Maeneo 5 muhimu ya kuvutia ya Doha, mji mkuu wa Qatar

Getty

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC WORLD

Maelezo ya picha, Ushauri bora katika Souq Wakif ni kupotea katika mitaa yake iliyofunikwa ili ugundue maajabu

Furaha ya soka haikupi muda wa kutosha kuelekeza macho kwingine nje ya viwanja saba vya kifahari zinakochezwa mechi za Kombe la Dunia.

 Lakini nje ya viwanja hivyo, Qatar hususan mji mkuu Doha, ni mji unaojidhihirishwa wenyewe kwa maelfu kwa maelfu ya mashabiki.

 "Ni tofauti na kile ambacho tumekizoea, lakini tunafurahia kuwa na wakati mzuri kwa kufahamu sehemu tofauti za Doha," Maya Alba, shabiki wa Mexico, anaiambia BBC

‘’Tangu wakati tulipowasili, niliona ni mji wa kuvutia " anasema David Marcilli, kutoka Argentina.

1: Sauq Wakif, Soko la mji mkuu

g

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC WORLD

Maelezo ya picha, Ufugaji wa Tai unachukuliwa kama uraibu miongoni mwa watu wa Qatar

Souks – au Masoko kwa lugha ya kiarabu – yamekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku nchini Qatar kwa karne nyingi na Souq Wakif , soko lililopo katikati ya mji wa Doha, shughuli nyingi za kijamii hufanyika katika mwezi huu wa Kombe la Dunia.

Souq Wakif la sasa limejengwa katika eneo sawa na mahala ambapo lilikuwa soko la zamani na mahala akilipo kituo cha soko la biashara la mji mkuu.

Ushauri mzuri unaopewa kuhusu soko hili lenye muundo wa mraba lenye masoko mbali mbali ni kujipoteza ndani ya mitaa yake ili kulielewa vyema.

Hapa kuna maajabu ya kila aina. Viungo vya vyakula, mavazi, bidhaa za ukumbusho, marashi, na hata hospitali kwaajili ya wachuuzi wa mitaa yake na wanunuzi.

Ufugaji wa ndege aina ya tai umekuwa uraibu wa wenyeji wa Qatar kwa miaka mingi .

Kwenye mitaa ya souk, watembeji wote wa miguu huburudika na sauti za ala za Mashariki ya kati. Kwenye veranda, wenyeji na watalii huvuta shisha – sigara inayovutwa kwa kutumia mirija na kuna migahawa ya vyakula vya Kiarabu, kutoka Syria, Uturuki na Uajemi.

2: Makumbusho ya Kitaifa

g

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC WORLD

Maelezo ya picha,

Mjini Doha kuna majengo yaliyojengwa kwa mvuto na jumba la makumbusho la taifa ni mojawapo ya majengo maarufu zaidi.

 Muundo wake ulibuniwa na mhandisi wa Kifaransa aliyeshunda tuzo Jean Nouvel .

Maumbo ya jengo yake hutengeneza muundo unaofahamika kama waridi la jangwani.

Limejengwa karibu na ghuba na mahala lilipo unaweza kuitazama kasri asilia ya Sheikh Abdullah bin Jassim al Thani.

 Ndani yake kuna historia ya watu maarufu wa wa Qatar na matukio ya kihistoria ya nchi.

3: makumbusho ya Sanaa ya Kiislamu

g

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC WORLD

Majengo mengine yanayoonekana kwa urahisi kwa macho yalibuniwa na msanifu majengo Mmarekani mwenye asili ya China IM Pei.

 Uislamu ni kila kitu na ndio unaotawala maisha, tamaduni na sheria nchini Qatar. Makumbusho haya huadhimisha urithi wote wa usanii ulioachwa katika Ulimwengu wa Kiarabu kuanzia vipuli, silaha , mazulia, michoro na vinyago.

 Miongoni mwa vitu vya thamani zaidi ni moja ya nakala za Koran iliyoandikwa kale zaidi . iliyoandikwa miongo michache tu baada ya kifo cha Mtume Muhammad na inaonyesha hatua chache za maandishi ya Kiarabu.

Makumbusho hayo yana maktaba na zaidi ya vitabu 20,000 .

4: Mwambao wa Ghuba wa Doha

g

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC WORLD

Kwenye kilomita saba, kuna mwambao wa Ghuba ya Doha.

Ni mahala panapowavutia wenyeji wa Qatar, wataalamu wanaokuja kufanya kazi pamoja na watalii husasan wakati jua linapotua na usiku kuingia.

Baadhi ya vivutio vya mji, kama vile Souq Wakif, na makumbusho ya taifa, makumbusho ya Sanaa ya Uislamu na kasri la Emir sehemu ya njia inayoelekea katika viwanja vya soka.

Zaidi ya hayo, kuna shughuli nyingi za burudani na maeneo mengi ya kuvinjari, ikiwemo migahawa, baa, bustani na vituo vya utamaduni.

5: Msikiti wa Imam Muhammad bin Abdul Wahhab

g

Chanzo cha picha, JOSÉ CARLOS CUETO / BBC WORLD

Tulifika kweney Msikiti mkubwa zaidi nchini Qatar muda mfupi kabla ya jua kuchomoza.

 Jua huchomoza nyuma ya jengo lake la kifahari na kuupatia rangi za kuvutia ambazo haiwezekani kuzisahau.

Msikiti ulizinduliwa mwaka 2011. Tofauti na jengo la makumbusho ya taifa na Makumbusho ya Sanaa ya Kiislamu, Msikiti muundo wa msikiti ni rahisi, ulijengwa kwa kufuata uhandisi wa muundo wa utamaduni wa zamani wa Kiislamu.

 Msikiti huu una maktaba tatu, vyumba vitatu tofauti vya kuswali kwa ajili ya wanaume na wanawake, na vyumba maalumu vya kusoma Quran.

Unauwezo wa kuwapokea waumini 30,000 na sakafu yake ya marumaru husaidia kupoza jengo la Msikiti wakati wa msimu wa joto kali .

Vivutio vingine

Qatar ni nchi ambayo inajengwa na kutengenezwa kwa usasa kwa kasi kubwa.

Hii inamaanisha kuwa katika miongo iliyopita imekuwa ikijazwa vituo vya vivutio vya kipekee vinavyoonekana kwa ubora wa muundo wake na huduma zinazotolewa

La Perla ni moja ya mifano hii. Kisiwa bandia chenye , makazi ya kifahari, fukwe binafsi, ofisi, maduka, migahawa na baa.

Ardhi yake kwanza ilitolewa kwa ajili ya kuuzwa kwa ajili ya wageni wawekezaji.

Pia kuna kituo cha Msheireb , mradi wa vizazi na moja wapo ya miji bora duniani ya kidigitali.

Mradi huu ni aina ya mradi wa majaribio wa Qatar katika juhudi zake za kutafuta njia za kudumu zaidi za kupunguza utegemezi wa mafuta yatokanayo na uchomaji wa makaa yam awe.

 Katika mkakati wa Qatar wa kuboresha elimu yake na kuifanya kuwa ya kisasa ilijenga Mji wa Elimu mwaka 2003 .