Rais wa Afrika mwenye umri wa miaka 91 ambaye anaendelea kukaidi waandishi wa habari za vifo

Muda wa kusoma: Dakika 6

Paul Melly

Mchambuzi wa Afrika

TH

Chanzo cha picha, AFP

Uvumi kuhusu hali ya kiafya na mahali alipo Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 91 umekuwa gumzo barani Afrika wiki hii.

Baada ya kuhudhuria mkutano wa kilele wa China na Afrika mjini Beijing mwanzoni mwa Septemba, labda haikuwa ajabu kwamba alikosa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York.

Lakini alipokosa kuhudhuria mkutano wa kilele wa wiki hii wa nchi zinazozungumza Kifaransa (La Francophonie) huko Viller Cotterêts, kaskazini mwa Paris, uvumi huo ulianza kupita kiasi, kwani hakuwa ameonekana hadharani kwa takriban mwezi mmoja.

Balozi wa Cameroon nchini Ufaransa alisisitiza kuwa Biya yuko "katika afya njema" na yuko Geneva - kituo chake cha kawaida anapokuwa nje ya nchi.

Vyanzo vingine vilipendekeza hii ni kwa sababu alihitaji kupumzika chini ya uangalizi wa matibabu baada ya ratiba nzito ya kidiplomasia mnamo Julai na Agosti.

Isitoshe, yeye ndiye mkuu wa nchi mwenye umri wa juu zaidi barani Afrika na wa pili kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi, akishindwa katika rekodi hiyo na Rais Teodoro Obiang Nguema wa nchi jirani ya Equatorial Guinea.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Dalili kama hizo za kawaida hazikutosha bado kufahamu kuhusu Biya katika vyombo vya habari vinavyovutiwa na masuala ya Afrika na duru za kisiasa.

Hivyo hatimaye msemaji wa serikali, René Sadi, alikanusha rasmi uvumi huo, na kuongeza kuwa rais atarejea nyumbani "katika siku chache zijazo".

Na mkuu wa ofisi ya kibinafsi ya rais, pamoja naye huko Geneva, alisisitiza kuwa ypo kayika hali "bora ya kiafya".

Cameroon ipo katika eneo muhimu la kimkakati, kama lango la kuelekea Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) zisizo na ufikiaji wa bahari.

Mbali na kujitahidi kukandamiza kikamilifu vurugu za wanajihadi katika Ziwa Chad, pia inapambana na mgogoro tata na mara nyingi wenye vurugu katika maeneo yake yanayozungumza Kiingereza.

Katika kuongoza majibu ya changamoto hizi, Biya ameleta mtindo wa kibinafsi usio wa kawaida ambao mara nyingi huepuka kumweka mbele ya jukwaa, bila hitaji lolote la kibinafsi la kujihusisha na uwasilishaji wa kidiplomasia au mkutano wa kilele wa utendaji.

Yeye ni mtu asiyehudhuria mikutano mingi ya viongozi wa Kiafrika.

Unaweza Pia Kusoma
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wafuasi wa rais Biya wanamtaka awanie muhula mwingine wa miaka saba katika uchaguzi wa mwaka ujao

Hata nyumbani, kwa hotuba yake iliyopimwa na sauti ya tahadhari, Biya kwa miaka mingi amedhibiti kujihusisha kwake binafsi katika masuala ya nchi , kwa kiasi kikubwa akikabidhi uendeshaji wa kila siku wa serikali, na kushughulikia ripoti za kiufundi, kwa msururu wa mawaziri wakuu ambao wamehudumu katika serikali zake.

Ukosefu usioelezeka kutoka kwa maoni ya umma umekuwa kitu cha kawaida kwa marais hawa wa ajabu zaidi.

Uvumi kwamba amekufa huibuka mara kwa mara, haswa kwa sababu ya kutoweka bila kutangazwa machoni pa umma .

Lakini mtindo huu wa hali ya chini unapingana na dhamira aliyoitumia kuwasili kwake madarakani mwaka 1982, akimweka kando mtangulizi wake Ahmadou Ahidjo, akiahidi mabadiliko huria kabla ya kushikilia urais kwa kiasi kwamba hakuna mpinzani au kampeni ya maandamano iliyofanikiwa kumtikisa .

Wakati wimbi la mabadiliko ya demokrasia ya vyama vingi lilipoenea katika sehemu kubwa ya Afrika mwanzoni mwa miaka ya 1990, Biya alikuwa mmoja wa viongozi kadhaa waliokuwa madarakani kubadilisha mkondo kwa busara, kuruhusu mageuzi ya kutosha kuondoa joto katika maandamano makubwa huku akinendelea kudhibiti mamlaka kwa nguvu .

Tangu ushindi mdogo wa uchaguzi mwaka 1992, amefaulu kushinda changamoto za kisiasa zilizofuata, akisaidiwa labda na uchakachuaji wa kura na kwa hakika na migawanyiko kati ya wapinzani ambao mara nyingi hawana mbinu ya kumuondoa madarakani.

Sasa, huku muhula wa sasa wa Biya wa miaka saba ukifika mwisho mnamo Novemba 2025, wafuasi wake wamekuwa wakimshinikiza kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 91 agombee tena.

Wakosoaji wanahisi kuwa ni muda sasa kwa uongozi wa kitaifa wa Cameroon kutwaliwa na kizazi kipya ambacho kinaweza kushughulikia matatizo ya kitaifa na kutafuta fursa za maendeleo na ustawi kwa kasi na nguvu zaidi.

Mnamo mwaka wa 2016 walimu na mawakili katika mikoa miwili hasa inayozungumza Kiingereza, Kusini-Magharibi na Kaskazini-Magharibi, walipinga hatua ya serikali kushindwa kutoa rasilimali ipasavyo za haki za lugha ya Kiingereza na huduma za umma.

Ikiwa Biya angejibu kwa haraka zaidi na kwa mpango wa mageuzi wenye ukaribu na utu zaidi na uliopigiwa debe kwa sauti kubwa, labda angeweza kupunguza malalamishi hayo mapema - na hivyo kuepusha hali ya makabiliano makali kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wenye silaha wanaodai kujitenga moja kwa moja.

Biya baadaye alileta mageuzi - ili kukidhi malalamiko ya mikoa inayozungumza Kiingereza na, nchi nzima, kupeleka madaraka kwa mabaraza ya kikanda.

Lakini wakati mwingine wananchi wamekabiliwa na hali ya kuhitajika kusubiri kwa muda mrefu kabla ya serikali kushughulikia matatizo yao - miundo ya ugatuzi haikuanzishwa hadi miaka mingi baada ya sheria ya mfumo wa awali kupitishwa.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cameroon imekumbwa na uasi wa kujitenga katika sehemu nyingi zinazozungumza Kiingereza nchini humo

Baadhi ya Wacameroon, hata hivyo, wameridhishwa na mbinu ya Biya - kwa uongozi na utayari wake wa kuwaacha mawaziri wakuu kushughulikia maamuzi ya kawaida.

Wanaona jukumu lake kama ishara na hata , inayofananishwa na ya mfalme wa kikatiba.

Hakika, jukumu hili la uwakilishi ni mwelekeo wa urais ambao ameonekana kuwa na urahisi nao.

Mnamo tarehe 15 Agosti, kwa mfano, alikuwa Boulouris, huko Côte d'Azur huko Ufaransa, ambapo alitoa hotuba ya kina ya dakika 12 katika ukumbusho wa kutua kwa Washirika wa 1944 kukomboa Ufaransa kusini kutoka kwa Wanazi - operesheni ambayo askari wengi kutoka maeneo ya Afrika ya Ufaransa walishiriki.

Na kwa hakika, licha ya kutokuwepo mara kwa mara katika mji mkuu wa Cameroon Yaoundé - kwa kawaida hurejea kijijini kwake kusini mwa nchi ,eneo lenye msitu au katika kituo anachopendelea cha kimataifa, Hoteli ya Intercontinental ya Geneva - Biya ameendelea kufanya maamuzi muhimu ya kisiasa na ya kimkakati.

Mlinda ngome mkuu wa mamlaka katika ikulu ya Étoudi ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Ferdinand Ngoh Ngoh.

Mfumo wa mamlaka ambapo Biya, kama mkuu wa nchi, huweka 'kadi zake karibu na kifua chake' (mipango yake kuwa siri) bila shaka huzua uvumi kuhusu nia yake mwenyewe kwa uchaguzi wa 2025 na kuhusu warithi wanaotarajiwa.

Lakini baadhi ya vigogo wa serikali kuu wanaodokezwa mara nyingi, kuwa warithi wake kama vile Laurent Esso na René Sadi, kwa sasa wao wenyewe hawawezi kuitwa kuwa vijana

Vikundi vya usaidizi pia vimeonekana kuhamasisha kupitishwa kwa mwenge kwa mtoto mkubwa wa rais Franck Biya, mfanyabiashara - ingawa Franck mwenyewe hajawahi kuonyesha nia yoyote katika siasa au kutoa dokezo lolote la matarajio hayo.

Lakini katika Afrika ya leo, ambapo kutoridhika na mwamko wa kisiasa kumekithiri, hasa miongoni mwa vijana wa mijini, majaribio ya watawala kundeleza siasa za urithi yanaweza kuzua hatari.

Katika nchi jirani ya Gabon, Rais Ali Bongo aliondolewa madarakani na jeshi mwaka jana baada ya serikali kuendesha uchaguzi wa 2023 ili kumpa muhula wa miaka saba zaidi licha ya hali yake ya kiafya kuwa dhaifu.

Na wakati Rais wa Senegal Macky Sall alipomchagua Waziri Mkuu wake Amadou Ba kama mrithi wake, alipingwa vikali na wapiga kura ambao walimchagua mpinzani mwenye umri mdogo na mwanamageuzi Bassirou Diomaye Faye .

Biya na washirika wake wa ndani wanaweza kuhisi ujasiri wa kuepuka hali kama hizo. Lakini hiyo itahitaji usomaji wa busara wa hisia za wengi haswa miongoni mwa vijana na watu wa tabaka la kati katika miji mikubwa kama vile Yaoundé na Douala.

Unaweza Pia Kusoma

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah