Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, ni mawe gani haya ya ajabu yamepatikana katika mwamba wa miaka bilioni 2.8
Mawe yaliyopatikana yalikuwa ya umbo la tufe yaliyong'aa, yakiwa na mistari iliyochongwa, iliyofanana sana na mpira wa kriketi.
Kwanza kabisa, inaonekana kwamba mawe hayo, kipenyo chake kisichozidi sentimita 10, yalichongwa na mikono ya binadamu na ni sehemu ya urithi wa akiolojia ya kale.
Lakini cha kustaajabisha ni kwamba mawe hayo yaligunduliwa ndani ya mwamba wa pyrophyllite (madini yanayotumika kwa michongo ya Kichina) iliyotengenezwa karibu miaka bilioni 2.8 iliyopita.
Ilikuwa ikisafirishwa hadi katika mji wa Klerksdorp kaskazini mwa Afrika Kusini kwa ajili ya utafiti na baadaye kuonyeshwa kwenye jumba kuu la makumbusho la mji huo.
Cairncross anadokeza kwamba mawe hayo yako mbali na kuwa fumbo, na pia ni yenye uwezo kidogo wa kueleza kuhusu viumbe kwenye sayari ya mbali.
"Tulifikiri hakuna haja ya kueleza jambo ambalo lilionekana dhahiri: kwamba mawe yalikuwa yametolewa kutoka kwa miamba iliyoundwa mabilioni ya miaka iliyopita," mwanajiolojia alisema.
"Ingawa inaweza kueleweka kuvutia hadhira, aina hii ya mawe ni ya kawaida sana katika uundaji wa pyrophyllite," alielezea.
Lakini ilikuaje hadi kuwa na umbo hili?
Kama mtandao wa IFScience unavyoonyesha, katika miaka ya 1980 machapisho kadhaa yasiyo za kisayansi yalianza kudai kwamba mawe ya Klerksdorp yalitengenezwa na "ustaarabu wa hali ya juu".
Kama ilivyobainishwa na machapisho mengine, ikiwa ni pamoja na Jarida la Lapidary, baadhi ya machapisho yalichambua zaidi na kuongeza kuwa mawe hayo yanazunguka yenyewe ndani ya sanduku la kioo ambako yaliwekwa.
Ndiyo maana jumuiya inayojulikana kama Society for the Rational Investigation of Paranormal Phenomena ilitafuta ushirikiano wa Cairncross kukanusha hoja zilizokuwa zikipata wafuasi zaidi na zaidi.
"Maelezo ya kimsingi hayakutosha, yaani kwamba mawe hayo yalitokana na mchakato uliofanyika zaidi ya miaka bilioni 2.8, lakini ilibidi kuelezea zaidi jinsi yalivyoundwa", alieleza msomi huyo.
Ili kufanya hivyo, anasema, miamba hiyo ilipatikana katika mchakato unaojulikana kama "dominant group" kwa kiingereza.
Sifa kuu ni kile kinachounda mkusanyiko huu, na tabaka kadhaa za lava ya volkano ambayo iko juu yake na ambayo, baada ya shinikizo nyingi na joto, imegeuka kuwa pyrophyllite, nyenzo inayofunika tufe," alisema.
Mwanajiolojia mwenyewe anaamini kwamba upekee wa mawe ni kutokana na ukweli kwamba yamebakia kwa mamilioni ya miaka chini ya shinikizo na joto ambalo hujitengeneza ndani ya mwamba mkubwa, ambako yamesalia, na kwamba pia yamekumbana na maji mengi kama inavyotokea kwenye mmomonyoko wa udongo.
"Mawe hujulikana kama ‘concretions’: umbo la duara au yai hivi yanayoundwa na madini mbalimbali yaliyopo kwenye miamba mwenyeji. Ni kawaida sana, yakiwa yamepatikana kwa maelfu ya miaka duniani kote," anabainisha mwanajiolojia.
Mawe hayo, anaongeza mtaalam, hupatikana katika miamba yenye chembe laini kama vile pyrophyllite ambayo hupatikana kwa wingi katika eneo hili la Afrika Kusini.
Maelezo ya kisayansi ya uwongo yanaenea
Cairncross anaeleza kwamba moja ya sababu aliamua kutoa maelezo mapana zaidi ya mawe hayo ni kwamba watu wengi waliamini katika machapisho ya kisayansi ya uwongo yaliyokuwa yakienea.
Mwanajiolojia huyo anarejelea jarida ambalo liliripoti kwamba mawe hayo yaliletwa kwa Shirika la Anga la Marekani (NASA) na kunukuu ripoti ambayo ilionyesha utengenezaji wake ulikuwa "mahali ambapo uvutano ni sifuri".
Lakini mtaalamu huyo anatambua kwamba mawe ya Klerksdorp yana umaalum ambao haupatikani katika mawe mingine yote yanayofanana nayo yanayopatikana ulimwenguni: mistari sambamba iliyopo juu yake na ambayo huyapa mwonekano wa mpira wa kriketi.
"Ukweli ni kwamba, sio mistari, lakini tabaka", anaelezea mwanajiolojia.
"Ni matokeo ya ishara iliyoachwa na mwamba mwenyeji, ambayo ilijijenga kwa tabaka kwa muda mrefu sana, na kusababisha hilo ambalo sasa unaweza kuona," alielezea.