Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ongezeko la joto duniani latarajiwa kupita kiwango cha nyuzijoto 1.5C kwa mara ya kwanza
Ulimwengu wetu wa joto kupita kiasi huenda ukapita kikomo muhimu cha halijoto kwa mara ya kwanza katika miaka michache ijayo, wanasayansi wanatabiri.
Watafiti wanasema sasa kuna uwezekano wa 66% wa kuvuka kiwango cha ongezeko la joto la 1.5C kati ya sasa na 2027.
Uwezekano huo unaongezeka kutokana na hewa chafu kutoka kwa shughuli za binadamu na uwezekano wa hali ya hewa ya El Niño baadaye mwaka huu.
Ikiwa ulimwengu utapita kiwango hicho cha ukomo, wanasayansi wanasisitiza huku wakiwa na wasiwasi, hali hiyo inaweza kuwa ya muda mfupi.
Kufikia kiwango hicho kunaweza kumaanisha kuwa dunia ina joto la 1.5C kuliko ilivyokuwa katika nusu ya pili ya Karne ya 19, kabla ya uzalishaji fueli za visikuku kutoka kwa ukuaji wa viwanda kuanza kuongezeka.
Na kupita kiwango hicho cha ukomo hata kwa mwaka mmoja tu ni ishara ya wasiwasi kwamba ongezeko la joto linaongeza kwa kasi na sio kupungua.
Kiwango cha joto cha 1.5C imekuwa ishara ya mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Nchi zilikubali "kuendeleza juhudi" za kupunguza viwango vya joto duniani hadi 1.5C chini ya makubaliano ya 2015 ya Paris.
Kupita zaidi ya kiwango cha 1.5C kila mwaka kwa muongo mmoja au miwili kunaweza kusababisha athari kubwa zaidi za ongezeko la joto, kama vile joto kali, dhoruba kali zaidi na moto wa nyikani.
Lakini kupita kiwango hicho katika moja ya miaka michache ijayo haimaanishi kuwa kikomo cha Paris kilikuwa kimepita.
Wanasayansi wanasema bado kuna wakati wa kuzuia ongezeko la joto duniani kwa kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa mazingira.
Tangu 2020 Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni limekuwa likitoa makadirio ya ulimwengu kupita kiwango cha nyuzijoto cha 1.5C katika mwaka wowote ule.
Hapo nyuma walitabiri kulikuwa na chini ya 20% ya uwezekano wa kupita kiwango hichi cha 1.5C katika miaka mitano ijayo.
Kufikia mwaka jana hii ilikuwa imeongezeka hadi 50%, na sasa imepita hadi 66%, ambayo wanasayansi wanasema inamaanisha kuwa "ina uwezekano mkubwa wa kutokea."
Je, kupita zaidi ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi inamaanisha nini?
Kielelezo si kipimo cha moja kwa moja cha halijoto ya dunia bali ni kiashirio cha kiasi gani ama kikubwa au kidogo Dunia imepata ongezeko la joto au kupungua ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu wa kimataifa.
Wanasayansi hutumia wastani wa data ya halijoto kutoka kipindi cha kati ya 1850-1900 kama kipimo cha jinsi kiwango cha joto ulimwenguni kilivyokuwa kabla ya utegemezi wetu wa kisasa wa makaa ya mawe, mafuta na gesi.
Katika miongo michache iliyopita ulimwengu wetu wa joto kupita kiasi umesongesha zebaki juu, hivi kwamba katika 2016, joto zaidi kuwahi kurekodiwa, halijoto ya kimataifa ilikuwa 1.28C takwimu hizo zikiwa za juu ya kabla ya viwanda.
Sasa watafiti wanasema takwimu hizo zimepangwa kuongezeka zaidi - wana uhakika wa 98% kiwango cha juu zaidi kitafikiwa kabla ya 2027.
Na katika miaka kati ya sasa, wanaamini kuna uwezekano mkubwa sana wa kikomo cha 1.5C kuongezeka kwa mara ya kwanza.
"Kwa kweli sasa tuko ndani ya uwezekano wa kupita kiwango cha joto 1.5C kwa muda mfupi kwa mwaka, na hiyo ni mara ya kwanza katika historia ya wanadamu kuwa karibu kiasi hicho," Prof Adam Scaife, mkuu wa utabiri wa masafa marefu katika Ofisi ya Shirika la Hali ya hewa ambaye hukusanya data kutoka kwa mashirika ya hali ya hewa duniani kote, alisema.
Watafiti wanasisitiza kuwa halijoto italazimika kuwa katika kiwango cha kuzidi nyuzijoto 1.5C kwa miaka 20 ili kuweza kusema kiwango cha makubaliano ya Paris kimefaulu.
"Ripoti hii haimaanishi kuwa tutapita kabisa kiwango cha 1.5C kilichoainishwa katika Mkataba wa Paris ambao unahusu ongezeko la joto la muda mrefu kwa miaka mingi," alisema Katibu Mkuu wa WMO Prof. Petteri Taalas
"Hata hivyo, WMO inatoa tahadhari kwamba tutapita kiwango cha 1.5C kwa muda mfupi ikiambatana na kuongezeka kwa kasi," alisema.
Je, El Niño italeta tofauti gani?
Kuna mambo mawili muhimu - kwanza ni kuendelea kwa viwango vya juu vya uzalishaji wa kaboni kutokana na shughuli za kibinadamu ambazo licha ya kupungua wakati wa janga la corona bado zinaendelea.
Sehemu ya pili muhimu, ni uwezekano wa kutokea kwa El Niño, hali ya hewa yenye athari za kimataifa.
Kwa miaka mitatu iliyopita dunia imekuwa ikishuhudia hali ya hewa ya La Niña ambayo imechangia katika kumepunguza ongezeko la joto kwa kiasi fulani.
Lakini joto la ziada ambalo El Niño italeta kwenye uso wa Pasifiki huenda likaongeza halijoto ya kimataifa hadi kiwango kipya cha juu zaidi mwaka ujao.
Hata hivyo bado kuna kutokuwa na uhakika kuhusu kuanza kwa tukio hilo na ukubwa wake.
"Inafaa kuzingatia kwamba utabiri wetu mwingi ambao unafanywa sasa kwa El Niño, ambayo tunadhani inaendelezwa msimu huu wa baridi, unaonyesha uwezekano wa juu wa kutokea," Prof Scaife aliwaambia wanahabari.
"Lakini kwa kweli kutabiri ukubwa, au tukio linalofuata ndani ya kipindi cha miaka mitano, hatuwezi kutoa tarehe kamili ya hayo zaidi ya mwaka huu ujao, kwa hivyo inaweza kuwa katika miaka mitatu au minne kutoka sasa, tukafika hadi kiwango cha mbili na nusu cha digrii ya El Niño, na hiyo ndio inayoweza kuwa inasababisha hilo."