Utafiti: Unajua binadamu anaweza kutembea gizani kwa hisia za 'masikio'?

Sio tu Pomboo, nyangumi na popo wanaoweza kuzunguka angani ama popote tena gizani kwa kupitia masikio, lakini pia binadamu wanaweza kufanya hivyo ingawa sio kwa ustadi mkubwa kama wanyama hao.

Utafiti uliofanywa na kundi la wanasayansi wa Uingereza lilionesha kwamba inawezekana kabisa kujifunza ujuzi huu mpya ndani ya wiki 10 tu, ukaweza kutembea bila kuona kwa kutumia hisia za masikio. hata katika uzee wako.

Ukweli ni kwamba watu ambao hawaoni ama wamepoteza kuona wanaweza kutembea vizuri kwa kutumia hisia za kusikia za masikio tena bila mafunzo maalum limeonekana wazi kwa wanasayansi kwa muda mrefu.

Lakini vipi kwa watu wenye uwezo wa kuona kama mimi na wewe? wanaweza pia kufundishwa ujuzi huu na kuanza kutembea wakiwa wamefumba macho katika maeneo mbali mbali mtaaani bila mashaka yoyote?

Ili kujibu swali hili na mengine, timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Durham ilikusanya kikundi cha watu wenye umri mchanganyiko cha watu 26 wa kujitolea: 12 walikuwa vipofu na 14 walikuwa hawana matatizo ya kuona, wanaona kama kawaida.

Tofauti na popo, ambao huchanganua mazingira yao kwa kutoa mawimbi mafupi ya ultrasonic (na kuokota ishara iliyoakisiwa), washiriki katika jaribio hilo walizoezwa kufanya vivyo hivyo kwa usaidizi wa kupiga ndimi zao.

Kulingana na mwandishi mkuu wa utafiti huo, Lore Thaler, profesa wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Durham, matokeo yalikuwa ya kuvutia sana kwamba hakuna utafiti mwingine unaohusisha kipofu katika kumbukumbu yake umepata jibu la shauku kama hilo.

Mafunzo ya kina - mara mbili kwa wiki, kwa saa mbili hadi tatu - ilidumu kwa miezi miwili na nusu.

Darasani, masomo yalifundishwa katika giza kubwa, walitumia ndimi zao, kusikiliza mwangwi ulioakisiwa - na kujua hitimisho kwa msingi wake. Hasa, kuamua ukubwa na sura ya chumba, vitu vilivyomo - na kwenda mahali walipotakiwa kwenda, wakijaribu kugusa vitu hivyo.

Baada ya kuchambua matokeo ya wataalam hawa, watafiti walihitimisha kuwa inawezekana kwa wale wazoefu kutembea gizani ingawa kwa ubora kidogo kuliko wale wapya waliofunzwa. Katika suala la kuamua sura na ukubwa wa vitu, vikundi vyote viwili wale wapya na wale wazoefu vilifanya karibu kwa usawa.

Inafurahisha, uwezo wa kujifunza ustadi huu wa kigeni uligeuka kuwa hauhusiani na uzee. Wanawake wawili wazee - wenye umri wa miaka 72 na 79 - walishiriki katika utafiti, na wote walipewa mafunzo kwa usawa na watu wengine wa kujitolea.

Wenye umri mdogo walikuwa naumri kati ya miaka 21-22, waliruhusu washiriki wengine pia lakini, kama waandishi wa kazi iliyochapishwa kwenye jarida la PLOS kumbuka, kwa majaribio, kama matokeo ya mafunzo, tabia ya washiriki wote ilibadilika na kuwa moja.

Hata hivyo, waandishi wa utafiti huo wanakubali kwamba kiwango chake ni kidogo sana kufikia hitimisho la uhakika.