Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Alhamisi: Palace wanaweza kupokea ofa kwa Mateta
Crystal Palace wako tayari kusikiliza ofa za majira ya kiangazi kwa Jean-Philippe Mateta ikiwa hawatafikia makubaliano mapya na mshambuliaji huyo wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 28. (Sun)
Napoli wanamlenga kiungo mpya Januari na chaguo lao la kwanza ni kiungo wa Manchester United Kobbie Mainoo, Muingereza mwenye umri wa miaka 20. (Gazzetta dello Sport)
Brighton wanaweza kumsajili mlinzi wa Cologne Said El Mala, Mjerumani mwenye umri wa miaka 19, Januari kwa dili linaloweza kugharimu hadi euro milioni 35 (£30.6m). (Teamtalk)
Manchester United, Liverpool na Chelsea pia wanavutiwa na El Mala, huku United wakitajwa kuwa "chaguo linalofaa zaidi". (Talksport)
Fulham italazimika kulipa AC Milan euro milioni 28 (£24.5m) ili kufanya uhamisho wa mkopo wa winga wa Nigeria Samuel Chukwueze, mwenye umri wa miaka 26, kuwa wa kudumu. (Calcio Mercato )
Manchester United, Arsenal na Real Madrid wanawania saini ya mlinzi wa Eintracht Frankfurt Nathaniel Brown, Mjerumani mwenye umri wa miaka 22. (Bild)
Tottenham, Newcastle na Aston Villa wanaweza kumfukuzia mshambuliaji wa Brentford Igor Thiago, Mbrazili mwenye umri wa miaka 24, Januari. (Caught Offside)
Mshambuliaji wa Mexico Santiago Gimenez anaweza kuondoka AC Milan Januari huku West Ham na Sunderland wakivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport)
West Ham wanamfuatilia kwa karibu mlinda lango wa Wolves José Sá, Mreno mwenye umri wa miaka 32, kuelekea dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)
Eintracht Frankfurt hawafanyi tena kazi ya kumsajili Niclas Füllkrug wa West Ham Januari, lakini klabu nyingine za Bundesliga bado zinavutiwa na mshambuliaji huyo wa Ujerumani, ikiwemo Wolfsburg. (Florian Plettenberg)
Roma wanamlenga mshambuliaji wa Tottenham Mathys Tel, Mfaransa mwenye umri wa miaka 20, kama mbadala wa mshambuliaji wa Manchester United Joshua Zirkzee, raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24. (Ekrem Konur)
Newcastle wanamfuatilia kiungo wa Morocco Bilal El Khannouss, mwenye umri wa miaka 24, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Stuttgart kutoka Leicester City. (Teamtalk)
Chelsea wana imani ya kukamilisha dili za kiungo wa Lille Ayyoub Bouaddi, Mfaransa mwenye umri wa miaka 18, na mshambuliaji chipukizi wa Metz Brian Madjo, Mluxembourg mwenye umri wa miaka 16. (Caught Offside)
Barcelona wanajaribu kumsajili mshambuliaji mwenye kipaji mkubwa JJ Gabriel, Muingereza mwenye umri wa miaka 15, kutoka Manchester United. (Sun)