Je, ushindi wa medali ya dhahabu una thamani gani?

Gold, silver and bronze medals from the Paris Olympics

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Washindi wa michezo mwili tu, mbio na ndondi ndio ambao watapata zaidi ya medali
Muda wa kusoma: Dakika 5

Wakati Michezo ya Olimpiki ya kisasa ilipoanza huko Athene, Ugiriki mwaka 1896, ilikuwa ni michezo ya kujifurahisha bila wanamichezo wataalamu au tuzo za pesa.

Lakini jijini Paris, Ufaransa msimu huu wa kiangazi, baadhi ya wana michezo huenda wakapata pesa, kwa wale ambao watashinda katika Olimpiki hiyo.

Wana michezo ya Olimpiki wanaweza kupata pesa kutoka vyanzo mbalimbali; wafadhili, tuzo za kifedha zinazotolewa na nchi zao, na sasa kwa mara ya kwanza, tuzo za pesa zinazotolewa kwenye mashindano yenyewe.

Lakini si kila mchezo utapata pesa, na hilo limesababisha mabishano kuhusu njia bora ya kugawanya mapato ambayo michezo hiyo inazalisha.

Ndondi na mbio tu

Julien Alfred celebrates after crossing the finishing line in a race

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Julien Alfred atabeba kitita cha dola za kimarekani 50,000 pia na medali yake ya dhahabu baada ya kushinda mbio za mita 100 kwa wanawake

Kati ya michezo 32 iliyoshindaniwa huko Paris 2024, zawadi ya pesa itatolewa katika michezo miwili tu - mbio na ndondi.

Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Mbio, lilitoa tangazo la kushangaza mwezi Aprili kwamba washindi wa medali za dhahabu huko Paris 2024, watapokea dola za kimarekani 50,000 kwa atakayeshinda.

Mwezi mmoja baadaye, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBA), lilisema pia litatoa zawadi ya dola 100,000 kwa mabingwa wa Olimpiki - ingawa robo moja ya pesa hizo itakwenda kwa mashirikisho ya kitaifa ya wakimbiaji na robo nyingine kwa makocha wao.

Katika michezo yote miwili, washindi wa medali za fedha na shaba watapata kiasi kidogo cha pesa, huku washindi katika ndondi wakituzwa hadi mshindi wa tano.

Zawadi ya pesa hazitoki moja kwa moja kutoka kamati ya Olimpiki, bali kutoka kwa mashirika mbalimbali yanayosimamia michezo hiyo.

Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Mbio linatumia baadhi ya fedha ambazo inapokea kutoka kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), kama sehemu ya mapato yanayotokana na Michezo ya Olimpiki. Hapo awali, pesa hizi zilitumika zaidi katika maendeleo ya wakimbiaji.

Pesa zitawasaidia?

A fencer in mask with a Singapore flag on it competes with an athletes with a US flag on his mask

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wana michezo kutoka Singapore watapokea bonasi kubwa zaidi kutoka nchini kwao kuliko wa Marekani
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Olga Korbut, nguli wa mazoezi ya viungo wa Sovieti ambaye alishinda medali nne za dhahabu na mbili za fedha wakati wa maisha yake ya Olimpiki, alilazimika kuuza medali zake tatu kwa dola 333,500 mnamo 2017.

Kuna njia nyingine nyingi ambazo wanamichezo hupata pesa. Wengi huzawadiwa na nchi zao. Singapore inaaminika kuwa ndio taifa linalotoa zawadi zaidi, kila mmoja wa washindi wa medali za dhahabu hupata dola 750,000.

Kwa wenyeji, Ufaransa, washindi hupewa dola 87,000. Wanamichezo wa Morocco wako juu zaidi kwani hupewa dola 200,000. Marekani kupitia mfuko wake wa "Operation Gold" hutoa dola 37,500.

Baadhi ya nchi, kama vile Uingereza, hazitoi zawadi yoyote ya fedha.

Timu ya GB hutoa ufadhili kwa wanariadha wakati wa kuelekea katika Olimpiki na wale wenye nafasi kubwa ya kushinda dhahabu hupata hadi dola 28,000 kwa mwaka.

Ingawa pesa hizi si kidogo lakini haziwafanyi wana michezo hao kuwa matajiri, kama wale wanamichezo matajiri maarufu duniani.

Changamoto za kifedha

LeBron James on court playing for the USA

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani, LeBron James ni moja ya wachezaji wanaolipwa zaidi

Mcheza gofu wa Uhispania Jon Rahm ndiye mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi Paris 2024 kulingana na orodha ya kila mwaka ya matajiri wa michezo iliyochapishwa na Forbes.

Jarida hilo linakadiria kuwa alipata dola milioni 218 mwaka uliopita, huku pesa nyingi zikitoka katika safari ya gofu ya LIV iliyofadhiliwa na Saudia.

Haishangazi, mchezaji wa pili anayelipwa vizuri zaidi ni nyota wa mpira wa vikapu wa Marekani - Lebron James. Anaaminika kulipwa dola milioni 128.

Kwa wana michezo wa chini, kushinda medali katika Olimpiki kunaweza kuwasaidia kuwapa nyongeza inayohitajika katika mapato yao. Mara nyingi huwa na mikataba inayosema watapokea bonasi kutoka kwa wafadhili ikiwa watashiriki na kushinda.

Mikataba hii mara nyingi ni siri, lakini ilifichuliwa wakati wa mzozo wa kisheria kati ya Nike na New Balance mwaka 2016, mwanamichezo wa Marekani Boris Berian alitarajia kupokea dola 150,000 ikiwa angeshinda dhahabu kwenye Olimpiki.

Kuna wanariadha wengi ambao wanatatizika kufanikiwa. Utafiti uliofanywa nchini Australia miaka michache iliyopita uligundua 40% ya wana michezo ya Olimpiki ya 2032 wanafanya kazi za muda au wameajiriwa mikataba ya kudumu.

Utafiti wa hivi karibuni wa Kamati ya Olimpiki na Olimpiki ya Walemavu ya Marekani uligundua 26.5% ya wana michezo wake wa sasa wanapata chini ya dola 15,000 kwa mwaka.

The Eiffel Tower seen from below with Olympics rings on it

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kila medali inayotolewa huko Paris ina sehemu ndogo ya chuma cha mnara wa Eiffel

Medali ya mshindi wa mwaka huu ina gramu 505 za fedha na gramu sita za dhahabu (medali za dhahabu sio dhahabu tupu tangu 1912) na thamani yake ni dola 950.

Lakini mabingwa wa Olimpiki wa Paris watakuwa na matumaini kwamba kumbukumbu zao za ushindi zitakuwa na thamani zaidi.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah