Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tanzania: Kituo cha utafiti chabuniwa kudhibiti ugonjwa wa malaria
Ugonjwa wa Malaria unachangia kwa kiasi kikubwa kwenye maradhi na vifo vya watoto Kusini mwa jangwa la Afrika.
Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, inakadiriwa kuwa watoto 260,000 chini ya umri wa miaka mitano hufa kila mwaka kwa ugonjwa wa Malaria.
Nchini Tanzania, watafiti wametengeneza mji maalumu, mahususi kwa ajili ya kuchunguza aina mbalimbali ya mbu, ambapo huwalisha damu na kisha kutafiti jinsi gani wanaweza kuwadhibiti na kuwaangamiza wale waenezao malaria.
Mwandishi wa BBC, Alfred Lasteck alifika kwenye mji huo maarufu ‘Mosquito City’, uliopo Kusini Mashariki mwa Tanzania kujionea jinsi gani tafiti hizo zinavyofanyika.