataifa."

Saa moja kabla ya viongozi hao wawili kukutana, Pyongyang ilikuwa imerusha makombora mawili ya balistiki - ya kwanza kurushwa bila kiongozi huyo nyumbani.

Kuna Mafanikio?

C

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Watu wakifuatilia katika runinga
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mbali ya shamrashamra, waangalizi wanahoji kama mkutano huo ulipata mafanikio yoyote madhubuti, wakati ambao kidogo kimefichuliwa hadharani.

"Kufikia sasa, inaonekana kwamba hakujakuwa na maendeleo makubwa," anasema Fyodor Tertitskiy, mtafiti wa kijeshi wa Korea Kaskazini katika Chuo Kikuu cha Kookmin huko Seoul.

"Tuliona tukio la pande mbili - tamasha kubwa ambalo limeundwa kwa ajili ya watazamaji wa kigeni na makubaliano ambayo hayajafichuliwa nyuma ya milango iliyofungwa, ambayo umuhimu wake bado haujulikani."

Badala yake hatua pekee inayojulikana inaonekana kuwa Putin akidokeza kuwa anaweza kuisaidia Korea katika malengo ya satelaiti.

Pyongyang imeshindwa mara mbili mwaka huu kupaisha satelaiti ya uchunguzi angani - teknolojia yake iko nyuma kwa miongo nyuma ya Urusi.

"Hii inapaswa kuwa wito wa kuamsha kwa nchi nyingine zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu haja ya kuongeza juhudi katika kutekeleza vikwazo dhidi ya Pyongyang," anasema Leif-Eric Easley, profesa katika chuo kikkuu cha Ewha, Seoul.

rfdf

Chanzo cha picha, KCNA

Maelezo ya picha, Kim husafiri mara chache kwa sababu za kiusalama

"Kuna uwezekano kwamba Putin analenga kutumia mkutano huu kama njia ya kukabiliana na Seoul, uwezekano wa kuwakatisha tamaa kutoa silaha kwa Ukraine, inasemekana wanataka kutoa teknolojia ya kijeshi kwa Korea Kaskazini kwa kulipiza kisasi," anasema Tertitskiy.

Lakini bado kuna mashaka makubwa juu ya kama Urusi ingeshiriki vyombo vyake vya angani, au hata kuona mikono ya Kaskazini kama kitu chochote zaidi ya usambazaji wa nakala.

"Hata kuhusiana na teknolojia ya satelaiti, kauli za Putin zilikuwa za tahadhari, si ahadi ya wazi ya kutoa msaada bali ni jambo ambalo linaweza kuzingatiwa," anasema Bw Tertitskiy.

Pia ameeleza kuwa hakuna mtiririko wa fedha kati ya nchi hizo mbili - biashara inasalia karibu sifuri kulingana na makadirio ya Korea Kusini. Korea Kaskazini bado inaitegemea China kwa zaidi ya 95% ya mapato yake ya kibiashara.

"Hii inatuacha kutokuwa na uhakika ikiwa mkutano huu utatoa matokeo madhubuti kama ule mkutano usio na matunda wa 2019," anasema Tertitskiy, akirejelea mara ya mwisho viongozi hao wawili kukutana.

Putin alichagua kumpa Kim jukwaa, katika ukumbi tofauti kabisa - akileta zulia jekundu, karamu, bendi - na yeye mwenyewe kufunga safari ya kukutana naye huko.

"Ni ishara ya heshima kwa Kim. Hii inaweza kuonekana kama ishara ya kuhakikisha Kim anahisi kuthaminiwa," anasema Tertitskiy.

Anasema, pia ni kuhusu ujumbe unaotumwa kwa nchi za Magharibi. Ni muhimu kuzingatia kile ambacho pande hizo mbili hufanya, anasema.

"Kim na Putin ni mahiri katika kutumia udanganyifu. Kwa mara nyingine tena, ni muhimu kuchunguza matendo yao badala ya maneno yao."

sdc

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Viongozi hao wakitembelea kituo cha anga za juu